- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Dori ya Wanawake katika Hizb ut Tahrir
Mnamo 1953, mwanachuoni maarufu na mwanafikra Sheikh Taqiuddin an-Nabahani aliasisi chama cha kisiasa cha Kiislamu, Hizb ut Tahrir kikiwa na lengo la kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha dola ya Khilafah. Hii ndiyo nidhamu ya utawala iliyoelezewa na dalili za Kiislamu ambayo inatekeleza hukmu za Shari’ah ya Kiislamu kwa ukamilifu juu ya mujtama, inaulinda Uislamu na kuulingania kwa wanadamu. Chama kilianzia Palestina lakini hivi sasa kimeenea ndani ya nchi zaidi ya 40 katika ulimwengu wa Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Na kinajumuisha katika safu zake wanaume na wanawake kwa usawa. Video hii inawasilisha dori, makongamano ya kimataifa na kujitolea kwa wanawake katika da’wah ndani ya chama duniani kote.
[Bofya Picha utizame Video]