Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  4 Dhu al-Hijjah 1447 Na: H 1447 / 081
M.  Alhamisi, 21 Mei 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hakuna Mwisho wa Mauwaji kwa Watoto wa Palestina na Lebanon Bila Kuondolewa kwa Umbile la Kiyahudi

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 13 Mei, UNICEF iliripoti kwamba angalau watoto 59 waliuawa au kujeruhiwa nchini Lebanon katika wiki iliyopita kutokana na shambulizi la umbile la Kiyahudi nchini humo. Tangu kuanza kwa usitishaji mapigano mnamo tarehe 17 Aprili 2026, angalau watoto 23 wameuawa na 93 kujeruhiwa, na kufikisha jumla ya watoto 200 waliouawa na 806 waliojeruhiwa nchini Lebanon tangu tarehe 2 Machi. Mapema mwezi huu, iliripotiwa kwamba msichana wa miaka 12 na baba yake waliuawa huko Nabatieh baada ya Jeshi la Ulinzi la ‘Israel’ kumlenga kupitia droni kwa mashambulizi matatu ili kuhakikisha kwamba haishi. UNICEF pia imekadiria kwamba watoto 770,000 nchini Lebanon wanakabiliwa na dhiki kubwa kutokana na kukabiliwa na vurugu mara kwa mara, hasara na kuhamishwa kutoka vitani, ikiwa ni pamoja na kuteseka kutokana na hofu kali, jinamizi, kukosa usingizi na hisia za kukata tamaa, na kuwapelekea kwenye hali zinazowezekana za afya ya akili maisha yote. UNICEF pia iliripoti mnamo tarehe 12 Mei kwamba watoto 70 wameuawa katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem Mashariki na 800 wamejeruhiwa tangu 2025, hasa mikononi mwa vikosi vya Mayahudi na walowezi. Yote haya, yanaambatana na mauaji yanayoendelea ya watoto huko Gaza licha ya kile kinachoitwa kusitisha mapigano, huku zaidi ya watoto 21,000 wakiuawa tangu Oktoba 2023 sawa na mtoto mmoja akiuawa kila saa moja kwa wastani.

Je, sio dhahiri kwamba hakuna usitishaji mapigano, makubaliano ya amani au mpango kutoka Amerika au dola yoyote ya Magharibi au chombo cha kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa kitakachokomesha mauaji haya ya kinyama ya watoto wa Lebanon, Palestina au nchi nyengine yoyote na umbile la Kiyahudi ambalo limeweka wazi kwamba halitakomesha mauaji yake ya kikabila ya watu wa Palestina na ardhi zinazozunguka hadi litakapofikia ruwaza yake ya kile kinachoitwa ‘Israeli Kubwa’?

Kulenga watoto ili kuwashambulia kimwili na kisaikolojia ili kudhoofisha kizazi kijacho na upinzani wake kwa kuwepo kwa umbile hili la vimelea, bila shaka ni sehemu ya mpango huu. Yote haya hayatakwisha hadi umbile hili halifu litakapong'olewa kabisa. Hata hivyo hili halitapatikana kamwe huku utawala wa serikali na viongozi wa sasa wasio na utu na wasaliti wa ardhi za Kiislamu ukiendelea, ambao wamejionyesha kuwa walinzi, watetezi na wafuasi wa umbile la Kiyahudi, wakilipa njia na nguvu zake, na kuzuia majeshi ya Waislamu kutetea Ummah wao na kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa. Hakika, kuwepo kwa watawala na serikali hizi kumeimarisha uvamizi huo ili kuongeza uhalifu wake dhidi ya Waislamu, wakijua vyema kwamba hakutakuwa na dola wala kiongozi wa kuwazuia.

Watoto wa Palestina, Lebanon na kwengineko hawatafurahia usalama kamwe, wala kufurahia maisha ya staha bila kuondolewa kwa tawala na watawala hawa na kusimamishwa kwa dola ya ulinzi, Khilafah kwa njia ya Utume, ambayo ni ngao na mlinzi wa Ummah na Dini yetu, na ambayo itahamasisha jeshi lake bila kusita au kuchelewa kung'oa uvamizi huu wa saratani milele na kukomboa kila shubiri ya ardhi Iliyobarikiwa.

Kwa hivyo, tunawauliza ndugu zetu katika majeshi ya Waislamu, mtasimama bila kuchukua hatua hadi lini huku watoto wa Ummah huu wakichinjwa na umbile hili la Kiyahudi? Mtaipa mgongo ardhi Iliyobarikiwa na kunajisiwa kwa Al Aqsa hadi lini? Mtawatumikia watawala hawa waoga hadi lini ambao wamewaletea aibu kwa kukuzuieni kutetea Ummah wenu? Na mtaacha Amri ya Mola Mlezi wenu ya kuwalinda Waislamu na kukomboa ardhi zao hadi lini? Jiokoeni kutokana na fedheha ya maisha haya na adhabu kali ya maisha yajayo kwa kuwaondoa watawala hawa wasaliti na kutoa Nusrah yenu kwa ajili ya kusimamisha Khilafah, ambapo chini yake mtakumbatia dori yenu ya kweli kama wakombozi na watetezi wa Waislamu na Dini yenu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِلاَّ تَنفِرُواْ يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلاَ تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Taubah: 39].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizbuttahrir.today

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.