Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Rajab 1447 Na: HTS 1447 / 81
M.  Jumatatu, 12 Januari 2026

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Ilifanya Kisimamo na Hotuba ya Hadhara huko Nile Mashariki jijini Khartoum
(Imetafsiriwa)

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan huko Nile Mashariki jijini Khartoum walifanya, mnamo Jumamosi, 10/01/2026, kisimamo na hotuba ya hadhara ya kisiasa huko Souq Sitta. Hotuba hiyo ilitolewa na Ustadh Hammad Al-Dayi, mwanachama wa Hizb, ambapo alielezea ubora wa Ummah huu, ambao ulitimiza wajibu wake katika kuwaongoza wanadamu chini ya Dola ya Khilafah, hadi ilipovunjwa na mkoloni kafiri mnamo Rajab 1342 H. Aliukumbusha Ummah kuhusu tukio hili uchungu, na jinsi, kwa kuvunjwa Khilafah, ulivyompoteza Imam ambaye ni ngao, umoja wake na kuchanika vipande vipande, na mkoloni kafiri akapata udhibiti juu yake ili kugawanya ardhi zake.

Kisha akaendelea na ufaradhi wa kufanya kazi ya kuiregesha kama dola ya uongofu kwa njia ya Utume, na kwamba faradhi hii ya Sharia ni faradhi ambayo sote lazima tuitekeleze sasa.

Wakati wa kisimamo na hotuba, mashababu wa Hizb walibeba mabango yanayoonyesha heshima ya Ummah chini ya Khilafah, na kukumbusha tukio hilo.

Hotuba hiyo ilipokea maingiliano kutoka kwa wale waliokuwepo.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.