Hizb ut Tahrir Ndio Inayofanya Kazi Ipasavyo Kusimamisha Khilafah Basi Acheni Kuvuruga Ulinganizi Wake na Kuwakamata Wanachama Wake
- Imepeperushwa katika Jordan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Tangu kuanzishwa kwake kama chama cha kisiasa chenye msingi wa Uislamu mwaka 1953, Hizb ut Tahrir imefanya kazi ya kurudisha mfumo kamili wa Kiislamu wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Kiislamu, ambayo dola yake ya kwanza ilianzishwa na Mtume Muhammad (saw) mjini Madina. Ingawa inafuata njia ya Mtume (saw) ya kusimamisha dola hii, haijishughulishi na kitendo chochote cha kinguvu au kile kinachoitwa vurugu katika kufanya hivyo.