Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  20 Muharram 1447 Na: 1447/02
M.  Jumanne, 15 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bwawa la An-Nahdha: Silaha Mpya ya Marekani ya Kuvunja Utashi wa Misri na Kuzuia Ukombozi Wake kutokana na Utiifu

(Imetafsiriwa)

Tangu Ethiopia ilipotangaza ujenzi wa Bwawa la Kuu la Ethiopia la An-Nahda Dam kwenye  Nile ya Samawati mwaka 2011, uhalifu mkubwa wa kisiasa na wa kimkakati umekuwa ukijitokeza. Wale wenye ufahamu wanaona sio tu kama jengo la maji au mradi wa maendeleo, lakini kama chombo kipya cha kikoloni kinachotumiwa na Amerika kutawala eneo hili - hasa Misri, kitovu cha ardhi za Kiislamu, ambayo inakusudiwa kubaki kudhalilishwa chini ya shinikizo la kiuchumi, kisiasa, na hata la maji, kama sehemu ya mtindo mpya wa vita visivyo vya moja kwa moja.

Licha ya matamshi rasmi ya Ethiopia kuhusu "haki ya maendeleo," ukweli ni kwamba bwawa hilo kamwe halikuwa uamuzi huru wa Ethiopia. Ni matokeo ya mipango iliyobuniwa kwa uangalifu ya Kiamerika iliyoanzia miaka ya 1950, wakati kampuni ya Kiamerika ya Brown and Root, chini ya usimamizi wa Afisi ya Marekani ya Urekebishaji Ardhi, ilifanya tafiti kuhusu ujenzi wa bwawa kwenye Nile ya Samawati. Eneo la sasa la bwawa liliteuliwa wakati huo kama moja ya miradi mikubwa ambayo ingeruhusu Amerika kuweka udhibiti wa kihaidrolojia juu ya Misri na Sudan.

Bwawa hili, basi, ni zao la ruwaza ya Marekani kwa eneo hili, sehemu ya zana zake za kuchora upya ramani ya utiifu barani Afrika, hasa Mashariki. Kama vile Amerika ilivyonyakua vyanzo vya utajiri katika Ghuba kupitia kwa watawala wake vibaraka, sasa inadhibiti chanzo cha Mto Nile kupitia ushawishi wake jijini Addis Ababa.

Ethiopia si chochote zaidi ya chombo kilicho mikononi mwa Amerika, kilichojaaliwa kutuma ujumbe wakati fulani unaokidhi maslahi ya Marekani katika eneo hilo, kama vile utawala wa Misri, ambao unajifanya kupinga lakini hausubutu kuchukua msimamo wowote wa kimaadili au wa kimaamuzi.

Bwawa la An-Nahdha haliwezi kutenganishwa na sera ya njaa na kizuizi kilichowekwa na Amerika kwa watu wa Misri. Maji ni uhai wa taifa lolote, na kuzuia sehemu kubwa yake nyuma ya bwawa hili huwezesha Amerika kutishia Misri kwa kiu na kuendesha maamuzi yake ya kisiasa na ubwana.

Amerika imesaidia bwawa hili sio tu kifedha lakini kwa ufadhili kamili wa kisiasa na kidiplomasia. Ilisimama katika majukwaa yote ya kimataifa na kikanda kuzuia jaribio lolote la kuishinikiza Ethiopia au kuilazimisha kutia saini makubaliano ya lazima. Leo, Amerika inasherehekea kukamilika kwake na inajiandaa kulitumia kama chombo cha kushinikiza watu wa eneo hilo, haswa wale wa Misri na Sudan.

Serikali ya Misri, huku ikidai ubwana, imechukua hatua tu kulingana na kile ambacho Amerika inaruhusu. Haikuchukua hatua wakati Ethiopia ilipotangaza bwawa hilo mwaka wa 2011, haikufanya lolote wakati wa ujazaji wa kwanza, ilibaki kimya hata baada ya kujazwa kwa mara ya nne, na sasa, baada ya Ethiopia kutangaza kukamilika kwake, inatoa taarifa za kuwa na "manung’uniko" na "kukataa rasmi" bila kuchukua hatua zozote halisi. Kinyume chake, inaendeleza ushirikiano wa kiusalama na kijasusi na Washington na Tel Aviv, hata kama maisha ya mamilioni yako hatarini!

Kwa nini? Kwa sababu serikali hii sio mtawala wa kweli. Ni mwajiriwa tu wa bwana wake, Marekani, anayetekeleza sera zake, asiyesubutu kuvuka mipaka iliyowekwa kwa ajili yake, bila kujali matishio makubwa kiasi gani kwa nchi.

