Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na Mashababu (Wanachama wa Hizb) Hasa kwa Mnasaba wa Sikukuu ya Idd al-Adha 1447 H Sawia na 2026 M

(Imetafsiriwa)

Sifa zote njema zote zinamstahiki Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimshukie Mtume Wake, jamaa zake, maswahaba zake, na wale wanaomfuata.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Alhamd

Kwa Ummah wa Kiislamu kwa jumla, umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu unaoamrisha mema na kukataza maovu na kumwamini Mwenyezi Mungu Al Aziz Al Hakim:

Kwa wabebaji wa Dawah haswa, Mwenyezi Mungu alete ushindi kwa mikono yao na Yeye (swt) awasaidie kusimamisha dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Kwa wageni waheshimiwa wanaozuru ukurasa huu, wale wanaotafuta kheri unaotoa, wakifanya juhudi za kusimama na haki na kuwaunga mkono watu wake.

Kwenu nyote, Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Ninawapongeza nyote kwa Idd al-Adha iliyobarikiwa kwa mwaka 1447 H. Ninamuomba Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz (Mwenye Nguvu na Mwenye Uwezo) kwamba Idd hii iwe ufunguzi wa kheri na baraka kwa Waislamu wote.

Wapendwa ndugu na dada: Idd hii inakuja huku uvamizi wa Mayahudi, unaoungwa mkono na Amerika na silaha zake, ukiendelea dhidi ya Gaza (Hashim) na Palestina yote. Watawala katika nchi za Kiislamu wanaangalia kinachoendelea, wakiwahesabu mashahidi (shuhadaa) na kuwaita wafu! Na bora zaidi kati yao ni wale wanaopatanisha kana kwamba hawaegemei upande wowote, lakini wako karibu zaidi na Mayahudi!

Na leo wameongeza uvamizi mwingine, mkali na wa kikatili zaidi dhidi yetu. Amerika na umbile la Kiyahudi walianzisha shambulizi kubwa la pamoja dhidi ya Iran, ambalo limekuwa likiendelea tangu lilipoanza Februari 28, 2026; yaani limekuwa likiendelea kwa miezi mitatu dhidi ya Iran, Lebanon, na maeneo ya jirani! Na sasa umbile la Kiyahudi linaanzisha eneo la ulinzi kusini mwa Lebanon, kama vile lilivyofanya Gaza (Hashim), huku watawala wa ulimwengu wa Kiislamu wakisimama kimya! Treni ya Trump ya kuhalalisha mahusiano iliregea kwa kasi nchini Lebanon ili kuzifikia nchi zengine ambazo zimehalalisha mahusiano na Mayahudi. Mazungumzo ya khiyana yanafanyika bila aibu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waumini! Hata makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 10 na wiki 3…

Makubaliano ya kusitisha mapigano waliyodai nchini Lebanon yamekanyagwa chini ya miguu na umbile la Kiyahudi, ambalo limezidisha mashambulizi yake. Vile vile, makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku 45 yaliyotangazwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani mnamo Ijumaa, 15/5/2026, kati ya umbile la Kiyahudi na Lebanon—“Israel na Lebanon zimekubaliana kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa siku 45” - si lolote zaidi ya wino kwenye karatasi kwa umbile la Kiyahudi. Mashambulizi yanaendelea kuongezeka bila kujali makubaliano haya yanayodaiwa. “Leo, Jumapili, “Israel” ilifanya mashambulizi mawili ya anga nje kidogo ya miji ya Yahmar na Sahmar katika Bonde la Bekaa Magharibi mashariki mwa Lebanon, pamoja na mashambulizi ya anga katika mji wa Zawtar al-Sharqiya kusini mwa Lebanon.” (Al Jazeera, 17/5/2026). Bila shaka, umbile la Kiyahudi halifanyi mashambulizi ya anga bila idhini ya Trump, ambaye alitangaza makubaliano ya amani! Hivyo, hakuna mchana au usiku unaopita bila uvamizi hapa na pale, huku watawala wa nchi za Kiislamu wakiwazunguka, lakini wanabaki kimya kama kimya cha makaburi, kana kwamba yanayotokea yako nchi fulani ya mbali na hayawahusu lolote. Hukumu yao ni mbaya ilioje

