Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  18 Dhu al-Hijjah 1446 Na: 1446 / 23
M.  Jumamosi, 14 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utawala wa Jordan Unalilinda Umbile Adui la Kiyahudi kwa Kuyapangua Makombora na Droni Zinazoelekezwa kwake
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Ijumaa, tarehe 13/6/2025, alfajiri, umbile la Kiyahudi lilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran, yakilenga vituo vyake vya nyuklia, viwanda vyake vya makombora ya balestiki, na viongozi wa kijeshi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa maisha na mitambo ya kijeshi na ya kiraia, kwa msaada na ushirikiano wa Marekani. Iran, kama kawaida, iliapa kutoa jibu kali na baya kwa umbile la Kiyahudi kupitia mashambulizi ya droni na makombora. Ilitekeleza mawimbi ya mashambulizi haya asubuhi na jioni ya siku hiyo hiyo, yakivuka anga ya Iraq, Syria, na Jordan. Baadhi ya mashambulizi haya yalisababisha uharibifu kwa baadhi ya vifaa katika miji ya umbile hilo, kabla ya baadhi yake kupanguliwa katika anga ya jirani kabla na baada ya kufika kwenye umbile la Kiyahudi.

Katika muktadha huu, mkuu wa serikali hii alisema kuwa Jordan haitakuwa uwanja wa vita kwa mzozo wowote, na haitaruhusu usalama na uthabiti wake kutishiwa. Waziri wa Mambo ya Nje, Safadi, alisema kuwa Jordan haitaruhusu ubwana wake kukiukwa au usalama wake kutishiwa. Duru moja ya kijeshi ya kuaminika katika Kamandi Kuu ya Vikosi vya Wanajeshi wa Jordan - Jeshi la Kiarabu ilithibitisha kwamba ndege za Jeshi la anga la Jordan na mifumo ya ulinzi wa anga ilinasa, mnamo siku ya Ijumaa asubuhi, idadi kadhaa ya makombora na droni ambazo ziliingia anga ya Jordan, ikimaanisha zile zinazokuja kutoka Iran kuelekea umbile la Kiyahudi.

Kwa hatua hizo, utawala huu unathibitisha kile kinachojulikana kuhusu utawala huu tangu kuasisiwa kwake, kwamba dhima yake ya kisiasa na kijeshi ni kulinda na kulipa nguvu umbile la Kiyahudi kutokana na hatari zinazoweza kutishia uwepo wake. Rekodi yake iliyovunjwa katika kuhalalisha upanguaji wake wa droni na makombora hayo - kwamba ni kulinda usalama wake, utulivu na raia - hakuhadai tena mwana Jordan yeyote. Ilianza kutenda bila aibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake au umma wa Kiislamu, katika kutetea umbile la Kiyahudi kupitia mikataba, makubaliano na usalama na ushirikiano wa kijeshi ambao haukukoma hata wakati wa vita vya mauaji ya halaiki, uhamishwaji na njaa ya watu wa Gaza. Vita ambavyo haikunusuru kwa majeshi yake; ambayo kwayo inalilinda umbile la Kiyahudi kutokana na makombora yanayolishambulia. Mwenyezi Mungu (swt) anawaonya watawala kama hawa kwa kusema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu. [Al-Ma’idah: 51].

Utawala huu upende usipende, Mayahudi na umbile lao ni adui wa kwanza wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na watu wa Jordan. Mnaweza kuona furaha inayojaza nyoyo za watu wanapoona makombora yakielekea kwenye umbile la Kiyahudi, na jinsi matumaini yao yanapokatizwa wanapopanguliwa na kutunguliwa kabla ya kulifikia.

[لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ النَّاسِ عَدَاوَةً لِّلَّذِينَ آمَنُوا الْيَهُودَ]

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi [Al-Ma’idah: 82].

Amerika, ambayo watu wa Jordan wanaizingatia kuwa adui, ndiyo inayolisambazia umbile hili vifaa na nyenzo. Ni adui wa Uislamu na Waislamu. Ndiyo iliyoiangamiza Iraq, Afghanistan, Syria, Yemen na Sudan, moja kwa moja au kupitia vibaraka wake. Hivyo basi utawala huu na ujifunze kutokana na haraka yake ya kufikia maslahi yake na kuwalinda Mayahudi, kwani wao hawana washirika isipokuwa maslahi yao binafsi.

Enyi Waislamu, Enyi Majeshi ya Waislamu: Wakati umefika wa nyinyi kumuitikia Mwenyezi Mungu na ahadi yake ya kuwapa tamkini pale mnapoitikia maamrisho yake ya kusimamisha dola yenu ya Kiislamu na kutekeleza sheria yake. Wakati umefika wa kuwakataa watawala wenu ambao uvundo wao wa uhaini umekuwa wa kuudhi. Tunakuiteni kwenye utawala wa Uislamu na dola yake, ambayo ni chimbuko la heshima na hadhi yenu, na ambayo kwayo mtapata ushindi juu ya umbile la Kiyahudi na kuifurusha Marekani na Ulaya kutoka katika ardhi za Waislamu. Enyi watu wenye nguvu na ulinzi, ikiwa mmeshindwa kuwanusuru watu wa Gaza na kuasi amri za Mwenyezi Mungu, mnawezaje kutosheka na kulilinda umbile la Kiyahudi kwa kuzuia makombora yanayoelekea huko, kuleta hata madhara kidogo kwake?! Tembeeni muelekee Palestina, mukomboe Msikiti wa Al-Aqsa na Palestina iliyobarikiwa.

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْناً يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئاً وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.