- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Umebarikiwa kwa Nguvu, Umedhoofishwa na Mgawanyiko
(Imetafsiriwa)
Habari:
Pentagon yasema, Marekani haitaki kuendeleza vita na Iran baada ya kulipua maeneo yake 3 ya nyuklia. (AP News)
Maoni:
"Pentagon yasema Marekani haitaki kuanzisha vita na Iran" - hii, baada ya kudondosha mabomu kumi na nne aina ya bunker-buster kwenye vituo vitatu vya nyuklia ndani ya ardhi ya Iran. Kauli kama hiyo si ya kinafiki tu - ni ya kuchukiza. Inaakisi mawazo ya kiburi, ya kikoloni. Mtu yeyote mwenye akili timamu anawezaje kuamini kwamba vita sio nia pindi taifa linapofanya mashambulizi yaliyoratibiwa kwa taifa jengine?
Hata hivyo, kinachoudhi zaidi kuliko ulaghai wa utawala huu ni kimya na kupooza kwa ulimwengu katika kukabiliana na uvamizi huo wa wazi. Operesheni ya hivi majuzi ya Marekani, iliyopewa jina la ‘Operesheni Midnight Hammer’, si uthibitisho wa nguvu ya Marekani - ni ufichuzi wa kufedhehesha wa kutokuwa na uwezo wa kisiasa na mfarakano unaoukumba Umma wa Kiislamu. Sio kwa sababu Ummah unakosa njia za kutetea haki zake - lakini kwa sababu utashi umetawanyika katika mipaka iliyovunjika, inayotawaliwa na tawala zinazojali zaidi kuhifadhi viti vyao vya utawala na utiifu kwa maslahi ya Washington badala ya watu wao wenyewe.
Pentagon ilijigamba waziwazi kwamba ndege za mashambulizi za Marekani ziliruka bila kutambuliwa katika anga ya Iran. Wakati huu lazima utumike kama wakati wa kutafakari kwa kina na kujihisabu. Umma wa Kiislamu unaenea mabara, unatawala mali nyingi, unadhibiti maeneo ya kimkakati ya baharini, na unamiliki baadhi ya majeshi makubwa zaidi duniani. Walakini mali hizi kubwa hazifai - sio kwa nguvu ya adui, lakini kwa kukosekana kwa umoja wa kisiasa na uongozi wa uwakilishi.
Mwenyezi Mungu (swt) ameujaalia Ummah huu kila kiungo kinachohitajika kwa ajili ya ubwana, mwamko, na uongozi wa kimataifa. Hata hivyo, rasilimali zetu zimesalia kugawanyika, na majeshi yetu yamezuiliwa na mipaka bandia. Mashambulizi dhidi ya Fordo, Natanz, na Isfahan si ya mbinu tu - ni kiishara. Yanatuma ujumbe ulio wazi kwa kila utawala wa Waislamu: nyenyekea, wapokonye silaha, jadiliana, au kabili maangamivu.
Hivyo basi, wito wa Mfumo wa Kisiasa wa Kiislamu - Khilafah - kuleta uadilifu, usawa, na rehema kwa wanadamu, kama ulivyofanya hapo awali, sio bora. Bali ni wajibu. Ni jambo la lazima. Na ndio njia pekee ya kusonga mbele. Khilafah itatengeneza upya mienendo ya kimataifa na kwa mara nyengine tena kuwa taifa bora la kubeba ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu.
[وَأَطِيعُواْ اللّهَ وَرَسُولَهُ وَلاَ تَنَازَعُواْ فَتَفْشَلُواْ وَتَذْهَبَ رِيحُكُمْ وَاصْبِرُواْ إِنَّ اللّهَ مَعَ الصَّابِرِينَ]
“Na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msizozane mkaingiwa woga, na zikapotea nguvu zenu. Na subirini. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanao subiri.” [8:46]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika