Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
H. 15 Muharram 1447 | Na: H 1447 / 003 |
M. Alhamisi, 10 Julai 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Enyi Waislamu: Yaelekezeni macho yenu kwenye makasri ya watawala wenu, sio Ikulu ya White House!
(Imetafsiriwa)
Macho ya Waislamu kwa jumla, na waandishi wa habari, wachambuzi, waangalizi, na wale wanaohusika hasa, yanaelekea Ikulu ya White House, na kwenye matokeo ya mikutano ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu. Je, Trump atamshinikiza Netanyahu kukubali kwa upole kusitisha vita vyake dhidi ya Gaza?
Hatutii chumvi tunaposema kwamba watu wanaohusika zaidi na kukomesha vita dhidi ya Gaza ni watu wa Gaza wenyewe, ambao wanaungua katika moto wa vita hivyo, wakiuawa, kujeruhiwa, wakiwekwa njaa, na kuhamishwa makaazi yao, na vile vile watu wengi katika nchi za Kiislamu, ambao wamefungwa minyororo ya mipaka bandia na tawala za dhulma na ufisadi zinazoongozwa na watawala vikaragosi, wajinga wasiostahiki kutawala, wanaowazuia kupigana jihad katika kuwanusuru watu wa Gaza na Palestina yote.
Tunaona chaneli za satelaiti na tovuti za habari katika nchi za Kiislamu zikiwakaribisha wachambuzi wa masuala ya kisiasa na wanafikra kuchambua matukio, misimamo, na taarifa chaneli na tovuti hizo zikifanikisha ushindi wa vyombo vya habari au mikwara ya wanahabari!
Je! yamefikia haya enyi Waislamu? Matukio yanakujieni, njama zinafanywa dhidi yenu, na munasimama kutazama na kusubiri?! Ndugu zenu wanauawa, wanakufa njaa, na wanahamishwa huku mkiwatazama, na aliye bora zaidi miongoni mwenu ni yule anayetazama tu na kuchambua! Je, Waislamu hawana majeshi yaliyojaa pesa, na silaha za hali ya juu zilizonunuliwa kwa mabilioni ya dolari, ambazo chini ya bendera zao zinahudumia wana bora wa Ummah, tayari kupigana na kujitolea mhanga maisha na mali katika kuulinda Ummah, matukufu yake, na heshima yake?!
Mna nini, Enyi Waislamu? Je, hamkuwa mabwana wa dunia kwa karne nyingi? Je, ninyi hamkuwa washawishi na washiriki mahiri katika siasa za kimataifa? Je, mumesahau kwamba jeshi lenu liliwahi kuitwa kuwa ni “jeshi lisiloshindwa”? Na leo, kundi dogo la takataka za dunia, viumbe viovu zaidi na vioga, vinakalia kimabavu ardhi yenu iliyobarikiwa, vinaua, vinawahamisha, na kuwaua kwa njaa ndugu zenu, na kuzunguka anga zenu na ndege zao bila kuogopa hata risasi moja kufyatuliwa kwazo!
Enyi Waislamu: Matukio ya leo hayahitaji tena uchambuzi - pazia imeinuliwa. Adui zenu wanatangaza waziwazi uadui wao kwenu, kwa uwazi na hadharani, kwa kila tukio. Na watawala wenu wamefichuliwa; uaminifu wao kwa mataifa ya makafiri wakoloni ni dhahiri kwa yeyote mwenye macho. Ili kuhifadhi viti vyao vibovu vya utawala, wanadumisha mgawanyiko wenu, wanazuia umoja wenu, na kuwatia mikononi mwa adui zenu. Basi, si ajabu kwamba wanakuzuienu kuwanusuru ndugu zenu wa Palestina na kwengineko.
Kwa hivyo, tutaendelea kusisitiza yale ambayo tayari yanajulikana na kukariri yale ambayo tayari yameeleweka: Ni wakati sasa wa macho yenu kuelekezwa makasri ya watawala wenu badala ya Ikulu ya White House, tukimngojea Trump kumshinikiza Netanyahu amalize kwa upole vita dhidi yenu. Umefika wakati macho yenu yaelekezwe kwenye kambi za jeshi lenu, mkiwahimiza kusonga na kuikomboa ardhi iliyobarikiwa na kuitakasa kutokana na Mayahudi, na kuwatia hofu walio nyuma yao kutoka katika mataifa makafiri.
Hii hapa Hizb ut Tahrir uongozi wa dhati usiowadanganya watu wake mbebaji mradi wenu wa mwamko, ikikuhimizeni mufanye kazi nayo ili ikuongozeni kwenye ushindi, heshima, na hadhi munayotamani. Inusuruni, na Mwenyezi Mungu atakunusuruni.
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today |