Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 520
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kalima ya kutaka kupinduliwa kwa viongozi wa vikundi, kuregeshwa kwa maamuzi ya kijeshi, na kufunguliwa kwa mipaka.
Pendekezo la hivi majuzi la Mswada wa Sheria ya Mufti 2024 (Maeneo ya Shirikisho) limezua mjadala mkali kote nchini Malaysia. Tangu kusomwa kwake kwa mara ya kwanza mwezi Julai, Mswada huo umesonga mbele, ukikaribia kusomwa mara ya pili na ya tatu kabla ya kuidhinishwa kamili na bunge. Mwanzo wa Mswada huu unatokana na mjadala unaoendelea kuhusu Ilm al-Kalam (Usomi wa Kiislamu), ambao umeongezeka hivi karibuni nchini Malaysia.
Hizb ut-Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo siku ya Jumamosi tarehe 23 Rabi’ al-Akhir 1446 H sawia na 10/26/2024 M katika afisi yake mjini Port Sudan, wenye kichwa: “Mkataba wa Entebbe, Bwawa la Al-Nahdha, na watawala kupuuza maslahi muhimu ya Umma”.
Zana Chafu za Marekani katika Vita vyake dhidi ya Umma wa Kiislamu ni Watawala Vibaraka wa Waislamu na Mayahudi!
Inasikitisha kwamba Malaysia inaendelea kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na China (na pia Urusi), licha ya ukatili uliothibitishwa na ukandamizaji unaofanywa na nchi hiyo ya kikomunisti dhidi ya Waislamu wa Uighur kwa miongo kadhaa. Mbali na uhusiano wa kidiplomasia, Malaysia pia imeanzisha uhusiano mkubwa wa kibiashara na China, na kuifanya kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa nchi hiyo.
Je, hakuna miongoni mwenu Abdul-Hamid, mlinzi wa Palestina kutokana na Mayahudi… ambaye alimrudisha mwakilishi wao akiwa amekata tamaa na kushindwa, bila kupata chochote, na akamfundisha somo la hekima, akisema: “Siwezi kupeana hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina?, kwani sio mali yangu, bali ni mali ya Ummah wa Kiislamu. Watu wangu waliipigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao… Mayahudi nawabakie na mamilioni yao, kwani ikiwa Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi hapo wanaweza kuichukua Palestina bila thamani yoyote, lakini maadamu niko hai, hilo halitafanyika…”?