Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  15 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 21 / 1446 H
M.  Jumatano, 11 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kongamano la Amani ya Kiraia jijini Damascus
Utangulizi wa Kuwaondoa Watiifu wa Serikali na Kuhalalisha Nembo za Ukandamizaji na Uhalifu

(Imetafsiriwa)

Mkutano na waandishi wa habari uliofanywa na Kamati ya Amani ya Kiraia katika jengo la Wizara ya Habari jijini Damascus mnamo Jumanne, Juni 10, 2025, chini ya uenyekiti wa mwanakamati Hassan Soufan, ulizua wimbi kubwa la hasira na chuki kubwa miongoni mwa Wasyria, hasa miongoni mwa familia za mashahidi na waliopotea, na watoto wa mapinduzi. Wengi waliona kauli za mkutano huo kama uchochezi kwa familia za wahasiriwa, kupuuza mihanga ya wanamapinduzi, kudharau damu ya mahsahidi, kukana ukweli usiopingika, na uhalalishaji wa wazi wa wahalifu wa kivita. Hafla hiyo ilionekana kama jaribio la kulalalisha mahusiano kwa nembo za utawala ulio ng’atuliwa chini ya mabango ya "amani ya raia," "kujenga taifa," na "kuzuia umwagaji damu."

Hasira hii iliyoenea ilifuatia matamshi ya Soufan wakati wa mkutano huo, ambapo alitetea sera ya kuwaachilia maafisa wa utawala wa uliopita bila uwajibikaji wa kisheria au mashtaka ya umma, wa kwanza kabisa miongoni mwao ni Fadi Saqr akipuuza kabisa rekodi zao za umwagaji damu. Soufan hata alifikia hatua ya kuwachukulia baadhi yao kuwa washirika katika ushindi, akidai kwamba walichangia "kuzuia umwagaji damu wa Syria" na "kushirikiana na uongozi wa kijeshi wakati wa vita vya ukombozi," akitaka wakosoaji kuwasilisha "ushahidi wa kuaminika" wa kuhusika kwao katika uhalifu.

Soufan alidai kuwa maafisa walioachiliwa huru walikuwa wakifanya kazi tangu 2021 na walijisalimisha kwa khiyari kwenye mpaka wa Iraq chini ya mpango unaojulikana kama "tabia salama". Alisema waliozuiliwa walifanyiwa uchunguzi wa kisheria ambao haukuthibitisha mashtaka yoyote ya uhalifu wa kivita dhidi yao, na kusisitiza kuwa kuendelea kuwashikilia hakuna maslahi ya kitaifa na hakuna uhalali wa kisheria. Muda mfupi baadaye, mitandao ya kijamii na kurasa za habari zilijaa ushahidi wa video na nyaraka zinazothibitisha kuhusika kwa watu kadhaa walioachiwa huru hasa Fadi Saqr na Socrates Al-Rihiya katika mauaji na ukiukaji wa wazi dhidi ya raia.

Soufan alidai zaidi kwamba watu kama Fadi Saqr wanacheza dori katika kutatua migogoro, kutatua matatizo, na kukabiliana na vitisho vya kitaifa, na kuongeza: "Tunaelewa uchungu na hasira iliyohisiwa na familia za mashahidi, lakini tunalazimika kufanya maamuzi ambayo yanahakikisha utulivu wa kiasi katika hatua hii." Alithibitisha kwamba kuachiliwa huru kunajumuisha wale tu "ambao mikono yao haikuwa na damu ya Syria," na kuiita kama "sehemu ya mchakato wa amani ya raia." Alisema kuwa haki ya mpito haimaanishi kumwajibisha kila mtu aliyetumikia serikali, bali ni wahalifu wakuu pekee waliofanya ukiukaji mkubwa. Alionya kuwa kuharakisha mchakato wa haki ya mpito au kuutekeleza mmoja mmoja kutasababisha machafuko na kuifanya serikali ionekane haina uwezo wa kutekeleza majukumu yake hivyo kufungua mlango wa uingiliaji wa nje. Alisisitiza kuwa kulipiza kisasi hakutaleta haki ya mpito, na kwamba kujumuisha watu wenye utata katika mchakato wa maridhiano ni jaribio la kushughulikia mizozo ya kimuundo nchini. Alisema kuwa kutoa msamaha kwa Fadi Saqr kunatokana na tathmini ya jumla ya hali ilivyo na ilikusudiwa kuzuia umwagaji damu katika maeneo yenye taharuki na kuzituliza jamii za wenyeji.