Baada ya kurudi kutoka ziara yake nchini China, Trump aliendelea kuufunga Mlango Bahari wa Hormuz, akitoa vitisho na maonyo: “Rais wa Marekani Trump alitishia Iran mnamo Jumapili kwa matokeo mabaya ikiwa viongozi wake hawatachukua hatua haraka. Trump aliandika katika chapisho kwenye jukwaa la ‘Truth Social’: “Saa Inasonga” kwa Iran kukubali makubaliano ya amani, na “hakutakuwa na chochote kilichobaki” ikiwa viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu “hawatasonga mbele, kwa KASI.” (Al Arabiya, 17/5/2026). “Kisha rais wa Marekani akarudia vitisho vyake vya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran. Alidokeza katika chapisho kwenye jukwaa la ‘Truth Social’ mnamo Jumatatu kwamba mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iran yanaweza kutoka pande zote...” (AP News, 18/5/2026). Aliendelea na kiburi chake, akisema: “Katika muktadha huo huo, Trump alisisitiza kwamba vikosi vya Marekani vilikuwa vimeangamiza kwa kiasi kikubwa jeshi la Iran na uongozi wake wa kisiasa, akisisitiza kwamba Marekani haitaruhusu Iran kwa hali yoyote kutengeneza silaha ya nyuklia.” (Middle East Online, 20/5/2026).

BBC ilichapisha katika taarifa yake mpya mnamo 21/5/2026, “Trump aliwaambia waandishi wa habari katika Kituo cha Jeshi la Anga cha Andrews, alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mazungumzo na Iran, kwamba yalikuwa kwenye njia panda. Aliongeza, “Niamini, ikiwa hatutapata majibu sahihi, yatakwenda kwa haraka sana. Sote tuko tayari kwenda” Itabidi iwe majibu mazuri 100%. (ilisasishwa na BBC mara ya mwisho, 21/5/2026). Anataka mazungumzo kwa masharti yake, au kama anavyosema kila mara: “Mazungumzo na Iran yamefikia hatua zake za mwisho, lakini alionya wakati huo huo kwamba kushindwa kwa mazungumzo hayo kutasababisha mashambulizi zaidi.” (Iran International, 21/5/2026).

Hivyo, Trump anataka mazungumzo yaendelee kulingana na kiburi chake cha “amani kupitia nguvu”! Anamsukuma mshirika wake wa karibu Netanyahu kuendelea na uharibifu na uvamizi, akilimakinisha umbile la Kiyahudi, kama tulivyosema hapo awali, akiwa na kambi mpya kwa ajili ya jeshi lake katika vijiji vya Lebanon vilivyokuwa linavyovikalia kimabavu, akivitangaza kuwa eneo la ulinzi, hivyo kurudia “hali” ya Gaza na Hamas na mstari wa manjano! Inaonekana kwamba kiburi cha Trump kwa madai yake ya amani kupitia nguvu kimeleta rasimu ya makubaliano yenye dosari kama utangulizi wa mazungumzo au majadiliano ambayo yataendelea kwa miezi miwili au zaidi, kama ilivyoripotiwa na mashirika ya habari mnamo Jumapili, 24/5/2026.

Ni dhambi kubwa kwamba Trump anaanza, anasimamisha, au anamaliza mapigano apendavyo, bila kujali damu aliyomwaga, nyumba alizoharibu, na miundombinu aliyoivunja. Yote haya ni kwa sababu hajapata nchi ya Kiislamu ya kuzuia mipango yake na kumpa funzo, kama ilivyowatokea watangulizi wake, Wafursi na Warumi. Hata mshirika wake wa karibu Netanyahu anafuata mpango na amri za Trump za kuangamiza watu, miti, na mawe huko Palestina, Lebanon, na maeneo ya jirani!!

