Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 5 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTS 1447 / 121 |
| M. Ijumaa, 22 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan
Ulikutana na Kiongozi (Amir) wa Makabila ya Hausa Mjini Port Sudan
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alhamisi, 21/5/ 2026, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Sudan, ukiongozwa na Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/ Wilayah ya Sudan, Ustadh Nasser Ridha, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mratibu wa Kamati ya Mawasiliano, walikutana na Amiri wa makabila ya Hausa katika Wilayah ya Port Sudan, Ustadh Salih Abdul Rahman, nyumbani kwake. Watu wafuatao pia walikuwepo kwenye mkutano huo:
1- Nour El-Din Mohammed, Mkuu wa Makabila ya Hausa katika Wilayah ya Bahari Nyekundu.
2- Hassan Osman Youssef, mzee wa kikabila.
3- Dkt. Abdullah Hassan Abdullah, mzee wa kikabila na profesa wa chuo kikuu.
4- Dkt. Amir Ahmad Osman, Katibu Mkuu wa kabila hilo.
Baada ya utambulisho, Ustadh Nasser Ridha alielezea kwamba lengo la Hizb ut Tahrir ni kuregeshwa kwa maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na udhihirisho wa Dini, akisisitiza faradhi ya kufikia hili na kuwaunga mkono wale wanaofanya kazi kuelekea hilo.
Pia alisisitiza uhusiano wa udugu wa Kiislamu na umoja wa Ummah na dola mbele ya mradi wa kikoloni wa kikafiri unaotaka kuuvunja Ummah kupitia umwagaji damu na ukabila.
Kila mtu alithibitisha na kusifu pendekezo hilo, akikubali kwamba watu wa Hausa wana mila ya Kiislamu ya muda mrefu na wanawakilisha ardhi yenye rutuba kwa mradi wa Kiislamu, na pia kuwa ulinzi muhimu kwa umoja wa nchi na muundo wa kijamii.
Waliukaribisha mkutano huo, wakisisitiza thamani yake na umuhimu wa ushirikiano endelevu katika mradi huu kwa manufaa ya nchi na watu wake.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |