Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 20 Dhu al-Hijjah 1446 | Na: HTS 1446 / 69 |
M. Jumatatu, 16 Juni 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kuharibu Masoko kama vile Soko la Dokhinat ni Vita dhidi ya Watu katika Riziki zao na ni Matokeo ya Kukosekana kwa Dola ya Kiislamu ya Khalifah
(Imetafsiriwa)
Katika kitendo cha kikatili na vurugu, mamlaka za eneo la Jabal Awlia, Jimbo la Khartoum, kwa kutumia askari waliokuwa na silaha nyingi, walibomoa Soko la Tumbaku lililoko kwenye Barabara ya Jabal Awlia kwa tingatinga mnamo siku ya Alhamisi asubuhi, 12 Juni 2025, na kuvunja meza za maonyesho. Hata wale waliotoroka soko hilo na bidhaa zao hawakusazwa!
Soko la Tumbaku ni moja ya masoko ya zamani zaidi. Lilipanuka baada ya masoko yote ya ndani na masoko mengi ya Khartoum kufungwa kutokana na vita. Likawa kimbilio la watu kutoka eneo hilo, ambapo raia wasio wanajeshi walinunua mankuli, mboga na vyakula vyengine. Ni moja ya masoko ambayo bidhaa za wizi haziuzwi. Kwa hiyo, soko lilipanuka, na bei ilishuka kutokana na wingi wa bidhaa. Chakula kilipatikana kwa bei nafuu zaidi, na nafasi nzuri za kazi ziliundwa kwa watu wa eneo hilo baada ya vita hivi vilivyolaaniwa, ambavyo vilitatiza biashara na kuondoa ajira. Kwa sababu ya uharibifu huu, bei ilipanda sana kutokana na ukosefu wa usambazaji, ambao ulizidisha mateso ya watu.
Vurugu, ukatili na unyama unaofanywa na viongozi wa eneo hilo na vikosi vyao vililaaniwa na watu wa eneo hilo. Hakika, wengi wao walishangaa na kuuliza, "Je, sio wakati sasa kwa serikali kuacha mbinu zake za zamani, wakiitaja kuwa ni dola ya ukusanyaji ushuru ambayo inawachukiza watu ambao inawajibika kisheria kuwalinda?" Vikosi hivi vilikuwa wapi wakati Vikosi vya Msaada wa Haraka vilikiuka heshima na kupora mali? Je, vikosi hivi vipo kwa ajili ya kuwalinda wananchi au kuwakandamiza na kuwadhalilisha? Ikiwa soko litakuwa nyembamba sana, linaweza kupangwa au kuhamishwa hadi maeneo makubwa zaidi, ambayo yanapatikana kwa urahisi katika eneo hilo.
Mwenyezi Mungu Mtukufu amehalalisha biashara. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):
[وَأَحَلَّ اللهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا]
“Lakini Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.” [Al-Baqarah 2:275]. Lakini riba imeruhusiwa katika masoko yetu, na biashara imeharamishwa kwa visingizio na sheria ambazo Mwenyezi Mungu hakuzihalalisha. Kazi ni faradhi kwa mwanamume mwenye uwezo ili kuhudumia familia yake. Abdullah bin Amr amesema: Mtume (saw) amesema: «كَفَى بِالْمَرْءِ إِثْمًا أَنْ يُضَيِّعَ مَنْ يَقُوتُ» “Inatosha kwa mtu kuhesabiwa kuwa ni mwenye dhambi, kwa kuwapuuza wale aliowajibishwa kuwasimamia.” Ikiwa mtu hawezi kufanya kazi, ima kiuhalisia au kisheria, mambo yake yanaachiwa hazina ya Waislamu, yaani, serikali. Je, itawajibishwa vipi wakati inapiga vita watu juu ya riziki zao?!
Pia hairuhusiwi kuharibu mali ya watu sokoni kwa kisingizio chochote kile, kama vile kuenea kwa kipindupindu, kudhibiti soko, au mengineyo. Badala yake, madhumuni msingi ya dola ni kuwasaidia watu, kutimiza wajibu wake wa kuwatunza, na kuwapa ulinzi na usalama, si kuwapiga vita na kuwakatisha riziki! Wale wanaofanya kazi sokoni lazima wafuate masharti ya Sharia katika uuzaji, biashara na shughuli zengine zinazoruhusiwa. Hawapaswi kuuza bidhaa zilizoibwa, vitu vilivyoharamishwa, au vyakula vilivyoharibika. Ni lazima pia washikamane na kuhifadhi mazingira na afya ya umma, wajiepushe na kufunga barabara, na wajiepushe na ulaghai mbaya, udanganyifu, miamala ya ulaghai, riba au miamala mengine iliyoharamishwa.
Wajibu wa serikali ni kuchunga mambo ya watu na kuyasimamia masoko ili kuyadhibiti, sio kuwazuia watu, bali kuwarahisishia mambo yao katika kununua, kuuza na kufanya kazi kwa mujibu wa amri ya Mtume (saw): «فَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imam ambaye ni msimamizi wa watu ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake.”
Kinachotokea leo katika masoko ni matokeo ya kukosekana kwa Dola ya Kiislamu. Dola ya ustawi ambayo inashikamana na sheria za Mwenyezi Mungu na kutekeleza sheria yake, na ambayo mtawala wake ni mchungaji wa watu, sio mtozaji wa mali zao. Kwa hiyo, kazi makini inahitajika ili kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na kuweka kiapo cha utiifu kwa Khalifah Rashid (Khalifa aliyeongoka). Atakayesimamisha Dini na kutekeleza Shariah, na uhalisia huu mbaya na mchungu utabadilika. Kutoka kwa Al-Arbadh ibn Sariyah, amesema: Mtume (saw) amesema:
«فَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ بَعْدِي فَسَيَرَى اخْتِلَافاً كَثِيراً، فَعَلَيْكُمْ بِسُنَّتِي وَسُنَّةِ الْخُلَفَاءِ الْمَهْدِيِّينَ الرَّاشِدِينَ، تَمَسَّكُوا بِهَا وَعَضُّوا عَلَيْهَا بِالنَّوَاجِذِ»
“Kwani yeyote atakayeishi baada yangu ataona ikhitilafu kubwa, basi lazima mfuate sunnah yangu na ya makhalifa waongofu. Shikamaneni na muikamate kwa majego.”
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |