Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  2 Safar 1447 Na: 1447/08
M.  Jumapili, 27 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pindi Milango Inapofungiwa wenye Njaa na Kunusuriwa Kukanyimwa,
Sura Hasiri ya Serikali ya Misri na Wapambe wake Inafichuliwa
(Imetafsiriwa)

Katika wakati ambapo Gaza inastahamili moja ya nyakati kandamizi na za kikatili zaidi katika historia, ambapo, pamoja na kuuawa kwa mashambulizi ya mabomu, watoto wanakufa kwa njaa, wanawake kwa huzuni, na wazee kwa magonjwa, Meja Jenerali Khaled Mewaghar, Gavana wa Sinai Kaskazini, alitoa matamshi ambayo yanakinzana na matakwa rahisi zaidi ya  maadili ya kiakhlaki na ya kibinadamu matakwa ya udugu wa Kiislamu. Alisema: “Ikiwa watu wa Gaza watafikia kiwango fulani cha njaa, wana chaguzi tatu: ima kwenda upande wa Israel na kukabili milio ya risasi, kujitupa baharini, au kuelekea Misri—jambo ambalo haliwezekani.”

Haya ni maneno yanayoakisi msimamo rasmi wa kinyama usiostahiki kwa afisa wa umma katika nchi ya Kiislamu, baya zaidi, yanawakilisha uhalifu wa kisiasa dhidi ya kaka na dada zetu mjini Gaza, ambao wamekuwa wakivumilia mateso ya pamoja chini ya mzingiro wa pamoja uliolazimishwa na umbile la Kiyahudi na serikali ya Misri kwa zaidi ya miaka 18.

Serikali ya Misri kwa muda mrefu imekuwa ikipigia debe fikra kwamba inatoa msaada na afueni kwa watu wa Gaza na inasimama nao mbele ya uvamizi. Ilhali kauli za Mewaghar zinapomosha barakoa hii kikamilifu, zikifichua sura halisi ya sera rasmi ya Misri kwa Gaza: hakuna nusra, hakuna huruma, na hata ruhusa kwa waliokata tamaa au wenye njaa kupita! Jambo hilo limefikia hatua ya kuuita uingiaji wa watu wa Gaza nchini Misri kuwa “haiwezekani,” kana kwamba ni maadui.

Kauli hizi za gavana haziwezi kutazamwa tofauti na muktadha wa sasa wa kisiasa ambapo maamuzi ya Misri yamewekwa chini ya matakwa ya Marekani, ambayo yanakidhi matakwa ya Mayahudi. Kuzingirwa kwa Gaza sio tu uamuzi wa umbile la Kiyahudi; ni operesheni ya pamoja inayotekelezwa na serikali ya Misri chini ya uungaji mkono wa moja kwa moja wa Marekani, yenye lengo la kuvunja matakwa ya watu wa Gaza, kuwalazimisha kusalimu amri, na kuutia Ummah wote katika hali ya kukata tamaa na kukosa matumaini.

Kauli za Mewaghar zinaonyesha kwa usahihi mkakati rasmi ambao unaiona Gaza kama mzigo wa usalama badala ya jukumu la kidini. Inakuza utamaduni wa kuchafua jina la watu wa Gaza katika fikra za umma, na kuwaonyesha kama "tishio linalowezekana" ambalo lazima lizuiwe kuingia Misri kwa gharama yoyote, kana kwamba ni ugonjwa wa tauni au wavamizi, sio ndugu katika imani au wastahiki halali kwa lengo la haki. Lengo lao ni lengo la Ummah wote, sio lao peke yao. Ardhi ya Gaza, na Palestina yote, ni ardhi ya kharaji inayomilikiwa na Ummah mzima, na ukombozi na ulinzi wake ni faradhi juu ya Ummah wote, wa kwanza kabisa miongoni mwao ni watu na jeshi la Misri, kwani wao ndio walio karibu zaidi na wenye uwezo zaidi.

Pindi afisa anapotangaza waziwazi kwamba wenye njaa wanazuiwa kuingia katika nchi yake, akijua kwamba wanaweza kufa ikiwa hawatafanya hivyo, hii ni jinai kamili. Na ingawa idara potovu ya mahakama ya Misri haiwezi kumhisabu, Mwenyezi Mungu (swt) atamhoji Siku ya Kiyama, na historia haitamsamehe. Mtume (saw) amesema: «وَأَيُّمَا أَهْلُ عَرْصَةٍ أَصْبَحَ فِيهِمْ امْرُؤٌ جَائِعٌ فَقَدْ بَرِئَتْ مِنْهُمْ ذِمَّةُ اللَّهِ تَعَالَى» “Mtu akiwa na njaa katika jamii, basi dhima ya Mwenyezi Mungu (swt) inaondolewa kwao.”

Hadith hii inafuta nyudhuru zote za tawala zinazodai “kutopendelea upande wowote au” au “mazingatio ya kisiasa.” Ikiwa watu wa Gaza leo wanakufa kwa njaa, na milango ya Misri imefungwa dhidi yao, na wakanyimwa chakula na dawa – basi dhima ya Mwenyezi Mungu itaondolewa kutoka kwa tawala hizi, na kutoka kwa yeyote anayekula njama pamoja nao, akanyamaza juu ya vitendo vyao, au kuvihalalisha – iwe ni wanazuoni, wanahabari, au wanasiasa. Watu kama hao ni washirika katika khiyana, na dhima ya Mwenyezi Mungu imeondolewa kwao.

Enyi watu wa Gaza: Kuweni na subira na uthabiti. Muko juu ya haki. Nyinyi ndio wenye kusimama kidete mpaka Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu hatapoteza jihad yenu, na damu yenu haitamwagika bure.

Enyi Watu wa Misri, Enyi Watu wa Kinana: Jueni kwamba Mwenyezi Mungu atakuulizeni kuhusu Gaza, na kuhusu nchi yenu ambayo mipaka yake imefungwa kwa watu wake, na kuhusu ushirikiano wenu wa kimya kimya katika kuzingirwa kwao na njaa. Kwa hiyo, fanyeni haraka kuvunja mzingiro huo. Gaza leo haihitaji tu kauli za huruma au misafara tu ya misaada—inahitaji majeshi kuandamana, kuikomboa, na kuitakasa kutokana na Mayahudi.

[هَٰذَا بَلَاغٌ لِّلنَّاسِ وَلِيُنذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ]

Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.” [Surat Ibrahim: 52].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.