Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  12 Rajab 1447 Na: 10 / 1447 H
M.  Alhamisi, 01 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pindi Uwakilishi Unapokuwa Badali ya Wahyi

(Imetafsiriwa)

Kuapishwa kwa Zohran Mamdani mnamo tarehe 1 Januari 2026, kama wengi kabla yake, kunasherehekewa kama hatua muhimu kwa “uwakilishi wa Waislamu” ndani ya demokrasia ya Magharibi. Hata hivyo, zaidi ya siasa za nembo na utambulisho kuna swali zito zaidi, ambalo linagusa msingi wa itikadi ya kisiasa ya Uislamu: Je, inaruhusiwa kwa Muislamu kushikilia wadhifa wa utunzi wa sheria?

Nyakati kama hizo za kuonekana kisiasa bila shaka huibua maswali muhimu kwa Waislamu kuhusu kanuni kuliko uwakilishi tu pekee. Uislamu haupimi vitendo kulingana na umaarufu, nembo, au manufaa yanayo dhaniwa, bali kulingana na muongozo wa wahyi. Kama Waislamu, vitendo vyetu hupimwa kwa kufuata kwake wahyi na si kwa kukubalika kijamii au manufaa ya kisiasa. Jambo kuu katika tathmini hii ni swali la nani ana haki ya kutunga sheria.

Demokrasia si utaratibu wa utawala usioegemea upande wowote au usio na thamani. Imejikita katika usekula na kanuni kwamba ubwana uko kwa wanadamu, unaoonyeshwa kupitia sheria ambapo sheria hutungwa, hurekebishwa, au kufutwa kulingana na maoni ya wengi. Uislamu, kwa upande mwingine, unatakwa bila shaka kwamba ubwana na sheria ziwe kwa Mwenyezi Mungu (swt) pekee. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنِ ٱلْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ]

Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu. [Yusuf: 40].

Tangazo hili haliachi utata wowote kuhusu chimbuko la sheria na mamlaka katika Uislamu. Ni Mwenyezi Mungu (swt) pekee, ambaye hana upendeleo, maslahi binafsi, na makosa, anayeweza kuwa Mtunga Sheria wa kweli na wa haki. Wanadamu, kwa upande mwingine, wana kikomo kimaumbile, huwa na tamaa, shinikizo, kutofautiana, na dhulma, na kufanya madai yao ya mamlaka ya kutunga sheria kuwa na dosari kimsingi.

Licha ya kanuni hii, wanasiasa Waislamu wameapa mara kwa mara kuunga mkono katiba zilizotungwa na wanadamu ambazo zinagongana na sheria za Mwenyezi Mungu (swt). Kiapo cha Zohran Mamdani cha afisi kwa Qur’an hakifanyi kitendo hiki kuwa cha uwakilishi au cha kusherehekewa. Badala yake, ni tangazo la utiifu wa kisiasa. Ni kiapo cha kuufunga Uislamu katika imani na ibada ya kibinafsi, huku kikithibitisha utawala, sheria, na maisha ya umma kubaki chini ya mamlaka ya kisheria yaliyotungwa na mwanadamu. Mwenyezi Mungu (swt) Anatoa onyo lililo wazi na kali kuhusiana na mambo kama hayo:

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَـٰفِرُونَ]

Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri. [Al-Maidah: 44]

[فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ]

“…basi hao ndio madhaalimu. [Al-Maidah: 45]

[فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْفَـٰسِقُونَ]

“…basi hao ndio wapotofu. [Al-Maidah: 47].

Aya hizi zinasisitiza kwamba kuhukumu kwa kitu chengine kando na kile ambacho Mwenyezi Mungu amekiteremsha si suala la pembeni wala si la pili, wala si jambo linalosamehewa kwa nia njema, umuhimu wa kisiasa, au hadhi ya wachache. Badala yake, ni jambo la msingi la imani kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kujisalimisha Kwake (saw).

Watetezi wa ushiriki wa kisiasa mara nyingi wanasema kwamba kujihusisha ndani ya mifumo ya kidemokrasia ya kisekula huruhusu Waislamu “kubadilisha mfumo kutoka ndani.” Hata hivyo, miongo kadhaa ya ushiriki wa kisiasa wa Waislamu katika nchi za Magharibi imethibitisha kinyume. Licha ya kuongezeka kwa uwakilishi, mauaji ya kaka na dada zetu huko Gaza, Sudan, Syria, Turkestan Mashariki, Kashmir, na kwengineko yanaendelea bila kuzuiwa. Uhalisia huu unafichua kazi halisi ya ujumuishaji wa kidemokrasia - sio uwezeshaji, bali udhibiti. Kwa kuwaoanisha Waislamu ndani ya mitambo yake, mfumo huo huzima upinzani huku ukihifadhi misingi yake ya kimfumo.

Uislamu hautetei uwakilishi wa kinembo na ulegezaji msimamo ili kujioanisha ndani ya utawala wa kisekula. Badala yake, unahitaji uongozi wenye msingi wa wahyi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) hakutafuta kiti katika mabaraza ya Maqurayshi, wala hakujaribu kurekebisha sheria ya kabla ya Uislamu (Jahiliyyah) kutoka ndani. Badala yake, (saw) alifanya kazi ya kuanzisha mamlaka juu ya Uislamu wenyewe.

Umma hauteseki kutokana na ukosefu wa watu mashuhuri wa Kiislamu walio madarakani. Badala yake, unateseka na ukosefu wa mamlaka ya Kiislamu. Hadi Waislamu watakapokataa ahadi ya uongo ya ushiriki wa kisiasa wa kisekula na kujitolea kuregesha utawala kupitia Uislamu, uwakilishi utabaki kuwa ubabaishaji na utiifu wa kisiasa kimsingi utabaki kuwa mahali pabaya.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.