Kwa kumalizia, watawala wa ardhi za Kiislamu wanawatukuza wakoloni makafiri badala ya kumtukuza Mola wa Walimwengu. Badala ya kuikomboa Palestina na kuliondoa umbile la Kiyahudi, wanatafuta kujadili na kuhalalisha mahusiano nalo. Watawala hawa wanashirikiana na Amerika na mrithi wake, umbile la Kiyahudi, ili kumfurahisha Trump! Hivyo, wanapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ili kumfurahisha dhalimu Trump. Wamesahau, au wanajifanya kusahau maneno ya Mtume (saw):

«مَنْ أَسْخَطَ اللَّهَ فِي رِضَا النَّاسِ سَخِطَ اللَّهُ عَلَيْهِ، وأَسْخَطَ عَلَيْهِ مَنْ أرضاهُ فِي سَخَطِهِ، وَمَنْ أَرْضَى اللَّهَ فِي سَخَطِ النَّاسِ رَضِي اللَّهُ تَعَالَى عَنْهُ وَأَرْضَى عَنْهُ مَنْ أَسْخَطَهُ فِي رِضَاهُ حَتَّى يُزَيِّنَهُ وَيُزَيِّنَ قَوْلَهُ وَعَمَلَهُ فِي عَيْنِهِ»

“Yeyote anayemkasirisha Mwenyezi Mungu ili kuwaridhisha watu, Mwenyezi Mungu atamkasirikia, na atamkasirikia wale aliowaridhisha katika hasira yake. Na yeyote anayemridhisha Mwenyezi Mungu dhidi ya hasira za watu, Mwenyezi Mungu Mtukufu atamridhisha na atawafanya wale aliowakasirisha katika raha yake wafurahi naye, hadi ampambe na kuyapamba maneno na matendo yake machoni pake.”

(Imesimuliwa na At-Tabarani katika Al-Mu'jam Al-Kabir). Vile vile, watawala hawa hawatambui uzito wa kosa la uaminifu kwa makafiri na kwamba ni fedheha katika dunia hii na adhabu kali kesho Akhera.

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُون]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124]

Watawala hawa wamefikia hatua ya uaminifu kwa wakoloni wa makafiri kiasi kwamba ikiwa nchi yao yoyote itashambuliwa, zengine haziendi kuisaidia. Badala yake, bora kati yao ni wale wanaohesabu waliokufa na waliojeruhiwa! Kiasili, Waislamu ni Umma mmoja, amani yao ni moja, na vita vyao ni vimoja, kwa hivyo shambulizi katika sehemu yoyote ni shambulizi kwa wote. Lakini hili haliwezi kupatikana huku ardhi za Waislamu zimegawanyika na watawala katika nchi za Waislamu ni waaminifu kwa wakoloni makafiri. Lakini litapatikana kwa Khilafah Rashida inayowarudisha Waislamu kuwa Umma mmoja, inayomnusuru Mwenyezi Mungu na kutabikisha sheria zake. Kisha itashinda kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na itaangaza dunia kwa uadilifu wake na mapambano yake, na Mwenyezi Mungu ataitukuza kwa ushindi wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad: 7]

Kwa hivyo, itikieni wito wa Mwenyezi Mungu, enyi Waislamu, na fanyeni kazi pamoja na Hizb ut Tahrir kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt).

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُولَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55].

Na bishara njema ya Mtume Wake (saw) baada ya utawala wa kitenza nguvu tunaoishi ndani yake, kama ulivyo tajwa katika Hadith ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) iliyosimuliwa na Ahmad kutoka kwa Hudhayfah ibn al-Yaman:

«.. ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

“... Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu (ملكًا جبرية) na utakuwepo kwa muda apendao Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa apendapo kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha yeye (saw) akanyamaza.”

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].

Katika hitimisho la mwisho, namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Idd hii iwe ufunguzi wa kheri, baraka, na izza kwa Uislamu na Waislamu,

[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُون]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21].

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi Alhamd

Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

10 Dhul Hijjah 1447 H                                                                                  Your Brother

27/5/2026 M                                                                                   Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.