Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
| H. 6 Muharram 1448 | Na: H 1448 / 003 |
| M. Jumapili, 21 Juni 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
[قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ]
“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Aal-i-Imran: 118]
(Imetafsiriwa)
Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz alitangaza mnamo Ijumaa kupinga kwake Muungano wa Ulaya kuweka vikwazo kwa umbile la Kiyahudi, huku Ufaransa ikitangaza kwamba haitakubali kuondoa vikwazo vilivyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Iran isipokuwa makubaliano yoyote ya mwisho kuhusu mpango wake wa nyuklia yajumuishe kushughulikia mpango wake wa makombora ya masafa marefu na uungaji mkono wake kwa makundi yenye silaha katika eneo hilo.
Viongozi wa Magharibi wanaendelea kufichua uovu wao na chuki yao ya ndani. Huku wakishuhudia uhalifu wa kikatili unaofanywa na Mayahudi dhidi ya Waislamu nchini Palestina, Lebanon, na Iran, na kuona kiburi na ufisadi wao Duniani, wakipuuza maadili, kanuni, na makubaliano yote—kuwaua watoto, wanawake, na watu wasio na ulinzi, na kuharibu kila kitu kilicho njiani mwao—Chansela wa Ujerumani anatangaza kukataa kwake kuweka vikwazo kwa umbile la Kiyahudi, ingawa vikwazo hivyo vinaweza kuwa vya nembo tu na havina athari halisi uwanjani. Anakataa wazo hilo kabisa kwa sababu Waislamu na ardhi zao ndio waathiriwa. Vile vile, Ufaransa inakataa kuondoa vikwazo kwa Iran hadi itakaposaini ahadi na makubaliano yanayohakikisha kwamba Iran haitainuka tena na kutishia umbile la Kiyahudi.
Mandhari hii inaashiria chuki inayofurika kutoka pande zao kuelekea kila kitu kinachohusiana na Uislamu na Waislamu. Hawawezi kuvumilia kuweka chuki hii ndani ya nafsi zao, kwa hivyo inajitokeza kuwafichua na kufichua uadui wao wa waziwazi dhidi ya Uislamu na Waislamu na upendo na uaminifu wao kwa Mayahudi wanyakuzi, hata kama watafanya ukatili na mauaji ambayo hata wanyama wa pori wangejiepusha nayo.
Huyu ndiye kafiri Magharibi, ambaye anadai kujali usalama, utulivu, amani, na haki za binadamu, lakini kiuhalisia, anatafuta kuwatawala Waislamu na ardhi zao. Anatamani usalama na amani, lakini si kwa Waislamu au wanadamu wote; badala yake, anatafuta kwa wakoloni makafiri pekee. Anatamani utulivu na amani, lakini si kwa Waislamu au ardhi zao; badala yake, anatafuta amani inayodhamini maslahi yake na kuzifanya nchi zetu zimtii. Anatamani haki za binadamu, lakini si kwa watu wote; badala yake, anazitafuta kwa ajili ya makafiri pekee, si kwa Waislamu.
Hili ndilo umbile halisi la kafiri Magharibi, na yeyote anayefikiri vyenginevyo amedanganywa. Waislamu hawana nusra au msaidizi isipokuwa wao wenyewe, baada ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni wana wao tu katika majeshi ndio watakaowakomboa wao na ardhi zao kutokana na udhalilifu na ukoloni. Hivyo basi, toeni msaada wenu (Nusra), Enyi majeshi!
[إِنَّ اللّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُواْ مَا بِأَنْفُسِهِمْ]
“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar-Ra’d: 11]
Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Afisi Kuu ya Habari |
Address & Website Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43 www.hizbuttahrir.today |
Fax: Telefax E-Mail: media (at) hizbuttahrir.today |