- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Silsila za Al-Waqiyah TV: Tafakari
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir inafuraha kuwasilisha kwa wafuasi na wageni wa kurasa za Afisi Kuu ya Habari katika mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan mwaka huu, 1446 H (2025 M), silsila mpya ya vipindi vya Al-Waqiyah TV vyenye kichwa “Tafakafi,” vilivyotayarishwa na kuwasilishwa na Mhandisi Baher Saleh, Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir.
Kwa hivyo jiunge nasi...
- Kipindi cha 1 -
Tafakari
Ari Jumla na Hisia ya Uwajibikaji
Moja ya masuala muhimu na ya msingi katika Uislamu ni suala la kazi ya pamoja na ari ya pamoja miongoni mwa Waislamu na ndani ya mujtamaa wa Kiislamu.
- Kipindi cha 2 -
Tafakari
Kazi ya Hizb (Chama)
Uislamu umeifanya kazi ya Hizb ni njia ya mabadiliko, na kuziathiri jamii na mifumo iliyopo.
- Kipindi cha 3 -
Tafakari
Umoja wa Ummah ni Kadhia Nyeti
Mfumo wa utawala katika Uislamu ni mfumo wa umoja, na kwa hiyo Uislamu umeifanya adhabu kuwa kali kwa yeyote anayejaribu kuugawa au kuutenga Umma.
- Kipindi cha 4 -
Tafakari
Hisia “Duni” ya Dini
Mojawapo ya njia hatari sana zinazochukuliwa na watu wengi ndani ya Umma wa Kiislamu ni mwelekeo wa udini "duni", yaani, kumwabudu Mwenyezi Mungu (swt) kwa kiwango cha chini kabisa, ambacho wazembe wanaamini kuwa kitawaokoa na Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) na kuwaondolea lawama yoyote kuhusu Ummah, Dini na ardhi zao.
- Kipindi cha 5 -
Tafakari
Je, Unachukua Dini Yako Kutoka Kwa Nani?
Tawala zimetengeneza masanamu ili watu wayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu bila ya wao kutambua. Hakika baadhi yao wanaamini kwamba kwa kufuata fatwa za Maulamaa hawa, wamefanya vyema na wakamuabudu Mwenyezi Mungu (swt). Hili ni janga.
- Kipindi cha 6 -
Tafakari
Siasa ni kazi ya Mitume (as)
Shughuli za kisiasa na kujihusisha na siasa zimekabiliwa na kampeni kubwa ya propaganda inayolenga jamii za nchi za Kiislamu pekee, kwa lengo la kuwatenga Waislamu na siasa.
Wakati huo huo kumweleza mtu kuwa mwanasiasa kunachukuliwa kuwa ni neno la kusifiwa na la kuheshimika katika jamii za Kimagharibi, kwani inaashiria kuwa mtu huyo anatoka katika tabaka la wasomi, wenye ufahamu wa kutosha na wenye maono.