Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ukamataji wa Waislamu nchini Urusi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Vikosi vya usalama vilipandikiza kazi za SIM wakati wa upekuzi katika nyumba za Waislamu, kesi za kushiriki katika shirika la kigaidi zilitungwa, jamaa zao walisema katika malalamiko kwa wanaharakati wa haki za binadamu. Kwa jumla, watu 48 walizuiliwa wakati wa operesheni ya vikosi vya usalama huko Nalchik na Nartan, Kavkazsky Uzel (tovuti ya habari) iliripoti mnamo Juni 3, ikinukuu wanaharakati wa haki za binadamu.

"Ukamataji mithili ya huo pia ulifanywa katika familia 42 katika jiji la Nalchik na kijiji cha Nartan. Watu wote waliowekwa kizuizini ni Waislamu," - tovuti ya kituo hicho ilisema. Walalamikaji wanadai kuwa upekuzi huo ulifuata mtindo huo huo: wakati wa upekuzi wa nyumba zao, kadi za SIM zilipatikana na kuchukuliwa, ambazo, kulingana na wao, hazikuwa zao na zilipandikizwa na maafisa wa kutekeleza sheria, wanaharakati wa haki za binadamu waliripoti, wakichapisha picha za malalamiko hayo.

Siku hiyo hiyo, mwanamke mwingine Muislamu, wa tano, alikamatwa huko Kazan kwa tuhuma za kupangilia shughuli za Hizb ut Tahrir. Wanne waliotangulia walikamatwa mnamo Septemba mwaka jana.

Maoni:

Kukamatwa kwa Waislamu nchini Urusi si jambo geni, lakini kutokana na kuzuka kwa vita nchini Ukraine, wameanza kucheza dori mpya kwa mara ya kwanza. Kila wakati upande wa Urusi unaposhindwa kijeshi, mateso dhidi ya Waislamu kwa kisingizio cha "kupambana na ugaidi" yamekuwa aina ya njia ya kutokea au skrini ya habari ambayo inawapurukusha raia kutokana na kushindwa uwanjani.

Hivi ndivyo ilivyotokea wakati huu: mnamo Juni 1, Ukraine ilisubutu kufanya operesheni inayoitwa "Spider Web", ambapo takriban ndege 40 za kimkakati zilishambuliwa, na baadhi ya viwanja vya ndege vilivyoko Siberia, yaani mbali sana na mpaka na Ukraine. Hii iliwezekana shukrani kwa teknolojia ya kisasa - masanduku yenye droni yaliletwa na malori chini ya pazia la usafirishaji wa mizigo ya cargo.

Kadiri serikali ya Urusi inavyozidi kuzama katika vita hivi, ndivyo inavyozidi kupata maadui wa ndani. Kwa bahati mbaya, hivi pia ndiyo inavyoelezea kampeni ya hivi punde dhidi ya wahamiaji ambayo mamlaka imekuwa ikitekeleza tangu vita kuanza. Ni vigumu kutabiri ni kwa muda gani hii itaendelea, lakini kwa sasa idadi ya watu wa Urusi inafaulu kumeza simulizi hizi, na kiwango cha chuki dhidi ya Waislamu na wahamiaji kimeongezeka sana na dhahiri katika miaka ya hivi karibuni. Hii pia inaonekana katika ongezeko la idadi kubwa ya uhalifu wa kikatili unaofanywa kwa msingi wa chuki na raia wa Urusi.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.