Jumatatu, 16 Rajab 1447 | 2026/01/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Angazo la Amali za Kimataifa za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa Khilafah 1447 H – 2026 M

Katika mwezi mtukufu wa Rajab wa mwaka huu, 1447 H (2026 M), tunakumbuka kumbukumbu ya miaka 105 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, vibaraka wa wakoloni makafiri. Dola hii ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad (saw), na Maswahaba zake Watukufu (ra). Mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) uliondolewa mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, sawia na 3 Machi 1924 M, mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir Mwalimu Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid)

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Jordan inaomboleza kifo cha mwalimu mtukufu, Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid), mwanachama wa Hizb ut Tahrir, aliyefariki Jumatano, 10 Disemba 2025, akiwa na umri wa miaka 79. Alikuwa miongoni mwa wabebaji da’wah wa muda mrefu na anayejulikana sana huko Tafila.

Soma zaidi...

Jibu la Swali: China na Ukombozi Wake Kutoka kwa Mtazamo Wake Mdogo wa Kikanda

 “China inamiliki hisia ya nguvu na mapambano, na kama lengo la China halikufungika tu na kudumisha eneo lake, na kukubali kukabiliana na Amerika kama jibu tu kwa harakati za Amerika kuelekea eneo lake, China haisubutu kupambana na Amerika katika maeneo yao ya ushawishi... na kama isingeanza kutumia ubepari katika nyanja nyingi, haswa katika uchumi... ingekuwa na sauti kubwa kimataifa, na athari yake kwa maslahi ya Amerika ingekuwa na nguvu zaidi. China kwa vyovyote vile ina hisia kali ya nguvu, na inafanya kazi ili kudumisha ubwana wa eneo lake, hata kama iko katika eneo lake...” — Kwa hivyo, je, kizuizi cha China cha mauzo ya nje ya madini adimu ya ardhini kwenda Amerika, kuyauza kwa dhamana za Hazina ya Marekani, kulisasisha jeshi lake, na kujenga jengo kubwa zaidi la kijeshi duniani kusini magharibi mwa Beijing... je, hiki si kiashiria cha ukombozi wa China kutoka kwa mtazamo wake wa kisiasa uliofungika katika eneo lake na upanuzi wa mtazamo huu kushindana na Amerika duniani kote?

Soma zaidi...

Trump Awaongoza Wafuasi wake kutoka kwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha alfajiri ya Jumanne mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza baada ya kuidhinisha rasimu ya azimio lililowasilishwa na Marekani na kuunga mkono mpango wa amani wa Trump katika sekta hiyo, na Rais Trump aliisifu kura ya Baraza la Usalama kuhusu azimio la Gaza kama wakati wa kihistoria...” (BBC, 18/11/2025). Kuhusu Azimio Nambari 2803, lilichapishwa na vyombo vya habari na lilikuwa ni idhini ya mpango wa pointi 20 wa Rais Donald Trump wa kukomesha mzozo mjini Gaza, lililotolewa mnamo tarehe 29 Septemba 2025.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu