Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  17 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 1446 / 22
M.  Ijumaa, 13 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Afisi ya NATO nchini Jordan: Kujisalimisha kwa Nchi na Kuahidi Kutumikia Maslahi ya Kikoloni ya Maadui wa Ummah
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Alhamisi, 12 Juni 2025, Jordan na Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) walitia saini makubaliano jijini Brussels ili kuwa mwenyeji wa afisi ya mawasiliano ya kidiplomasia ya muungano huo katika mji mkuu, Amman. Makubaliano hayo yalitiwa saini kwa niaba ya Jordan na Balozi Yusuf Bataineh, balozi aliyeidhinishwa katika NATO, na kwa niaba ya muungano huo na Javier Colomina, Mwakilishi Maalum wa NATO kwa jirani wa Kusini, ambaye alisifu uhusiano uliotukuka na Jordan na kuthamini ukaribishaji wa afisi ya Jordan na dori yake kuu katika kanda, akiizingatia kuwa mshirika wa kutegemewa kwa muungano huo katika nyanja tofauti tofauti.

Katika uamuzi wa awali wa Baraza la Mawaziri katika kikao chake kilichofanyika mnamo tarehe 4 Mei 2025, chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu Jaafar Hassan, ilielezwa kuwa kupitishwa kwa makubaliano hayo na NATO kunakuja sambamba na maslahi ya dola ya Jordan na mwelekeo wake wa kufungua makao makuu ya afisi ya mawasiliano ya NATO, kama sehemu ya kuvutia mashirika mengi iwezekanavyo ya kimataifa kuufanya Ufalme huu kuwa kitovu cha Mashirika ya kimataifa na kieneo.

Katika Mkutano wa Viongozi wa NATO wa 2024 jijini Washington, muungano huo ulipitisha uamuzi wa kuanzisha afisi ya mawasiliano nchini Jordan – ya kwanza ya aina yake katika eneo hili. Wakati huo, Wizara ya Mambo ya Nje na Wageni ilisisitiza kwamba uamuzi wa kufungua afisi hiyo unawakilisha "hatua muhimu katika ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya Jordan na muungano huo, na inapongeza mafanikio ya muda mrefu ya Jordan katika kupambana na vitisho vya mipaka kama vile ugaidi na itikadi kali kali."

Muungano huu wa kijeshi wa kimataifa umejikita katika uhodari, upanuzi, na utawala wa kikoloni wa Magharibi unaoongozwa na Amerika na Ulaya, na katika kuwasha vita vya ndani na vya kikanda ambavyo vimeiingiza dunia katika migogoro na mivutano isiyokwisha. Ulianzishwa baada ya Vita Vikuu vya II vya Dunia wakati nchi 12 waanzilishi zilitia saini Mkataba wa NATO mwaka 1949 ili kulinda nchi za Ulaya kutokana na tishio la Umoja wa Kisovieti wakati huo. Baada ya Mkataba wa Warsaw kumalizika kwa kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti, NATO ilipaswa kuvunjwa, lakini Amerika ilikuwa na hamu ya kuendelea na kudumisha utawala wake juu ya nchi za Magharibi hasa Umoja wa Ulaya na kuutumia dhidi ya nchi nyingine.

Uhalali ulitungwa kwa ajili ya kuendelea kuwepo kwake, kama vile "Vita dhidi ya Ugaidi," ambavyo vina maana ya vita dhidi ya Uislamu. NATO iliunda kile ilichokiita ushirika na miungano kupitia mifumo ya kikanda kama vile Mazungumzo ya Mediterania na Mpango wa Ushirikiano wa Istanbul, na hata ushirika wa watu binafsi wa hali ya juu na baadhi ya nchi kama Jordan, kuhudumia maslahi ya kimkakati ya NATO, na kuigeuza kuwa chombo cha kikoloni mikononi mwa Amerika.

