Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
| H. 16 Jumada II 1447 | Na: H.T.L 1447 / 15 |
| M. Jumatano, 17 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon Yamzuru Mbunge Ibrahim Mneimneh
(Imetafsiriwa)
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon, unaojumuisha Dkt. Muhammad Jaber, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Lebanon, na Mhandisi Saleh Salam, mjumbe wa kamati hiyo, walimtembelea jana, Jumanne, 16 Disemba 2025, Mbunge wa Beirut Bw. Ibrahim Mneimneh.
Mwanzo, ujumbe huo uliitambulisha hizb, fikra zake, na yanayoitofautisha na vyama vyengine, pamoja na msimamo wake wa kimaadili na kupinga kwake umadhehebu, utaifa, na ukiri.
Ujumbe huo kisha uliwasilisha ruwaza ya hizb ya suluhisho msingi kwa Lebanon, ambalo liko katika kurudi kwenye uhalisia wa asili kama sehemu ya Bilad al-Sham, mbali na masuluhisho yasiyo ya Kiislamu na yasiyofaa ambayo hurefusha mgogoro, kuuzidisha, na hayautatui.
Ujumbe huo pia ulizungumzia matatizo ya kanda hii na juhudi endelevu za watawala wa Lebanon kivitendo zinazopelekea kutambuliwa rasmi kwa umbile la Kiyahudi na kuanzishwa kwa mahusiano ya kiuchumi nalo.
Ujumbe ulionya kuhusu umuhimu wa wabunge na wanasiasa wote wenye ikhlasi kusimama dhidi ya mradi huu waziwazi, kwa uchache kupitia msimamo na kauli wazi.
Mwishoni mwa mkutano, pande zote mbili zilikubaliana kuhusu mikutano ya mustakbali ili kuendelea kujadili maendeleo.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Lebanon
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Lebanon |
Address & Website Tel: 009616629524 http://www.tahrir.info/ |
Fax: 009616424695 E-Mail: ht@tahrir.info |