Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  4 Dhu al-Hijjah 1446 Na: H 1446 / 119
M.  Jumamosi, 31 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Nani atakayewatetea Wanawake wa Sudan na Darfur?
(Imetafsiriwa)

Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (Médecins Sans Frontières) limeonya kuwa wanawake na wasichana katika jimbo la Darfur nchini Sudan wako katika hatari ya karibu kila mara ya unyanyasaji wa kijinsia. Mizani halisi ya mgogoro huu inasalia kuwa vigumu kubainisha, kwani huduma bado ni chache na watu wanakabiliwa na vikwazo katika kutafuta matibabu au kuzungumza kuhusu masaibu yao. Hata hivyo, manusura wote waliozungumza na timu za MSF huko Darfur na kuvuka mpaka nchini Chad walisimulia hadithi za kutisha za ghasia za kikatili na ubakaji. Huku wanaume na wavulana pia wakiwa hatarini, kiwango cha mateso kinapita maelezo.

Mzozo ulioanza mnamo Aprili 2023 kati ya jeshi la kawaida la Sudan na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) umesababisha vifo vya makumi ya maelfu, watu milioni 13 waliokimbia makaazi yao, na kuacha miundombinu ya nchi hiyo tayari kuwa magofu. RSF imekuwa ikishutumiwa tangu kuanza kwa vita vya unyanyasaji wa kingono nchini kote, ambavyo vimeenea sana huko Darfur kiasi kwamba vimefikia kiwango cha kutisha, na kuwafanya watu wengi kuiona kama hatima isiyoepukika. Wasichana na wanawake wanahisi kutokuwa salama kila mahali, wanashambuliwa majumbani mwao, huku wakikimbia vurugu, wakikusanya chakula, wakikusanya kuni, au wakifanya kazi mashambani.

MSF iliripoti kuwa kati ya Januari 2024 na Machi 2025, iliwatibu manusura 659 wa ghasia huko Darfur Kusini, 94% yao wakiwa wanawake na wasichana. Zaidi ya nusu walivamiwa na vikundi vyenye silaha, karibu theluthi moja walikuwa watoto, na wahasiriwa wengine walikuwa na umri wa miaka mitano.

Kulingana na mkurugenzi wa matibabu ya dharura katika MSF, kuna ukosefu mkubwa wa huduma za matibabu kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na msaada wa kisaikolojia na huduma za ulinzi, sawa na huduma nyingi za kibinadamu na afya nchini Sudan. Ni muhimu kwamba waathiriwa wapate huduma baada ya kushambuliwa, kwani unyanyasaji wa kijinsia ni dharura ya kiafya, na matokeo yake ya haraka na ya muda mrefu ya kimwili na kisaikolojia yanaweza kuhatarisha maisha. Hata hivyo manusura wanatatizika kupata huduma za matibabu na ulinzi kutokana na uhaba wa huduma na ugumu wa kuwafikia. Aibu, uoga wa unyanyapaa, au uoga wa kulipiza kisasi pia husababisha wengi kusita kusema kuhusu mashambulizi.

Hali ni sawa katika maeneo mengine ambapo MSF inatoa huduma kwa waathirika, kama vile mashariki mwa Chad, ambayo kwa sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 800,000 wa Sudan. Huko Adré, MSF iliwatibu manusura 44 tangu Januari 2025, karibu nusu yao wakiwa watoto. Katika eneo la Wadi Fira, manusura 94 walipata matibabu, 81 kati yao wakiwa na umri wa chini ya miaka 18. Ushuhuda wa wagonjwa na wahudumu katika mashariki ya Chad na Darfur unathibitisha uhalisia huu wa kutisha.

Kwa Maafisa wa Jeshi na Wanajeshi: Mnaendeleza mapigano haya ya kuchukiza, ambayo gharama yake kubwa hulipwa na raia, wanawake na watoto, yanayotumikia maslahi ya Amerika na Ulaya ambao wanatamani ubwana juu ya Sudan na kutafuta udhibiti wa mali yake na hatima ya watu wake, hata kama itasababisha kugawanywa kwake katika nyanja za ushawishi mnaofikiri itakuwa wenu. Basi ondokeni katika udanganyifu na upotofu wenu ili mrehemewe.

Kwa Watu Wetu Nchini Sudan: Hili ni tone tu katika bahari ya mateso ambayo mumestahamili tangu kuzuka kwa mzozo wa umwagaji damu, ambao umeingia kwenye handaki la giza la vurugu, uhamishwaji, na mporomoko wa kiuchumi na kijamii, ambao kwao munaishi matokeo ya kutisha.

Mzozo huu unaendeshwa na dola za kikoloni zinazoimezea mate nchi yenu—basi kwa nini musichukue hatua ya kuusimamisha, kuwang’oa walaji njama, na kumpata mtawala muongofu wa Kiislamu na kiongozi shupavu ambaye haogopi batili, haibembelezi, wala hataki madaraka wala cheo, bali anatafuta badala yake kutabikisha sheria ya Mwenyezi Mungu na mfumo wake wa wahyi. Haya ndiyo yanayowaunganisha wananchi na Ummah:

[وَإِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ]

“Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.” [Surat Al-Mu'minun:52]

Hili litakuja tu kupitia kazi umakini ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itasahihisha kile kilichopotoka, kurudisha haki kwa wamiliki wake, na kuregesha mali kwa watu wake, ili Sudan kwa mara nyengine tena iweze kuwa kapu la chakula la Waislamu na ngome ya Dola ya Kiislamu.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizbuttahrir.today
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizbuttahrir.today

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.