Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Khilafah kwa ajili ya Ulimwengu usio na NATO

(Imetafsiriwa)

Habari:

Marais wa nchi na serikali za nchi wanachama wa NATO walikutana jijini The Hague, Uholanzi mnamo tarehe 24-25 Juni.

Maoni:

25 Juni 2025 - Katika Tangazo la Mkutano wa The Hague lililotolewa na Marais wa Nchi na Serikali wa NATO, taarifa zifuatazo zilijumuishwa: “Katika kukabiliana na vitisho vikali vya usalama na changamoto, haswa tishio la muda mrefu kwa usalama wa Euro-Atlantiki unaoletwa na Urusi na tishio linaloendelea la ugaidi, washirika wanajitolea kutenga asilimia 5 ya Pato la Taifa kwa ajili ya mahitaji ya ulinzi na usalama na matumizi ulinzi ya kila mwaka hadi 2035. Kujitolea huku kutatuwezesha kutimiza wajibu wetu wa kibinafsi na wa jumla chini ya Kifungu cha 3 cha Mkataba wa Washington. Uwekezaji huu utahakikisha kwamba tuna nguvu zinazohitajika, uwezo, rasilimali, miundombinu, utayari wa kupambana na uthabiti kwa misheni tatu kuu za kuzuia na ulinzi, kuzuia na kudhibiti mgogoro, na usalama wa ushirika.”

Katika mkutano wa kilele wa NATO jijini The Hague, Urusi na ugaidi ziliibuka kuwa vitisho viwili muhimu zaidi, huku suala jengine muhimu likiwa ahadi ya nchi wanachama kutenga 5% ya Pato la Taifa kwa matumizi ya usalama na ulinzi.

NATO ni shirika la kijeshi ambalo Marekani hutumia kwa maslahi yake binafsi. Kwa sasa, Marekani inaziona Urusi, China, Ulaya na kwa neno ugaidi katika tamko la Uislamu na Waislamu kama vitisho kwake duniani.

Katika muktadha huu, Marekani inataka kutumia NATO kulinda maslahi yake dhidi ya Uislamu na Waislamu, Urusi na, kwa muda mrefu, China.

Pia ilikuwa chini ya shinikizo la Marekani kwamba nchi wanachama wa NATO zilijitolea kuongeza matumizi yao ya usalama na ulinzi hadi 5% ya Pato la Taifa.

Nchi 32 wanachama wa NATO zina jumla ya Pato la Taifa la karibu dolari trilioni 50. Nchi wanachama hutumia $1 trilioni 250 bilioni kwa usalama na ulinzi kila mwaka. Katika Mkutano wa The Hague, Marekani inalenga kuongeza idadi hii hadi dolari trilioni 2.5 kwa kujitolea kwa nchi wanachama.

Kwa hivyo, nchi wanachama wa NATO zitaingia kwenye kinyang'anyiro cha silaha, na nchi zilizo na maendeleo ya viwanda vya ulinzi na silaha, haswa Amerika, zitafaidika na hali hii. NATO pia itaimarika zaidi katika masuala ya ulinzi na usalama.

Uhalisia ni huu: Shirika la kijeshi la mataifa 32 lenye silaha za hali ya juu na majeshi yenye nguvu duniani, ni nani anaweza kulipinga, anawezaje kulipinga, nani anaweza kupigana dhidi ya nguvu kubwa kama NATO.

Marekani inataka kudumisha utawala wake duniani kwa kutumia nguvu hii kubwa, NATO, kwa maslahi yake binafsi.

Ndio maana NATO ni moja ya vitisho muhimu kwa Waislamu na wanadamu ambavyo lazima viangamizwe, vivunjwe, vikataliwe na kupigwa vita.

Kwa hivyo ni nani anayeweza kupigana na NATO na kuifanya isifanye kazi?

Jibu pekee na la kweli ni Khilafah.

Ikiwa Waislamu wanaweza kuunganisha kitovu chao chenye umuhimu wa siasa na mikakati ya kijiografia ulimwenguni, utajiri wao wa chini ya ardhi na juu ya ardhi na rasilimali, idadi yao ya karibu bilioni 2, majeshi yao makubwa yakiwa na silaha za hali ya juu ambazo zimeorodheshwa katika safu za ulimwengu kwa mradi wa kisiasa kama Khilafah, basi watakuwa nguvu kubwa ambayo inaweza kupigana na NATO na kuifanya isifanye kazi.

Khilafah ndio nguvu na chaguo pekee la kuwakomboa Waislamu na wanadamu kutoka kwa utawala wa wakoloni.

[لِمِثْلِ هٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ]

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [As-Saffat: 61]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Remzi Özer

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.