Enyi Madhalimu! Fungueni Macho yenu!
- Imepeperushwa katika Uzbekistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo 19 Mei 2025, kesi ya wanachama 33 wa Hizb ut Tahrir, iliyodumu kwa karibu miezi minane, ilifikia kikomo. Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama, Musayev Shukrullah alihukumiwa kifungo cha miaka 17 katika jela maalum ya utawala; Selimov Dilshod alihukumiwa miaka 16 katika gereza maalum la utawala; Watu 20 walihukumiwa kifungo cha miaka 12 katika gereza maalum la utawala; Watu 8 walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 8 na 10, 4 kati yao katika hali maalum na wengine 4 katika hali kali; na watatu waliosalia walihukumiwa kati ya miaka 4 na 5 chini ya kifungo cha nyumbani.