Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  28 Muharram 1447 Na: 1447/06
M.  Jumatano, 23 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Wanazuoni wa Al-Azhar: Ikiwa hamtasema neno la haki leo... lini basi?!
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo sura za mauaji yanayofanywa na Mayahudi mjini Gaza zikiongezeka, na chakula, dawa, na maji vikizuiliwa kwa watoto, wanawake na wanaume, Al-Azhar ilitoa tamko la kulaani "jinai ya kuweka njaa" inayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi. Taarifa hiyo ilifutwa baadaye! Basi je, inajuzu kilio dhidi ya dhalimu kifutwe?! Na je, sauti ya wanazuoni inaweza kukaa kimya dhidi ya mauaji?! Taarifa hiyo ilikuja ikiwa imejaa misamiati ya kibinadamu, yenye kuwavutia watu wenye dhamiri hai, jumuiya ya kimataifa, na dola zenye ushawishi, na kutoa wito wa kufunguliwa kwa vivuko na utoaji wa misaada. Umbile la Kiyahudi lilielezewa kuwa linafanya uhalifu wa njaa, likituhumiwa kwa mauaji ya halaiki na kuzuia misaada, na ilitoa wito kwa mashirika ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kimataifa kusonga mbele kufungua vivuko, pamoja na kuwaombea dua watu wa Gaza kwamba Mwenyezi Mungu awanusuru na alipize kisasi kwa ajili yao.

Lakini kilichokosekana katika taarifa hiyo – na ndio kiini cha jambo hilo – ni kwamba faradhi ya Kiislamu, ambayo lazima itolewe kutoka kwenye jukwaa muhimu kama Al-Azhar Al-Sharif, ni wito kwa majeshi kutaharaki, kuondolewa kwa tawala zinazolinda umbile la Kiyahudi kwa chuma na moto, na kutangaza haki mbele ya mtawala anayefunga kivuko, kuzuia chakula, na kula njama pamoja na Mayahudi.

Taarifa hiyo imegeuka kutoka katika faradhi ya Kiislamu na kuwa maandishi hafifu ya kibinadamu, ya kuuvutia mfumo wa kimataifa – yaani, kutafuta msaada kutoka kwa wahalifu wale wale wa kivita wenyewe – wakati Waislamu wana majeshi, zana, imani, na Shari'ah ambayo inawawajibisha kuwanusuru wanaodhulumiwa.

Al-Azhar ilipaswa kutangaza haki, sio kuificha. Kwani wanazuoni waongofu hawatosheki na kuelezea tu mikasa, bali hutangaza haki, wanaziita jinai kwa majina yake, huwafichua walaji njama, na hulingania kwa uwazi mabadiliko ya uovu.

Na sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Misri, tunathibitisha kwamba:

Serikali ya Misri ni mshirika kamili katika jinai ya kuwaua kwa njaa watu wa Gaza, kwa kuzuia misafara ya mshikamano pamoja nao kuvuka Misri, kufunga kivuko cha Rafah, na kuwatia nguvuni wale wanaowanyooshea mkono, hivyo kubana mambo juu yao kutoka kila upande.

Kukaa kimya kwa utawala huu, au kupuuza, ni kushiriki uhalifu. Na kauli ambazo haziufichui wala kufichua mabwana zake ni kauli za khiyana zilizofunikwa katika vazi la mahubiri.

Katika suala hili, tunawataka wanavyuoni wa Al-Azhar, kiongozi wao akiwa Sheikh wake, ikiwa yeye ni mkweli katika kujali damu ya Gaza, wachukue msimamo wa haki mbele ya mzingiro huu wa uoga, na watoe kilio cha wazi na dhahiri kutoka kwa Msikiti wa Al-Azhar kwamba utawala unaozuia nusra kwa Gaza una dhambi, na kuondolewa kwake ni faradhi, kuasi dhidi yake ni wajibu, na kwamba kuwanusuru watu wa Gaza kwa silaha ni faradhi juu ya majeshi ya Waislamu, na yeyote anayenyamaza juu ya hili ni mfichaji haki na mshirika katika uhalifu.

Na hatimaye, tunarudia wito wetu wa kuasisiwa Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, kwani ndio pekee inayotekeleza Uislamu, inayokusanya majeshi, itayong'oa mizizi ya umbile la Kiyahudi na kuikomboa Al-Aqsa na Palestina yote. Na tunawalingani askari wa Misri kufanya kazi pamoja nasi kwa ajili ya faradhi hii kubwa; huenda Mwenyezi Mungu akawakubalia na kuwasamehe kwa yale yaliyopita, na akawafanya wawe maanswari wa dini hii. Ewe Mwenyezi Mungu, ifanyie hima na uifanye Misri kuwa msingi wake, na uwajaalie askari wa Kinanah kuwa ni maanswari wake.

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَٰذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّاً وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيراً]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako [An-Nisa: 75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.