Ijumaa, 24 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mlima Geneva Umefanya Kazi Na Kuzaa Panya Aliyekufa!!

Jana, Ijumaa, Agosti 23, 2024, mkutano wa Geneva, ulioanza Agosti 14 kujadili mgogoro wa Sudan, ulihitimishwa kwa kuunda “Muungano wa Umoja wa Kimataifa” ili kumaliza vita nchini Sudan. Kwa mujibu wa Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Prillo, muungano huo unajumuisha, pamoja na Marekani, Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, IGAD, pamoja na Uswizi, Saudi Arabia, UAE na Misri. Hata hivyo, pamoja na urefu wa majadiliano ya Geneva, matokeo hayana thamani ya halisi katika kusimamisha vita vya kikatili vinavyoendelea nchini Sudan.

Soma zaidi...

Marekani Yarefusha Vita ili Kufikia Ajenda yake, Kuteketeza Watu, Miti, na Mawe - Hakuna Njia ya Kutoweka Isipokuwa Kupitia Khilafah!

Mnamo Jumapili, Agosti 11, 2024, mikutano ya Jeddah ilikamilika kati ya wajumbe kutoka serikali ya Sudan na Mjumbe Maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Periello, bila kufikia maelewano yoyote kuhusu ajenda ya mazungumzo na waangalizi. Baada ya kuregea kwa wajumbe wa mazungumzo, serikali ilitoa taarifa ikibainisha kushindwa kwa ujumbe wa Marekani kuwasukuma wanamgambo wa waasi kujitolea kutekeleza Azimio la Jeddah.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yaandaa Maandamano mjini Al-Qadarif Kutaka Kukomeshwa kwa Vita na Umwagaji damu ya Waislamu

Mnamo siku ya Ijumaa, Agosti 2, 2024, Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iliandaa maandamano katika mji wa Al-Qadarif baada swala ya Juma’a karibu na Jami’ Al-Atiq (Msikiti Mkongwe) katika Soko la Al-Qadarif. Maandamano hayo yalitaka kukomeshwa kwa vita na umwagaji damu ya Waislamu.

Soma zaidi...

Njaa: Silaha Halisi ya Ubepari Mbali na Usanii wa Kipuuzi wa Misaada ya Kibinadamu ya Marekani

Samantha Power, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), alitoa taarifa akionyesha kuzorota kwa hali ya kibinadamu katika kambi ya IDP ya Zamzam nchini Sudan. Alibainisha kuwa matumaini yametoweka, nafasi yake kuchukuliwa na hofu, kwani wataalamu kutoka mfumo wa Uainishaji wa Awamu ya Usalama wa Chakula ulithibitisha kuwa njaa imeendelea kambini humo kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Soma zaidi...

Wale Ambao Hawakufa kwa Risasi za Vita Walikufa ndani ya Makaazi ya Serikali!

Sudan Tribune iliripoti jana, Jumamosi, Julai 27, 2024, ikinukuu taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari wa Sudan, iliyosema: “Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari ilisema katika taarifa iliyopokelewa na Sudan Tribune kwamba watu waliokimbia makaazi yao mjini Kassala wanaishi kwenye mahema yaliyochakaa na kuzungukwa na maji kila upande, na watoto wao wanalia kwa njaa. Iliongeza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi, kwani watoto wawili walikufa kwa shoti ya umeme, na kuna vifo kutokana na kuumwa na nyoka na kesi zingine zisizojulikana.”

Soma zaidi...

Kongamano la Cairo Larudisha tena Utawala ule ule Uliosababisha Migogoro na Kuichana Nchi

Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita…

Soma zaidi...

Amiri Jeshi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala Anataka Kuipeleka wapi Sudan?!

Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito na Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, alisema kuwa vita vya Sudan bado viko katika hatua za awali. Al-Burhan, wakati akitoa salamu za rambirambi kwa mauaji ya afisa mmoja wa jeshi la Sudan, aliapa kuviandama Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na kuregesha haki za watu wa Sudan.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu