Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Marekani Yapanga Mpango Mpya baada ya Mpango wa Awali Kufichuliwa na Kutibuliwa na Umma

(Imetafsiriwa)

Habari:

Makundi yenye silaha ya Rohingya yameanza kusajili kutoka kambi za wakimbizi za Cox's Bazar kusaidia katika mapigano dhidi ya Jeshi la Arakan huko Rakhine. Taarifa hiyo ilifichuliwa katika ripoti moja ya Shirika la Kimataifa la kutatua Migogoro yenye kichwa "Bangladesh/Myanmar: Hatari za Waasi wa Rohingya". Ripoti hiyo inabainisha kuwa, baada ya Jeshi la Arakan kupata ushindi dhidi ya jeshi la Myanmar huko Rakhine, makundi ya Rohingya yamezidi kuwa changamfu na yamekubali kufanya kazi kwa pamoja dhidi ya Jeshi la Arakan, kundi ambalo lenye Mabudha wengi wa Rakhine kuwa kambi yake. (The Business Standard, 18 Juni 2025)

Maoni:

Ule unaojulikana kama ukanda wa misaada ya kibinadamu wa jimbo la Rakhine nchini Myanmar ulikuwa ni mradi waziwazi wa Marekani wa kuibughudhi Serikali ya Kijeshi ya Myanmar inayoungwa mkono na Uingereza. Kiasili uliundwa kusukuma Junta wa Kijeshi kutoka Kyaukpyu na Sittwe (Akyab), ngome za mwisho katika jimbo la Rakhine kwa serikali ya kijeshi (Tatmadaw). Hata hivyo, kutokana na msimamo wa kijasiri wa watu wa Bangladesh, vikiwemo vikosi vyake vya kijeshi, dhidi ya huu unaoitwa ukanda wa msaada wa kibinadamu, neno "ukanda" likawa ni kisawe cha 'tishio kwa usalama wa taifa' wa Bangladesh na 'hila chafu ya Marekani'. Kwa hivyo, Marekani ilibidi kurekebisha mkakati wake na kuleta mwelekeo wa Kiislamu katika eneo hilo ili kuleta hisia za umma kwa niaba yake na kucheza siasa zake mbaya za kijiografia. Jeshi la Arakan ambalo linawakilisha Mabudha walio wengi katika Jimbo la Rakhine ndilo kitovu cha vita vya wakala vya Marekani dhidi ya Serikali ya Junta. Wakati, ARSA (Jeshi la Wokovu la Arakan Rohingya) linawakilisha Waislamu wachache katika Jimbo la Rakhine. Hata hivyo, makundi yote mawili yana uhusiano na Marekani chini ya 'Sheria ya Burma Imeungana kupitia Uwajibikaji Mkali wa Jeshi ya 2022' ya Marekani, ambayo inajumuisha kifungu cha kumuunga mkono mtu yeyote na kila mtu anayepinga au kupigana na Tatmadaw. Mnamo 2023, Sheria ya Burma ilijumuishwa katika Sheria ya Uidhinishaji wa Ulinzi wa Kitaifa wa Marekani (NDAA) ili kutuma pesa na usaidizi wa vifaa vya kijeshi kwa vikundi vinavyopigana na serikali ya Junta. Na sasa, baada ya Marekani kuhisi kwamba mpango wake wa kulitia moyo Jeshi la Arakan kwa jina la ukanda wa msaada wa kibinadamu kupitia Bangladesh umefichuliwa, imeamua kuamsha makundi mengine yenye utambulisho wa Kiislamu ili kubadilisha hisia za umma nchini Bangladesh. Chini ya dhurufu hizi ongezeko la ghafla la usajili katika kambi za Rohingya linafanyika.

Haishangazi kwamba Marekani itatumia njia zote zinazowezekana kutekeleza njama zao ovu katika Ghuba ya Bengal. Hata hivyo, Ummah lazima ujitenge na kuwa sehemu ya mipango hii. Ummah lazima uelewe kwamba uasi wowote (hata kwa jina la Jihad) chini ya usimamizi na usaidizi wa moja kwa moja wa Marekani au Dola nyengine yoyote ya makafiri hautatatua tatizo hata moja ambalo Ummah unakabiliana nalo. Uasi umethibitishwa kutokuwa na matunda kwa Ummah matukio mengi yakiwemo matatizo ya Wasyria, Wakurdi, Baloch, Kashmir na maeneo mengine mengi. Ingawa mito ya damu ya Waislamu ilitolewa kafara, Ummah haukuweza kusonga mbele kuelekea ushindi na heshima. Wakoloni makafiri ndio waliofaidi kutokana na kafara za damu takatifu za Umma wa Mtume Muhammad (saw). Ikiwa damu na maisha ya Waislamu lazima yatolewe muhanga, basi kwa nini tusitoe kafara hiyo kwa ajili ya sababu safi ya Kiislamu?

Kando na hayo, Waislamu wa Bangladesh lazima watupilie mbali wazo la 'utaifa' katika kuwatazama Waislamu wa Rohingya. Kwa sababu utaifa ni ile sumu hatari ambayo iliufanya Ummah huu mtukufu kugawanyika na kuwa dhaifu mbele ya maadui zake Makafiri. Waislamu lazima watafakari juu ya mafanikio yasiyo na kifani ya mababu zao ambao walikumbatia kila kabila, tabaka na rangi inayowezekana na kuyayeyusha chini ya La ilaha illallah kuunda Ummah wa kutisha. Kwa hivyo, Waislamu wa Bangladesh lazima wasiwaone Waislamu wa Rohingya kama wageni na wakimbizi, badala yake wanapaswa kuwaona kama ndugu wa Kiislamu. Ni lazima wawakumbatie Waislamu wa Rohingya kama Waislamu wa Madina walivyowakumbatia Waislamu wa Makka. Sababu na maslahi ya Waislamu wa Bangladesh hayatenganishwi na sababu na maslahi ya Waislamu wa Rohingya, hivyo ni lazima wafanye sababu yao kuwa moja chini ya Khalifa mwadilifu.

[إِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱعْبُدُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbiya: 92]. Khalifa atahakikisha ukombozi wa kweli wa Arakan; ukombozi wa ardhi za Waislamu kutoka katika ukaliaji wa kimabavu wa Makafiri, pamoja na ukombozi wa nyoyo na akili za Waislamu kutokana na fikra za makafiri kama vile utaifa na usekula. Hapo ndipo njama za mkuu wa makafiri, Marekani zitaweza kutibuliwa kabisa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Risat Ahmed – Wilayah Bangladesh

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.