Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Australia

H.  9 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 11 / 1446 H
M.  Alhamisi, 05 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutafakari juu ya Gaza, Mfano wa Ibrahim (as) na Wito wa Haraka wa Nusrah Leo

(Imetafsiriwa)

Umma unapoingia katika siku tukufu za Tashriq, katikati ya ibada za Hijja, tunakumbushwa kwamba nguzo hii adhimu ya Uislamu ni safari ya kiroho, faradhi wa kiwahyi inayoonyesha kujitolea kipekee kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Ibada za Hijja zinajumuisha mila ya Nabii mtukufu Ibrahim (as), mke wake mtukufu Hajar (as), na mwanawe Ismail (as), familia ambayo mitihani yao iliufundisha Ummah asili ya tawakkul, imani isiyoyumba kwa Mwenyezi Mungu (swt), na kujisalimisha kikamilifu kwa amri Yake tukufu, hata pale amri hiyo inapopingana na mantiki ya kidunia.

Katika siku hizi hizi za Tashriq, karne nyingi baadaye, waumini watukufu wa Aws na Khazraj walikutana kwa siri na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) huko al-‘Aqabah. Ahadi yao wakati huu haikuwa kwa ajili ya wokovu wa kibinafsi, bali kuisnusuru Dini kwa nguvu, kutoa nusrah (msaada wa kijeshi na kisiasa), ili kusimamisha mamlaka ya Uislamu. Bay’ah al-Harb (Ahadi ya Vita) hii iliugeuza Uislamu kutoka kwa ulinganizi ulioteswa hadi kuwa misheni iliyopangwa, yenye kubeba dola. Ilipelekea Hijrah, kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu ya kwanza mjini Madina, na pambazuko la Uislamu kama nguvu ya kisiasa duniani.

Leo, Ummah unajikuta katika hali mbaya mno, si kwa kukosa imani, wala kwa kukosa idadi au mali, bali kwa kukosa nguvu. Tumetawanyika na kutendewa ukatili, kutoka Gaza hadi Kashmir, kutoka Turkestan Mashariki hadi Sudan, huku madhalimu wakitutawala na maadui zetu wakitudhibiti. Majeshi ya Waislamu, wana wa Khalid ibn al-Walid na Salahuddin, yamekaa kimya, yamefungwa minyororo na tawala zinazoiogopa miji mikuu ya Magharibi kuliko wanavyomuogopa Mwenyezi Mungu (swt).

Gaza inasimama kama ishara kali zaidi ya utelekezaji wetu, jeraha linalovuja damu kwenye mwili wa Ummah, na inatukumbusha kuathirika kwetu wakati uwezo mkubwa wa Ummah umenyongwa na maadui na watawala vibaraka. Vilio vya watoto wa Palestina si tu kwa ajili ya misaada au kauli mbiu, bali ni vilio vya nusrah, kwa ajili ya msaada wa kweli unaoungwa mkono na nguvu na vitendo.

Mafunzo ya Hijja na Ahadi (Bay’ah) ya pili ya al-‘Aqabah ni mwongozo wa Mwenyezi Mungu wa kuchukua hatua. Kama vile Answar wa Madina walivyochukua msimamo wa kijasiri wa kumnusuru Mtume (saw) na wakampa njia ya kusimamisha hukmu ya Mwenyezi Mungu (swt) duniani, wakati umefika kwa majeshi yetu kufuata nyayo zao. Tunatoa wito kwa Umma wa Kiislamu - wanazuoni wake, viongozi wake, watu wake wa kawaida - kuyataka majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu waalekeze utiifu wao kwa Uislamu pekee. Wajiepushe na viti vya khiyana vya utawala na wavuruge mipaka na amri za makafiri, na badala yake watoe nusra yao kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa njia ya Utume.

Katika siku hizi zilizobarikiwa, tunapokumbuka kujitolea mhanga kwa Ibrahim (as) na ujasiri wa Answar, ni lazima tuinuke kwa mara nyengine tena tukiwa na imani na Mwenyezi Mungu (swt), utiifu kwa amri Yake, na azimio thabiti la kukomesha mateso ya Waislamu wa Gaza milele. Hili linatuhitaji sisi sote kuzidisha ulinganizi kwa wale wenye nguvu halisi ya kumuitikia Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) na kuupa Ummah Nusrah, kama vile Answar walivyofanya kwa maneno yao: “Tunatoa ahadi ya kutii katika mazuri na machukivu, katika wepesi na uzito, na, kusema kweli kila wakati, na kwamba katika kumtumikia Mwenyezi Mungu hatutaogopa lawama ya yeyote.”

[يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱسْتَجِيبُوا۟ لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” (Surah Al-Anfal: 24)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 0438 000 465
www.hizb-australia.org
E-Mail:  media@hizb-australia.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.