Yeyote aliyefuatilia matukio ya mkutano huu wa wanahabari angeona kama uthibitisho wa mwelekeo wa utawala wa sasa wakati wa awamu ya mpito sera zake kuhusu mabaki ya utawala, msimamo wake wa kubadilika kuhusu kanuni na malengo msingi ya mapinduzi, na kushughulikia kwake madai ya haki na uwajibikaji kwa wale wanaomwaga damu isiyo na hatia. Hili limewafanya wengi kutangaza kwamba hakuna upande wowote ulio na haki ya kuwanyima haki waathiriwa, kusamehe kwa niaba yao, au kumlinganisha muuji na mhasiriwa. Pia kulikuwa na maonyo kuhusu kuongezeka kwa uhasama kwa sababu ya kutojali hisia za familia za mashahidi na waliopotea, ambao wanashuhudia kuachiliwa huru kwa wahusika wa utawala wa kihalifu mmoja baada ya mwengine wakiuona msamaha kama huo kama "kushiriki katika uhalifu."

Suala la kuondolewa kwa vikwazo kwa muda mrefu limekuwa shinikizo la Marekani na Ulaya kwa utawala wa sasa, kwa lengo la kuweka maono yao kwa utawala wa Syria kutoka "kupambana na ugaidi" hadi kulazimisha usekula, kukiuka ubwana wake kwa kuifunga kwa maamuzi na maagizo ya Magharibi, na hatua kwa hatua kujumuisha upya mabaki ya serikali katika taasisi za serikali chini ya visingizio na miito dhaifu.

Zaidi ya hayo, kusafishwa hadharani kwa Fadi Saqr na mfano wake, bila kuona aibu, ni uchokozi wa wazi kwa watu wa Syria, hasa kuonekana kwake kando ya gavana wa Damascus, pamoja na athari zote na ujumbe unaobebwa. Badala ya kuwashtaki wahalifu chini ya sheria iliyo wazi na ya haraka ya jinai, mamlaka zinatumia mipango inayofifisha chini ya majina ya mazungumzo, umoja wa kitaifa, amani ya kiraia, na maridhiano ya kijamii, kana kwamba matukio ya miaka 14 yalikuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na sio mojawapo ya mapinduzi makubwa zaidi katika historia.

Ni lazima ikumbukwe pia kwamba wakati wengi wenye historia za uhalifu dhidi ya mapinduzi wanachukua majukwa makubwa leo, wabebaji wengi wa da'wah, wafungwa wa maoni, wanamapinduzi, na mujahidina wanasalia kufungwa bila haki huko Idlib kwa miaka mingi. Wakati huo huo, watu wetu wengi katika kambi za kuhama makaazi bado hawana uwezo wa kujenga upya nyumba zao zilizoharibiwa na wale ambao sasa wamebadilisha ngozi zao na kuchukua dori mapya.

Katika mkondo huo huo, kuibuka kwa Fadi Saqr na viongozi wengine wakuu kutoka kwa utawala uliokufa kama mabingwa wa amani ya raia, wakiwa na ulinzi salama, pamoja na wafanyibiashara wakubwa na wahalifu mashuhuri wa kivita walioregea hivi karibuni Damascus pamoja na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali, na watu mashuhuri ambao kwa miaka mingi walimuunga mkono dhalimu aliyekimbia na kutoa wito wa mauaji na uharibifu, na ambao wanasalia kutoguswa na kutowajibishwa chini ya kisingizio cha “amani ya raia” yote haya yanazidisha hasira na uchungu wa familia za mashahidi na waliopotea.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameonya dhidi ya dhulma na hatima ya madhalimu. Mapinduzi ya Syria hayatakwisha, wala migogoro yake iliyozidi kutatuliwa baada ya kuanguka kwa utawala uliokufa, isipokuwa kama kanuni msingi za mapinduzi yetu zitatimizwa. kuporomoka kwa utawala lazima iwe ndio utangulizi wa haki, usalama, uhakikisho na maisha ya staha. Hilo haliwezi kupatikana kupitia mfumo wa kisekula unaotenganisha dini na maisha, serikali, na jamii, kama nchi za Magharibi zinavyotaka kutulazimishia juu yetu, lakini badala yake kwa kusimamisha mfumo unaojikita katika imani zetu msingi, mzizi unaotimiza matarajio yetu na kufikia malengo ya mapinduzi yetu. Ni kupitia tu sheria na hukmu za Uislamu, na kupitia dola ya Kiislamu, ndipo uadilifu wa kweli, usalama na amani vitapatikana. Kwa kheri kubwa kama hii, na wajitahidi wenye ikhlasi.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.