Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 10 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: H 1447 / 084 |
| M. Jumatano, 27 Mei 2026 |
Pongezi kwa Idd ul-Adha Iliyobarikiwa 1447 H
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar… Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lillahi al-Hamd
(Imetafsiriwa)
Kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema: «إِنَّ أَعْظَمَ الْأَيَّامِ عِنْدَ اللهِ يَوْمُ النَّحْرِ» “Hakika siku tukufu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni siku ya Arafah”, basi kwa mnasaba huu uliobarikiwa na kwa kutukuza alama za Mwenyezi Mungu Azza wa Jalla: ﴾ذَلِكَ وَمَن يُعَظِّمْ شَعَائِرَ اللَّهِ فَإِنَّهَا مِن تَقْوَى الْقُلُوبِ﴿ “Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo.” [Al-Hajj: 32], na Licha ya majanga ambayo Umma wa Kiislamu unapitia chini ya watawala waliouangusha na kuusalimisha kwa adui yake, ambayo yamejaza nyoyo zetu maumivu na huzuni, bado tunapaswa kutoa pongezi na baraka zetu za dhati kwa Umma wetu wa Kiislamu, wenye subira, na wenye kutaraji mema katika Idd al-Adha iliyobarikiwa, tukimwomba Mwenyezi Mungu azifanye siku hizi za Idd kuwa za baraka, ushindi, na kuinuliwa.
Pia tunafurahi kutoa pongezi zetu, na pongezi za mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake, kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Rashta, Mwenyezi Mungu amhifadhi, tukimwomba Mwenyezi Mungu kwamba Umma hivi karibuni umpe ahadi ya utiifu (bay’ah) kwake bay’ah ya Khilafah Rashida, ambayo itamaliza enzi ya udhalilifu ambayo Umma unaishi ndani yake, ili pamoja nao enzi ya ushindi, ukombozi na tamkini iweze kuanza, kwa kusadikisha kauli ya Mwenyezi Mungu:
﴿وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً﴾.
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [An-Nur: 55]
Mwaka huu, Idd al-Adha inakuja huku Umma wa Kiislamu ukiendelea kuugua chini ya uzito wa ukoloni, ambao unaleta mateso mabaya zaidi juu yake, na kuuacha bila furaha ya Idd au furaha katika maisha yake, nchini Palestina, Lebanon, Sudan, Iran, Yemen, Syria, na kwengineko, hivyo kuunyima furaha ya Idd na furaha ya masiku bora ﴿وَلَيَالٍ عَشْرٍ﴾ “Na kwa masiku kumi” [Al-Fajr: 2]
Trump yule mwenye kiburi huwatoa povu mdomoni, ngurumo na ghadhabu, huwashambulia Waislamu na ardhi zao, na kuwatishia moto wa kuzimu isipokuwa wamtii. Mshirika wake wa karibu na mwenzake, Netanyahu, hunguruma na kukandamiza ardhi za Waislamu, akiapa kuunda Mashariki ya Kati mpya kulingana na maono na ndoto zake. Dola zengine za kikoloni ziko pamoja nao, zikiwaunga mkono na kuwatia nguvu mradi tu sisi ni wahanga na faraja yetu pekee iko pamoja nasi, si wao—kama Uingereza, Ufaransa, Australia, Ujerumani, na nyenginezo—au wanaangalia na hawafanyi chochote kuwasaidia wanaokandamizwa au kuwasaidia walio na shida. Kuhusu watawala wa Waislamu, wao ni wabaya zaidi, kwani wanakula njama dhidi yetu badala ya kusimama nasi, wakiisaidia Amerika katika kiburi chake na Mayahudi katika uhalifu wao. Mbora kati yao ni yule anayetazama hili, akihesabu wahanga au kulaani kwa ulimi wake wa kinafiki.
Haya ni baadhi ya mambo yanayosumbua maisha yetu na kuharibu furaha yetu. Kinyume chake, bado kuna bishara njema za faraja inayokaribia na mwamko utakaobadilisha meza kwenye ukoloni na kuunda upya mandhari ya kisiasa kwa njia ambayo itawafurahisha waumini. Umma wa Kiislamu unazidi kuwa na nguvu siku hadi siku na kuonyesha uthabiti ambao Magharibi haikutarajia. Umewakataa watawala wake wahalifu na hauwaamini tena baada ya nyuso zao kufichuliwa, dosari na usaliti wao kuonekana wazi, na wakautelekeza katika nyakati za giza na hali ngumu zaidi. Imani hii pekee inatosha kuleta mabadiliko katika mchakato wa mabadiliko unaotarajiwa﴿إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ﴾ Tunamuomba Mwenyezi Mungu siku hiyo iwe karibu.
Kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye amesema: «مَا مِنْ أَيَّامٍ الْعَمَلُ الصَّالِحُ فِيهِنَّ أَحَبُّ إِلَى اللهِ مِنْ هَذِهِ الْأَيَّامِ الْعَشْرِ»، “Hakuna siku ambazo amali njema inayofanywa ndani yake inapendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko siku hizi kumi”, wakasema: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hata Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu? Akasema (saw): «وَلَا الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللهِ، إِلَّا رَجُلٌ خَرَجَ بِنَفْسِهِ وَمَالِهِ فَلَمْ يَرْجِعْ مِنْ ذَلِكَ بِشَيْءٍ». “Hata Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, isipokuwa kwa mtu ambaye atatoka kwa nafsi yake na mali yake kisha visirudi vyote (nafsi na mali)”
Basi hii ni fursa kwa kila mja mcha Mungu kuzitumia siku hizi zenye baraka kuunganisha mkono na juhudi zake katika kampeni ya kufanya kazi ili kufikia faradhi kubwa zaidi ya zama zetu, ambayo ni kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, ili tuweze kurudi kuwa Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, na kupewe izza kwa Uislamu.
Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha illa Allah... Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa Lillahi al-Hamd
Mhandisi Salah Eddine Adadah
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today |