- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Amali na shughuli wakati wa Mwezi Mei 2026
Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan imeongeza amali zake za umma katika miezi ya hivi karibuni, ikiuhimiza Ummah kufanya kazi nayo ili kusimamisha jengo tukufu la Uislamu: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Amali na shughuli maarufu zaidi za Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan wakati wa mwezi wa Mei 2026 M zilikuwa kama ifuatavyo:
1/ Majaribio ya Ulaya Kujihusisha na Hali ya Kisiasa ya Sudan:
Tangu kuzuka kwa vita vya Marekani vya kubuniwa nchini Sudan, Ulaya imekuwa ikijishughulisha na kujaribu kuvizuia, hata kujaribu kuwaingiza watu wake kama washirika katika mazingira ya kisiasa ya Sudan. Imefanya makongamano kadhaa katika miji mikuu ya Ulaya, ikiwemo London, Paris, Geneva, na hivi karibuni Berlin mnamo Aprili 2026, kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani. Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alifichua uhakika halisi wa mapambano ya kimataifa ya ushawishi nchini Sudan katika mkutano na waandishi wa habari, akisema kwamba Ulaya si shirika la hisani, wala halijali kikweli watu wa Sudan na mateso wanayopitia kutokana na vita hivi visivyo na maana. Badala yake, lengo lake ni kunyakua madaraka kutoka kwa jeshi—vibaraka wa Amerika—na kuyakabidhi kwa vibaraka wake ndani ya vikosi vya raia. Hili linaonekana wazi katika kauli zao za kumalizia! Katika kongamano la hivi karibuni la Berlin, walidai kwamba njia hii ya kiraia inawakilisha hatua msingi kuelekea mpito kamili wa kisiasa... lakini ulaghai wa Amerika unazuia majaribio haya.
2/ Mpango wa Marshall nchini Sudan:
Mnamo Jumamosi, Aprili 18, 2026, Waziri Mkuu wa Sudan Kamil Idris alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Khartoum kwamba serikali ilikuwa karibu kuzindua kifurushi cha miradi ya kimkakati, inayoongozwa na “Mpango wa Marshall wa Sudan,” ili kujenga upya kile ambacho vita vilikuwa vimeharibu. Kujibu, Muhammad Jami' Abu Ayman, Msaidizi wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, aliandika: “Serikali inazungumza kwa ujasiri mkubwa kuhusu kukabidhi Khartoum kwa makampuni ya Marekani.” Aliongeza, “Siku hizi, viongozi wa serikali nchini Sudan wanasisitiza kuonyesha utiifu wao kwa Amerika na wanajaribu sana kutekeleza ajenda yake.” Kisha akanukuu makala ya Burhan katika Jarida la ‘Wall Street’ mnamo Novemba 26, 2025, ambapo Burhan alisema: “Sudan inataka kuwa mshirika mkubwa wa Marekani katika kupambana na ugaidi na kujenga upya miji na vijiji vilivyoharibiwa. Makampuni ya Marekani yatakuwa na dori muhimu katika ujenzi upya, uwekezaji, na maendeleo ya muda mrefu.” alionya dhidi ya maovu ya Amerika na utegemezi wake, akisema kwamba ni “dola ovu inayonyonya damu ya maskini na wala haijali."
3/ Athari za Vita nchini Sudan
Ama kuhusu athari za vita nchini Sudan, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir nchini Sudan ilimkaribisha Ustadh Nasser Ridha, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano nchini Sudan, kwa majadiliano yenye kichwa: “Vita Vinaingia Mwaka Wake wa Nne ... Sudan Inaelekea Wapi?” Alizungumzia matokeo mabaya ya kiuchumi, hali uwanjani, na mapigano yanayoendelea bila dalili za azimio la kijeshi.
Alionya kuhusu masaibu ya Sudan, kutokana na kuongezeka kwa wanamgambo, ambao wamefikia vikundi 110 vyenye silaha vinavyofanya kazi nje ya udhibiti wa jeshi. Alidai kwamba hali hii bila shaka itasababisha masaibu kwa Sudan, hasa baada ya mandhari ya Libya kuthibitishwa kutokea nchini Sudan.