Ama kuhusu dori ya afisi ya NATO jijini Amman, ilielezwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg kama ifuatavyo: "Jordan inachukuliwa kuwa mshirika wa muda mrefu na anayethaminiwa sana wa NATO." Msemaji wa kikanda wa Idara ya Wizara ya Kigeni ya Marekani, Samuel Werberg, alisema katika mahojiano na Shirika la Habari la Jordan kando ya mkutano uliopita wa NATO kwamba nchi yake inathamini dori muhimu inayochezwa na Ufalme huu katika utulivu wa kikanda.

Kauli hizi za NATO na maafisa wa Marekani zinaonyesha kuwa utawala wa Jordan umekuwa ukitekeleza dori yake uliyopewa tangu kuanzishwa kwake kama chombo cha kiutendaji kinacholinda maslahi ya wakoloni wa Magharibi, hasa miongoni mwao ni uwezeshaji na uhifadhi wa umbile la Kiyahudi kama Uingereza, na baadaye Marekani na Ulaya, kiongozi wa kimkakati wa kutekeleza miradi ya kikoloni na kuzuia Ummah na mwamko wa Kiislamu kufikia mradi wake wa Khilafah Rashida. Utawala huu kuwatelekeza watu wa Gaza ni mfano wa wazi wa utiifu huu na wa huduma ambazo kwazo dori ya Jordan inainuliwa ili kutumia rasilimali na watu wake kumtumikia kafiri wa kikoloni kwa kufungua afisi ya mawasiliano ya NATO.

Utawala huu haukuishia kwenye makubaliano ya pamoja ya ulinzi na Marekani; pia ulianzisha kambi za kijeshi kwa ajili ya Marekani na Ulaya na kuruhusu maelfu ya askari wao kuwekwa kwenye eneo lake si kwa madhumuni yoyote isipokuwa kulinda umbile la Kiyahudi na maslahi ya mkoloni Magharibi. Hii ndiyo dhamira ya kweli nyuma ya ushirikiano unaotarajiwa ambao unaweza kuonekana kutokana na ufunguzi wa afisi ya mawasiliano ya NATO, kutumikia maslahi yake katika utawala na udhibiti, na kutumia uwezo wa usalama, jeshi, vifaa, na mtandao wa Jordan, kuruhusu Amerika kushughulika na vita vyake vya ushindani na utawala.

Utawala huu umekwenda mbali zaidi katika kuiweka Jordan katika jicho la hatari na katika kukusanya rasilimali na vikosi vyake ili kuwalinda maadui zake na kuupiga vita Uislamu na watetezi wake. Umenyamazisha sauti na kumkandamiza kikatili mtu yeyote anayefichua uhalisia wake kupitia ukamataji, unyanyasaji, na mateso. Umekusanya kundi la vikaragosi, wanaojulikana sana kwa Ummah ili kupamba khiyana na matendo yake maovu. Shughuli za miungano ya kijeshi, hivi karibuni ikiwa ni afisi ya NATO juu ya ardhi za Waislamu, kama vile usalama na ushirikiano wa mtandao na mazoezi ya kijeshi kama "Eager Lion" yaliyofanywa nchini Jordan kwa zaidi ya muongo mmoja, pamoja na makubaliano ya kijeshi na kiusalama kuhusiana na kambi, viwanja vya ndege, na bandari, huipa NATO uzoefu wa kivitendo wa umuhimu mkubwa ambao matokeo yake yanaathiri maisha, damu, na matukufu ya Waislamu, na kuzipa nchi za kikafiri nguvu juu ya ardhi za Kiislamu. Hili linadhoofisha ubwana wa dola juu ya ardhi yake yenyewe jambo ambalo ni haramu katika Uislamu, kwa kuwa inawapa makafiri mamlaka juu ya waumini.

[وَلَنْ يَجْعَلَ اللهُ لِلْكَافِرِينَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ سَبِيلاً]

wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surat An-Nisa:141]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.