Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
| H. 7 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTS 1447 / 122 |
| M. Jumapili, 24 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Salamu za Idd al-Adha Iliyobarikiwa
(Imetafsiriwa)
Tunafurahi, katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, kuupongeza Ummah mzima wa Kiislamu, na haswa watu wa Sudan, kwa kuwasili kwa Idd al-Adha iliyobarikiwa, tukimwomba Mwenyezi Mungu, Mtukufu, Mwenye Nguvu Zote, kuirudisha tena huku Ummah ukiwa umeungana chini ya umbo lake linalounganisha; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na umeachwa huru kutokana na minyororo ya utumwa kwa wakoloni makafiri wa Magharibi, ukiwa umebeba bendera ya mabadiliko, ili wanadamu waweze kujitolea katika ibada kwa Mola Mlezi wa walimwengu.
Tunakupongezeni licha ya kuendelea kwa vita visivyo na maana ambavyo vimeharibu mazao na vizazi, na kugeuza maisha ya watu kuwa kuzimu isiyovumilika!
Vita hivi, ambavyo vimeingia mwaka wake wa nne, huku Amerika na vibaraka wake wakiendelea kuvirefusha, baada ya Amerika kuunda hali inayofanana na mandhari ya Libya, kama maandalizi ya kutenganisha Darfur na mwili wa Sudan. Kupitia vibaraka wake, iliunda umbile sambamba huko Darfur; serikali inayofanya kazi kana kwamba ni dola, tofauti na serikali katika sehemu zengine za Sudan. Droni za Vikosi vya Msaada wa Haraka zinaendelea kuwapiga mabomu watu wasio na hatia wasio na silaha jijini Khartoum, Omdurman, na miji mingine, zikieneza uoga na hofu katika nyoyo za watu ili kuwaandaa kukamilisha uhalifu wa kutenganisha Darfur.
Hakika, wajibu wetu sote katika nchi hii tunaoteseka na watawala wake na baadhi ya wanasiasa wake ni kufahamu njama hii na kufanya kazi ya kuivuruga, kwa kuungana na wale wanyoofu na wenye ufahamu, mashababu wa Hizb ut Tahrir, kwa ajili ya kurudisha tena mfumo kamili maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itakata mkono wa Amerika na wengine kuingilia kati katika ardhi zetu. Wallahi (swt), hii ndiyo heshima ya dunia hii na thawabu bora ya Akhera.
Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akubali matendo yenu ya utiifu, na kila mwaka muwe karibu Naye (swt). Kila mwaka muwe katika kheri.
Allahu Akbar Allahu Akbar Allahu Akbar la ilaha illallah… Allahu Akbar Allahu Akbar wa lillahil hamd
Ukumbusho Muhimu: Mkusanyiko wa salamu za Idd, Mwenyezi Mungu akipenda, utafanyika katika afisi za Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan; mjini Port Sudan, Khartoum, na Al Qadharif, siku ya nne ya Idd, Jumamosi,13 Dhu al-Hijjah 1447 H, sawia na 30/5/2026, saa 11:00 asubuhi.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |