Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  7 Dhu al-Hijjah 1447 Na: 1447 H / 29
M.  Jumapili, 24 Mei 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kutoka kwa Ramisa hadi kwa Waathiriwa wa Epstein: Ulimwengu Unahitaji Mfumo wa Khilafah

(Imetafsiriwa)

Ramisa Akter, mwenye umri wa miaka minane, ambaye alipenda shule na alikuwa na ndoto ambazo kamwe hakuna mtu atakayejua, aliingia chumbani kwa jirani na kubakwa na kukatwa kichwa. Alistahili kitu bora kuliko hashtag.

Bangladesh imekasirika. Wanasiasa wanataka adhabu ya kifo. Baadhi wanataka Shariah ya Kiislamu lakini si mfumo unaoitabikisha. Visimamo vya kulaani na hashtag hazifikii chochote. Hakuna atakayezuia Ramisa anayefuata. Mzunguko: mtoto anakufa, umma unalipuka, viongozi hujifanya kughadhabika, sheria zinabadilishwa, kimya. Halafu mtoto mwengine.

Tunaishi katika thaqafa ya Kibepari inayouza mwili wa binadamu kwa faida. Ponografia ni tasnia ya mabilioni ya dolari. Ubepari unakuza anasa - raha kama lengo kuu kabisa la maisha. Utafiti unanasibisha ponografia na mitazamo potofu, uchokozi, na kuwageuza watoto kama vyombo vya matumizi. Ulishe utamaduni lishe hii, na wakatili wakubwa wataibuka.

Utamaduni wa unyama uliochangia mauaji ya Ramisa ni utamaduni ule ule wa kibepari, wa anasa unaosherehekewa katika duara za kipote cha mabepari. Jeffrey Epstein hakuwa mnyama pekee. Aliendesha mtandao wa biashara ya ngono ya watoto kwa miongo kadhaa. Taasisi zilijua. Watu wenye nguvu walitazama kando. Ubepari ule ule wa kiliberali, unaoruhusu, na unaoabudu utajiri unaoupa kisomo ulimwengu kuhusu uhuru, ulikuwa, katika viwango vyake vya juu, unalangua watoto. Ramisa alikuwa na umri wa miaka minane katika nyumba ndogo ya Pallabi. Waathiriwa wa Epstein walikuwa katika visiwa vya kibinafsi. Kufeli kimfumo kuna fanana: utamaduni wa kibepari, wa anasa ambao hauwalindi watoto kwa sababu unawaheshimu tu kama vyombo vya kutamaniwa au faida.

Kila wakati Ramisa anapotokea, mfumo wetu unaoitwa wa kidemokrasia hutoa haki ya kihamasa: kukamatwa, kushtakiwa, kunyongwa, kesi imefungwa. Lakini jamii hailindwi. Jamii ile ile inayodai kunyongwa inaendelea kuishi ndani ya utamaduni uliomzaa katili. Mfumo wa kibepari wa kisekula hauna ulinzi wa maana kwa watoto, hakuna udhibiti wa maudhui ya ukatili, hakuna uwajibikaji wa jamii, na mahakama zinazochukua miaka mingi. Haki ya kihamasa chini ya demokrasia ya kibepari ni ulaghai. Kumnyongwa mtu mmoja huku utamaduni ukiendelea kuwa huru si uadilifu. Ni ukumbi wa usanii.

Enyi watu, je, soi wakati sasa wa kutafuta njia badali halisi ya mfumo huu mbovu wa kisekula unaowafelisha wanawake na watoto wetu? Kwa miaka 1,400, Khilafah ya Kiislamu ilitoa njia tofauti - sio utopia ya kimapenzi (Uislamu kamwe haudai uhalifu hutoweka), bali mfumo unaoondoa vyanzo vya uhalifu na, ukiukaji unapotokea, hutoa haki ya haraka, kali, na ya heshima. Wakati mwangalizi wa mtumwa alipomlazimisha msichana mtumwa kinyume cha mapenzi yake, Khalifa Umar (ra) alimfanya apigwe viboko na kufukuzwa, na akakataa kumwadhibu mwathiriwa kwa sababu alilazimishwa - akithibitisha kwamba Uislamu unamchukulia katili huyo kuwa ndiye anayewajibika pekee, sio dhaifu. Wakati binti mayatima wadogo wa wafanyibiashara walipochukuliwa mateka na Raja Dahir wa Sindh (711 M), Al-Hajjaj alituma jeshi chini ya Muhammad ibn Qasim ambalo liliwaokoa na kulikomboa eneo hilo. Wakati mtoto mmoja alipotekwa nyara na kusilimishwa kwa nguvu, Khalifa wa Abbasiya al-Mahdi aliamuru arudishwe na kuwaadhibu watekaji nyara. Khalifa hakusubiri visimamo vya kulaani na hashtag - alihamasisha majeshi kwa ajili ya watoto walio hatarini.

Khilafah ilijenga jamii ambapo uchafu haukuwa burudani, wanawake na watoto hawakuwa bidhaa, ponografia haikuchafua akili, na dola iliwalinda walio dhaifu. Kilio cha mwanamke mmoja kingeweza kuhamasisha jeshi. Hiyo ndiyo tofauti. Khilafah Rashida kwa njia ya Utume si mfumo wa adhabu tu - ni mfumo pekee unaoondoa kabisa mazingira ya kuzalisha wakatili.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.