Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi ya Takbira “Allahu Akbar na Sheria ni ya Mwenyezi Mungu Pekee”

Baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 5 Dhul-Hijjah 1447 H, matembezi ya Takbira (Allahu Akbar) yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalianza kutoka Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu, Tunis. Umati mkubwa wa Watunisia ulishiriki, wakipiga Takbir na Tahleel (Allahu Akbar na La Ilaha illa Allah), na kuandamana kupitia barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra (Mapinduzi). Mabango yaliinuliwa, ikiwa ni pamoja na moja lililoandikwa, “Allahu Akbar, na sheria ni ya Mwenyezi Mungu pekee,” jengine liliandikwa, “Allahu Akbar: Uislamu ndio kitambulisho chetu na Khilafah ndio Dola yetu,” na la tatu liliandikwa, “Allahu Akbar, Uislamu ni dini yetu na njia yetu ya maisha, Khilafah ni dola yetu, na Jihad ni njia yetu.”

Matembezi hayo yalimalizika mbele ya ukumbi wa michezo wa manispaa kwa mkutano ambapo mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir alitoa hotuba yenye kichwa “Na mkumbukeni Mwenyezi Mungu katika siku chache zilizowekwa.” Ndani yake, aliwasilisha ujumbe kwa Ummah wa Kiislamu: kwamba ni umma unaokirimiwa na Mwenyezi Mungu kupitia Uislamu, umma ambao mizizi yake imepandwa katika mwongozo wa wahyi wa kimungu, ukilelewa chini ya kivuli cha ujumbe, na kushikamana kwa uthabiti na kamba ya Mwenyezi Mungu. Hakuna adui anayeweza kung'oa Uislamu kutoka kwenye kina chake. Ni umma wenye ukarimu ambao umepitia kikwazo, ukiwaongoza wale wanaosubiri na wenye roho dhaifu kuamini kwamba umeangamia, lakini udanganyifu wao ulithibitika kuwa ni mazimwi. Kutoka kwenye majivu na vifusi, Ummah unaiangaza dunia kwa watu wanaoibuka kama alfajiri ya kweli, simba kwenye viwanja, ambao hawakubali maelewano wala majadiliano, na ambao nyoyo zao hazijui hofu. Leo, kutoka moyoni mwa ukweli huu mchungu, kundi hili la watu waaminifu linajiandaa kukaribisha alfajiri ya mabadiliko makubwa na ya kina. Treni ya mabadiliko haitasimama hadi viti vya utawala vya madhalimu vitakapoangushwa, na juu ya magofu yao, dola kubwa ya Kiislamu na Khilafah yake Rashida kwa njia ya Utume, kusimamishwa. Hapo pekee ndipo ukurasa wa mkanganyiko na unyenyekevu utakapogeuzwa, utawala wa ukandamizaji utaanguka, na umma wetu utarudi katika hali yake iliyoamriwa na Mwenyezi Mungu: taji juu ya vichwa vya mataifa, chemichemi ya uadilifu, nuru ya uongofu, na (خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ) Umma bora uliotolewa kwa ajili ya watu.”

Matembezi hayo na kaulimbiu zake zenye lengo zimepata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, huku watu wa Tunisia na kwengineko wakijibu kwa “Allahu Akbar” na maneno ya kutamani kurudi kwa Uislamu na dola yake. Matembezi hayo yalithibitisha kwamba umma wa Kiislamu leo ​​unatamani kuishi chini ya uadilifu wa Uislamu baada ya kuonja kila aina ya umaskini, udhalilifu, na fedheha chini ya utawala wa mfumo huu dhalimu na mwovu wa kirasilimali na watawala wake Ruwaibidha (wajinga na watepetevu), na kwamba una hamu ya kumridhisha Mola wake Mlezi kwa kumfuata Mtume wake.

(فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدًى فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشْقَىٰ (123) وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا).

Na ukikufikieni uwongofu kutoka kwangu basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika. Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Taha: 123-124]

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia

Ijumaa, 05 Dhu al-Hijjah 1447 H sawia na 22 Mei 2026 M

-Video ya Matembezi -

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir

Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.