Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  5 Safar 1447 Na: H 1447 / 06
M.  Jumatano, 30 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ni Lazima ikumbukwe kwamba Marekani ni Nchi ya Kikoloni; Kujisalimisha kwa Sera zake za Ushuru Kutahatarisha Ubwana wa Taifa!

(Imetafsiriwa)

Marekani, mchuuzi wa kimataifa wa ubepari, imeibua 'dhoruba ya ushuru' duniani kote, ikipuuza kanuni za uchumi wa soko huria – moja ya falsafa kuu za ubepari – na sheria na kanuni za kile kinachojulikana kama Shirika la Biashara Duniani (WTO) ililounda. Hii, kwa mara nyingine, inathibitisha kwamba mfumo wa kibepari hauna utu na wa kinyonyaji. Serikali ya mpito ya Bangladesh imetabanni sera ya utiifu katika kukabiliana na hatua za ushuru za Marekani. Tayari wamefanya uamuzi wa kujitoa mhanga kununua ndege 25 za gharama kubwa aina ya Boeing, pamoja na kuagiza pamba na LNG kutoka Marekani, ingawa nchi nyingi zinaghairi oda zao kutokana na utendakazi duni wa Boeing. Na wanafanya mikutano ya moja kwa moja na Marekani, wakiweka umma katika giza kupitia 'makubaliano fiche ya kihistoria' (NDA). Sababu ni kwamba wananchi wenye ufahamu wa nchi hii, wanasiasa waaminifu, na wasomi wanajua kwamba Marekani inataka kuitumia Bangladesh kama kibaraka wa kieneo na inatamani sana kutekeleza miradi yake ya kikoloni katika eneo hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِن يَثْقَفُوكُمْ يَكُونُوا لَكُمْ أَعْدَاءً وَيَبْسُطُوا إِلَيْكُمْ أَيْدِيَهُمْ وَأَلْسِنَتَهُم بِالسُّوءِ]

“Wakikuwezeni wanakuwa maadui zenu, na wanakukunjulieni mikono yao na ndimi zao kwa uovu...” [Surah Al-Mumtahina: 02].

Wanauchumi wa kibepari, licha ya ujuzi wao wa uchumi wa kisiasa, ni wajinga kiasi kwamba wanaitazama sera ya ushuru ya Marekani kwa mtazamo wa kiuchumi pekee na wanashindwa kupata suluhisho zaidi ya hatua za kiuchumi za kukabiliana nazo. Wamarekani wangepokea jibu linalostahiki lau serikali ya mpito ingeyafukuza makampuni ya Kimarekani kutoka kwa sekta ya nishati ya Bangladesh kama jibu kwa sera hii ya kinyama ya ushuru ya Amerika. Walakini, suala hili halijazingatiwa hata katika hesabu ya nakisi ya biashara ya Marekani -Bangladesh. BNP yenye uchu wa madaraka imewalaghai wananchi kwa kuahidi ushirikiano kamili kwa serikali katika kuamiliana na ushuru wa Marekani. Wakati Marekani inaendeleza udhibiti wake juu ya Bangladesh, baadhi hawajasita kutoa zawadi ya sare za Jamdani kwa wanadiplomasia wa Marekani. Kwa niaba ya Hizb ut Tahrir, tunaionya serikali ya mpito: Marekani ni nchi ya kikoloni; jiepusheni kuingia nayo makubaliano yoyote ambayo ni kinyume na maslahi ya nchi. Badala yake, fursa hii lazima itumike ili kuepuka aina zote za utegemezi, ikiwemo biashara, kwa Marekani.

Enyi watu, watu walio na ufahamu kisiasa wanajua kwamba Marekani imerudia mara kadhaa kusukuma uchumi wa dunia katika mdororo kutokana na sera zake za Kikoloni za Kibepari. Sasa imetangaza vita vya kibiashara ili kuanzisha udhibiti wake wa upande mmoja juu ya dunia. Sera za biashara ya upande mmoja na ushuru mpya wa Marekani ni tishio kwa biashara ya kimataifa [Dkt. Moazzem, Mkurugenzi wa Utafiti, CPD]. Sasa, kwa hakika, ‘ndoto’ ya uchumi wa soko huria imefichuliwa kwa wanauchumi wa kisasa.

Mfumo wa Khilafah pekee ndio utakaoifanya nchi kujitegemea kiuchumi na kubadilisha sera za kiuchumi zinazotegemea FDI (Foreign Direct Investment). Utang'oa taasisi za Kikoloni za Marekani, kama vile IMF na Benki ya Dunia, kutoka nchi hii na kuanzisha uchumi unaoongoza kwa msingi wa Uislamu, na kuuleta ulimwengu chini ya kivuli cha uchumi wa uadilifu na uwiano. Mnajua kwamba Hizb ut Tahrir hapo awali iliwasilisha manifesto ya sera za kiuchumi zinazo ongoza za Khilafah katika makongamano mbalimbali ya ndani na kimataifa. Kwa hiyo, unganeni na uongozi wa dhati na wenye maono wa Hizb ut Tahrir na songeni mbele kusimamisha Khilafah. Mwenyezi Mungu ﷻ asema:

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنْ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Surah Al-A'raf: 96].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.