Hii ndiyo hali ya tawala zote zinazotawala hivi leo katika ulimwengu wa Kiislamu: tawala vikaragosi, zisizo na uwezo wa kufanya maamuzi, zikienda tu kulingana na ajenda za Magharibi na kuridhika kwa ukoloni.

Mto Nile sio mali ya Misri, Ethiopia, au Sudan kama dola za kitaifa zilizoibuka baada ya ukoloni. Ni mali ya umma inayosimamiwa na hukmu za Kiislamu. Imeharamishwa kabisa kwa chombo chochote kuzuia maji yake au kuyabadilisha ili kulazimisha uhalisia mpya juu ya Waislamu.

Je, tunawezaje kukubali kwamba Misri imezuiwa kupata maji ya Nile, au kwamba yamehifadhiwa nyuma ya bwawa linalodhibitiwa na Ethiopia au tuseme, kiuhalisia na Amerika? Je, Waislamu wanawezaje kunyamaza mbele ya uchokozi kama huo, ambao hauna tofauti na uvamizi wa kijeshi?

Ikiwa kuchunga mambo ya watu ni jukumu la dola, basi kuzuia uchokozi huu ni wajibu wake sio kwa kuwasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa au kutoa taarifa za kupinga, lakini kwa kukomboa utashi wa kisiasa kutoka kwa udhibiti wa kigeni, na kutumia nguvu iwapo italazimika kumzuia mvamizi na kuregesha haki. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[فَمَنِ اعْتَدَى عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَى عَلَيْكُمْ]

Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni.” [Al-Baqarah: 194].

Suala la Bwawa la An-Nahdha, kama masuala na migogoro yote ya ummah, linathibitisha kwamba tatizo haliko kwenye bwawa hilo pekee, wala Ethiopia peke yake, bali kwa kukosekana dola ya Kiislamu inayoshughulikia mambo ya watu, inayowalinda kutokana na uvamizi, na kuwalindia maji, chakula na usalama wao wa kisiasa.

Kwa hiyo, wajibu wa kidini na kisiasa wa Umma wa Kiislamu ni kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, Khilafah inayoondoa mipaka baina ya ardhi za Waislamu, kuwaunganisha chini ya uongozi mmoja, na kuuhifadhi Mto Nile kuwa mali ya umma kwa raia wake wote.

Enyi wenye ikhlasi katika jeshi la Misri, enyi wana wema wa Misri, nyinyi ambao nyoyo zenu bado zinawaka moto wa imani na heshima ya Kiislamu, nyinyi ambao mmeapa kuilinda Misri na watu wake, kuwa upanga wa Uislamu, si mjeledi wa madhalimu.

Je, sio wakati sasa wa kusema ukweli? Je, sio wakati sasa kwenu kusimama kama walivyofanya Umar, Khalid na Salahuddin? Je, sio wakati sasa kwenu kuondoa pote hili la wasaliti ambalo lilikabidhi shingo zetu kwa adui na kuuza maji ya Mto Nile kwa bei duni katika soko la utegemezi? Bwawa lililojengwa kwenye urefu wa Mto Nile sio bwawa tu, ni kisu cha sumu cha Amerika, inayosubiri wakati mwafaka kuwashambulia watu wenu kwenye kina cha maisha yao.

Historia inaandikwa, na leo munakabiliwa na fursa isiyosahaulika: Ima muwe wanaume ambao kupitia kwenu Mwenyezi Mungu atawapa ushindi na tamkini kwa kusimamisha utawala wa Uislamu na dola yake, na kuukata mkono wa Marekani kutoka Misri na watu wake au mubakie kimya na kunyenyekea, mukibeba dhambi ya kunyamaza na khiyana mpaka Siku ya Kiyama!

Kuweni wasaidizi wa Dini hii kama Answar walivyokuwa mjini Madina. Inueni bendera ya Uislamu, tangazeni kuangushwa kwa utawala kibaraka, na ifanyeni Misri kuwa nukta kianzio ili kuukomboa Ummah kutoka katika udhibiti na ukoloni wote na kusimamisha Khilafah Rashida yenye kuhifadhi maji ya Mto Nile, damu ya Waislamu, na hadhi yao.

Huu ndio wakati wenu, inukeni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama wafanyavyo wakweli... Ushindi unakusubirini, na Mwenyezi Mungu kamwe hapotezi ujira wa wafanyao wema.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ...]

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa …” [An-Nisa: 75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.