Afisi ya Habari
Wilayah Syria
| H. 1 Muharram 1448 | Na: 02 / 1448 H |
| M. Jumanne, 16 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mwaka Mpya wa Hijri Sio Maadhimisho ya Kihistoria, Bali Mwanzo wa Kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu Na Khilafah Rashida ya Pili kwa Njia ya Utume Itarudi Tena
(Imetafsiriwa)
Mwaka Mpya wa Hijri unatujia tarehe 1 Muharram 1448 H, sawia na 16/06/2026 M. Hii ndiyo tarehe iliyochaguliwa na Al-Faruq Umar ibn Al-Khattab na Maswahaba watukufu (ra) kama kalenda ya Waislamu. Alichagua tarehe hii kwa sababu iliashiria kuzaliwa kwa Dola ya kwanza ya Kiislamu iliyosimamishwa na Mtume wetu (saw) mjini Al-Madinah Al-Munawwarah.
Dola hii iliendelea kwa karne nyingi, ikitawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ikitabikisha mfumo aliouidhinisha kwa waja Wake, ikibeba ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu kama ujumbe wa uongofu, haki, na nuru, na kufungua ardhi ili kuwaleta watu kutoka kwenye ibada ya waja hadi kwenye ibada ya Mola wa waja.
Katika kumbukumbu ya Hijra na kuanzishwa kwa Dola ya kwanza ya Kiislamu, tunawapongeza Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata ibn Khalil Abu Al-Rashtah, kwa ndugu zetu wote miongoni mwa wabebaji Dawah katika Hizb ut Tahrir, na kwa Waislamu kote ulimwenguni. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atukirimu katika mwaka huu kwa ushindi na tamkini kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo Hizb ut Tahrir imejitolea kwayo, ikifuata mfano wa Mtume (saw) na kubaki imara katika njia ambayo alianzisha Dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Al-Madinah Al-Munawwarah.
Pia tunawaapia watu wetu nchini Syria na kwa vijana na mabinti wote wa Ummah wetu kwamba tutabaki imara katika njia ya bwana wetu Muhammad (saw), tukifanya kazi na watu wa Ummah wetu na kwa ajili yao hadi Mwenyezi Mungu (swt) atukirimu sote kwa kusimamishwa kwa Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt) na bishara njema ya Mtume Wake (saw). Tunawalingania wafanye kazi nasi kwa ajili ya kusimamisha faradhi hii kubwa, kwani katika hilo pekee ndiko kwenye heshima, mafanikio, na ustawi wetu hapa duniani na Akhera, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Kipengee chetu ni kuamini ahadi ya Mola wetu Mlezi na kauli yake:
[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Nur:55]. Na tumeziamini bishara njema za Mtume wetu (saw) aliye tubashiria alipo sema:
«... ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا اللهُ إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ، ثُمَّ سَكَتَ»
“...Kisha kutakuwa na utawala dhalimu, nao utakuwepo kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka uwepo kisha Mwenyezi Mungu atauondoa atakapotaka kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume. Kisha akakaa kimya.”
Dola ya Khilafah ambayo tunajitahidi kwayo, tukifuata njia ya Mtume wetu (saw), si dola ya kundi au pote; badala yake, ni dola ya Waislamu wote. Inasimamisha sheria za Mwenyezi Mungu, inawaunganisha Waislamu, inaukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, na inabeba ujumbe wa Risalah ya Uislamu ambao utawaokoa wanadamu wote kutokana na dhulma ya ubepari na dhulma ya mifumo iliyotengenezwa na wanadamu. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kwa yakini itasimamishwa licha ya mipango ya wapangaji na njama za walaji njama.
[وَاللَّهُ غَالِبٌ عَلَىٰ أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]
“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf:21]
Ustadh Ali Mustafa Al-Bakri
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Syria |
Address & Website Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria www.tahrir-syria.info |
E-Mail: media@tahrir-syria.info |