Tangu kuanguka kwa dhalimu Assad mnamo tarehe nane mwezi huu, makundi ya umbile la Kiyahudi yamekuwa yakishambulia ardhi ya Ash-Sham, na ndege zake zimekuwa zikivamia anga yake kwa mashambulizi ya angani yenye nia mbaya ambayo yalilenga miji kadhaa, na maeneo ya kijeshi. Mashambulizi haya yamefika katika mji wa Deir ez-Zor mashariki mwa Syria. Mashambulizi hayo ya chuki na kihalifu yamejikita kwenye maghala ya silaha, vikosi vya ulinzi wa anga katika maeneo ya kati na kusini, vituo vya utafiti wa kisayansi wa kijeshi, na viwanja vya ndege vya kijeshi, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Al-Mazzeh viungani mwa Damascus.