Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  1 Jumada II 1447 Na: HTY- 1447 / 09
M.  Jumamosi, 22 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Uingereza, kupitia Wafuasi wake na Mabwege wake, Imarati na Serikali ya Al-Alimi, Yamezea Mate Aden na Bahari Nyekundu, Lakini Je, Kuna Mtu Yeyote Aliye Tayari Kuifukuza?

(Imetafsiriwa)

Vyombo vya habari ndani na nje ya Yemen vilisambaza, mnamo Jumanne, 18/11/2025, habari za kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Hamish Falconer, mjini Aden; ambapo alikutana na Rashad Al-Alimi, Mwenyekiti wa Baraza la Rais lenye wanachama wanane, na waziri huyo wa Uingereza pia alikutana na Waziri Mkuu Salem bin Buraik na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Shaya Zindani, na mawaziri kadhaa, na Mwewe huyo aliandamana na Balozi wa Uingereza mjini Aden, Abda Sharif.

Waziri huyo wa Uingereza aliye ziarani alitangaza kusaidia kikosi cha Coast Guard kwa kiasi cha pauni milioni 149, pamoja na milioni 4 nyengine ambazo London iliahidi kutoa katika Kongamano la Usalama wa Baharini la Yemen liliofanyika tarehe 16/09/2025 jijini Riyadh, kwa kisingizio cha kulinda usafiri wa baharini katika Bahari Nyekundu na Bab al-Mandab; huku Mwewe huyo akizingatia kwamba ziara yake ilikuja ndani ya muundo wa kuimarisha usalama wa baharini, na alisema kwamba “msaada wa Uingereza umechangia kukabiliana na ulanguzi wa silaha na kulinda njia za usafiri wa baharini.”

Ziara yake ilikuja baada ya vitendo vyote ambavyo Abu Dhabi imechukua katika kuihudumia London; kutokana na uwepo katika maeneo na visiwa vya Yemen katika Bahari Nyekundu, Mayun na Zuqar, na Mayun katika Bahari ya Arabia, pamoja na uwepo wake huko Bosaso nchini Somalia, pamoja na udhibiti wa Tareq Afash juu ya mji wa pwani wa Mocha karibu na Bahari Nyekundu.

Je, inawezekana, enyi mnaosherehekea tarehe 30 mwezi huu kumbukumbu ya miaka 58 ya kuondoka kwa mwanajeshi wa mwisho wa Uingereza kutoka Aden, kwamba wakati huo huo mnapokea maafisa wa Uingereza, na baada ya hapo waziri wa Uingereza ambaye nchi yake ilikuja kuikalia Aden anazungumzia kuhusu ushirikiano kati ya Uingereza na Yemen, na kuhusu kutoa msaada katika kukabiliana na mateso ya watu wa Yemen?! Hakika, Uingereza, ambayo iliwaondoa wanajeshi wake kutoka Yemen, imerudi kupitia watawala hawa waovu walioendelea kujali maslahi yake, na ziara hizi za mara kwa mara kati ya watawala wa Yemen na London zinawathibitishia watu wa Yemen kwamba hawa ni wafanyikazi wa nchi za kikafiri za Magharibi, kwa hivyo inastahiki kwamba tuwatoe nje ya nchi yetu, wao na wale walio nyuma yao.

Kwa upande mwingine, kuna sura nyengine ya dola ya kikoloni ambayo maslahi yake yanagongana na maslahi ya Uingereza katika eneo hili, yaani Amerika, ambayo inasimama nyuma ya kauli za Rais wa Eritrea Isaias Afwerki mnamo 16/11/2025, kwamba kambi za kijeshi za kigeni katika visiwa vya Yemen ni tishio la moja kwa moja kwa usalama wa Bahari Nyekundu na Ghuba ya Aden, na kisingizio cha kutokuwa na utulivu… na kwamba usalama wa Bahari Nyekundu ni jukumu la nchi za eneo hili, na alitaka ushirikiano wa pamoja miongoni mwa serikali za pwani na yoyote kutochukua hatua kipeke yake. Ikifuatiwa na kutoridhika kwa Mahouthi na Kongamano la Usalama wa Baharini la Yemen, na uwepo wa Abu Dhabi kwenye visiwa vya Yemen, na tishio lake kwa Bandari ya Hodeidah, na hatua zote za Uingereza wanazoziona kama zimeelekezwa kwao na zinawalenga wao.

Kwa mara nyengine tena, mapambano ya kimataifa ya Uingereza na Amerika kudhibiti Yemen na Bahari Nyekundu yanaonekana wazi machoni, kwa kutumia vibaraka wao wote wa ndani na wa kikanda, chini ya utiifu wa serikali tawala jijini Sana'a na Aden licha ya uwezo wao wa kuwarudisha nyuma wakoloni wanaoshindana. Hizb ut Tahrir, chama cha waanzilishi ambacho hakiwadanganyi watu wake, kinawalingania watu wa Yemen na Waislamu wote kufanya kazi pamoja nayo ili kusimamisha Dola ya pili ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili kuwaunganisha Waislamu, kutabikisha Uislamu, na kukata mkono wa makafiri.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizbuttahrir.today
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.