Wananchi Wanataka Kupinduliwa kwa Serikali na Kusimamishwa kwa Utawala wa Kiislamu
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Aden, mji mkuu wa muda wa serikali ya Yemen, umeshuhudia maandamano matatu ya wanawake na wanaume katika wiki mbili zilizopita. Kutokana na mateso yanayoendelea kwa wananchi, maandamano ya hasira yamefanyika mjini Aden, wakidai huduma za msingi na kukemea hali ngumu ya maisha na huduma duni. Maandamano haya yalijumuisha kauli mbiu dhidi ya muungano wa Waarabu, serikali ya Yemeni, na Baraza la Mpito, ambalo linadhibiti mji mkuu wa muda, Aden. Maandamano haya pia yalishuhudia milio ya risasi na kukamatwa kwa baadhi ya waandamanaji. Maandamano haya yalifanywa na wanawake na wanaume kwa siku tofauti. Kilichotia fora ni kuregea kauli mbiu isemayo “Wananchi wanataka kupinduliwa kwa serikali,” ambayo inatukumbusha Mapinduzi ya Kiarabu dhidi ya ukandamizaji na udhalimu.