4/ Mawimbi ya Mfumko wa Bei na Msimamo wa Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan
Kwa kuendelea kwa utekelezaji wa sera za kiuchumi za kibepari na kuambatana na maagizo ya taasisi za fedha za kimataifa, wimbi la mfumko wa bei mkubwa limeenea katika eneo hilo, likizidi matarajio yote, hasa ongezeko la ghafla la ushuru wa umeme. Msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan alitoa taarifa kwa vyombo vya habari, akielezea vitendo vya serikali ni kama vile mwizi anayeiba gizani, na kuelezea jinsi Uislamu unavyoshughulikia rasilimali za umma kama vile umeme na mahitaji mengine muhimu. Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan ilifanya kongamano lake la kila mwezi mnamo Mei 2, 2026, ikizungumzia mada ya “Mawimbi ya Mfumko wa Bei, Ufanisi wa Sera za Serikali, na Masuluhisho ya Kiislamu.” Kongamano hilo lilifichua sababu za kupanda kwa bei na majaribio ya serikali ya kusuasua katika masuluhisho yasiyofaa ambayo yamezidisha mateso. Pia ilifafanua uharamu wa kuagiza masuluhisho kutoka Magharibi ya kikoloni na kuwasilisha masuluhisho ya Kiislamu kwa matatizo ya kiuchumi, ambayo bila shaka yatatoa tiba ya masuala ya kiuchumi na mengineyo.
Wakati huo huo, Hizb ut Tahrir/Sudan ilifanya mkutano wake wa kawaida mnamo Mei 16, 2026, katika afisi yake mjini Al-Qadharif. Mkutano huu ulishughulikia kushuka kwa uchumi, kushindwa kwa sera ya kiuchumi nchini Sudan, na mapungufu ya kiutawala yanayoikumba sekta hii muhimu. Uliangazia uwezo wa kilimo, viwanda, na mifugo wa nchi hiyo, ukitoa data ya kutosha kuonyesha kwamba rasilimali hizi zinatosha kutatua mgogoro wa kiuchumi ikiwa dola itasimamishwa kwa kuzingatia msingi wa Uislamu mtukufu, ambaoo hutumia rasilimali kuwahudumia watu.
5/ Kuongezeka kwa Mashambulizi ya Droni na Kulenga Miji
Vikosi vya Msaada wa Haraka viliongeza mashambulizi yao ya droni, vikizirusha kutoka maeneo yaliyo chini ya udhibiti wao na kutoka nchi jirani, haswa Ethiopia, kufuatia kipindi cha utulivu wa kiasi na kuhamishwa kwa baraza la mawaziri hadi Khartoum. Kujibu, msemaji rasmi wa Hizb ut Tahrir alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akionya dhidi ya shinikizo linalotolewa na vibaraka wa Marekani na pande zinazopigana kufikia makubaliano ya amani yaliyotangazwa na Musad Boulos mara kwa mara. Taarifa hiyo iliendelea kusema kwamba makubaliano haya yanaendeleza hali ya kutokuwa na vita wala amani na hatimaye yanapelekea makubaliano ya kutenganisha Darfur na Sudan.
6/ Mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Luteni Jenerali Burhan, alifanya mfululizo wa ziara za kigeni
Mnamo Aprili 2026, akitembelea Saudi Arabia, Oman, Bahrain, na nchi zingine. Wakati huo huo, Waziri Mkuu Kamil Idris alitembelea Vatican na kisha Uingereza. Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan ilitambua umuhimu wa ziara hizi za kigeni. Msemaji rasmi wa hizb katika Wilayah ya Sudan, Ustadh Ibrahim Othman Abu Khalil, alifichua msururu huu wa shughuli za kigeni kama mapambano ya kuhalalisha serikali. Alisema kwamba Ulaya, haswa Uingereza, ilikuwa ikijaribu kunyakua madaraka kutoka kwa jeshi linalounga mkono Amerika na kuyaweka mikononi mwa wa vibaraka wake. Hili lilidhihirika katika Kongamano la Berlin, lilioongozwa na Waziri Mkuu wa zamani Hamdok, ambaye anajionyesha kama mwakilishi wa Sudan. Msemaji huyo alisema kwamba huu ni mzozo wa zamani wa Uingereza na Amerika ambao utaendelea hadi dola ya kimfumo haitasimamishwa ili kukomesha mapambano haya ya kimataifa.
7/ Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, Ustadh Nasser Ridha, afanya ziara za kuitangaza Hizb ut Tahrir
Na kwamba lengo lake ni kufufua maisha kamili ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Mkuu huyo wa kamati aliongoza ujumbe uliomtembelea Amir Jenerali wa kabila la Hausa nyumbani kwake Kassala. Amir alithibitisha umuhimu wa kuunganisha umma chini ya bendera ya Uislamu, akisisitiza hitaji la haraka la kukataa ukabila.
8. Hizb ut Tahrir/Wilayah Sudan yafanya mijadala ya kisiasa katika masoko na maeneo ya umma, ikishughulikia matatizo ya watu, ikifichua mapungufu ya masuluhisho yaliyopo, na kuwasilisha kwa nguvu masuluhisho ya kimungu yanayoletwa na Uislamu mtukufu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan
Jumatano, 3 Dhu al-Hijjah 1447 H – 20 Mei 2026 M

-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
-
Click to open image!
Click to open image!
https://hizbuttahrir.today/sw/index.php/dawah/sudan/5381.html?print=1&tmpl=component#sigProId1df406a80c

Kwa Maelezo zaidi, Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan
