- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mgogoro wa Uhaba wa Maji Dar Es Salaam
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo Jumapili 14 Disemba 2025, Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) ilitoa ratiba ya usambazaji wa maji kwa jiji. Katika baadhi ya maeneo chombo cha plastiki cha lita 20 cha maji kutoka kwa wachuuzi wa ndani kimefikia hadi Sh1,000 mara tano zaidi ya bei ya kawaida.
Maoni:
Tangu uhuru wa bendera, Tanzania na jiji la Dar es Salaam hasa halijawahi kupata huduma ya maji ya muda wote. Kwa mfano, mwaka jana 2024, 2022 na 2021, jiji lilikuwa na uhaba mkubwa wa maji. Uhaba wa sasa kama ilivyoelezwa na serikali umetokana na kushuka kwa uzalishaji katika Kiwanda cha Ruvu kunakosababishwa na mvua kuchelewa kunyesha.
Mgogoro wa maji nchini Tanzania ni wa mzunguko, karibu kila mwaka ukiwa na viwango tofauti vya ukali. Umeathiri maisha ya watu kwa usambazaji wa maji usio thabiti kwani sehemu nyingi za jiji hupata gharama kubwa za kununua maji kutoka kwa wachuuzi na wakati mwingine watu wanalazimika kusubiri mgao wa maji usiku.
Ni aibu kwamba, licha ya Tanzania kuwa na vyanzo vingi vya maji, lakini inakabiliwa na mgogoro wa uhaba wa maji. Nchi ina maziwa makubwa kama Victoria, Tanganyika, na Nyasa, mito mingi ikiwemo Rufiji, Pangani, Wami, Ruvuma, Mara, Kagera, na Gombe, bila kusahau Bahari ya Hindi, chemichemi ya chini ya ardhi, ardhi nyevu na maji ya mvua.
Zaidi ya yote, Tanzania inapitia mambo mengine kama vile mabomba yaliyo zeeka na uvujaji unaoendelea ambao ulisababisha miundombinu ya maji katika hali ngumu na kupelekea takriban asilimia 37 hadi 49 ya maji yanayotolewa kupotea kutokana na uvujaji.
Hii ni karibu nusu ya maji yanayotolewa yanapotea. Kama maji yaliyopotea yangeokolewa, usambazaji ungekuwa bora kuliko hali ya sasa.
Hivi ndivyo serikali za kibepari kila mahali zinavyowatendea watu wao bila kujali mambo yao hata katika mahitaji ya msingi ya uhai kama vile maji.
Masuala ya kutowajibika na kupuuza katika kuwahudumia watu kwa uadilifu ndio uhalisia katika ubepari, kwani msingi wa itikadi hii na mfumo wake wa kisiasa ni maslahi binafsi pekee. Kwa hivyo, yote ndani ya wigo wa mfumo huu kutoka kwa wanasiasa na watumishi wa umma yana ajenda moja tu ya kujitajirisha, familia zao na marafiki zao na kamwe kutoshughulikia matatizo ya watu. Maslahi binafsi ndiyo yaliyowachochea wanasiasa kufikia nyadhifa za kisiasa sio hamu ya kutumikia na kutatua matatizo ya watu.
Tofauti na Uislamu, dori ya Dola ya Khilafah ni kuwahudumia watu na kipaumbele chake kikuu ni kuwafanya watu wote waweze kupata na kukidhi mahitaji yote ya msingi ya uhai. Dola ya Kiislamu (Khilafah) inawajibika na ina jukumu kutoa huduma zote za kijamii kwa raia wake wote bure au kwa gharama nafuu. Ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa wote, ni haramu kubinafsisha vyanzo vikuu vya maji au mali nyingine zozote za umma.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania