Ijumaa, 24 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kinachapisha Barua ya Wazi kwa Majeshi ya Waislamu ili Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Takriban watu 40,000 wameuwawa mjini Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, huku serikali za ulimwengu, zikiwemo nchi za Waislamu zikitazama kama watazamaji pekee wa mauaji haya ya umwagaji damu, bila ya dhamira yoyote ya kisiasa ya kukomesha mauaji hayo. Hakika, tawala nyingi za ardhi za Kiislamu kwa miongo kadhaa zimeimarisha mkono wa uvamizi wa Kiyahudi kupitia mikataba yao ya amani, kuhalalisha mahusiano ya kidiplomasia, na ushirikiano wa kiuchumi na umbile hili la mauaji ya halaiki.

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kitengo cha Wanawake “Wito kwa majeshi kutoka kwa kina Mama, Mabinti na Dada wa Umma wa Kiislamu kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)!”

Wanawake wa Kiislamu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wameelekeza wito kwa wana wa majeshi ya Kiislamu kutekeleza wajibu wao wa Kiislamu katika kuwalinda Waislamu wa Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) kutokana na uchafu wa umbile la kiyahudi linaokalia kwa mabavu, na kukomboa kila shubiri ya ardhi hii iliyobarikiwa kutoka kwa makucha ya uvamizi huu wa kikatili.

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Tufani ya Twitter “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir yaandaa Tufani ya Twitter kwa kichwa: “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!” ili kuwanusuru wabebaji ulinganizi wenye ikhlasi wanaonyanyaswa na utawala dhalimu wa Uzbekistan.

Soma zaidi...

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kampeni “Enyi Umma; Kilio Wanacholia Wafungwa wa Dhamiri nchini Uzbekistan!”

Vyombo vya usalama nchini Uzbekistan vimewakamata tena wanachama 23 wa Hizb ut Tahrir na kuendelea na taratibu za kesi zao Mei 9 mwaka huu kwa mashtaka yale yale waliyoshtakiwa wakati wa enzi ya dhalimu aliyefariki Karimov, ambayo kwayo walitumia karibu miaka 20 jela na mateso tangu 1999 - 2000 M.

Soma zaidi...

Pongezi za Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1445 H

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake za dhati kwa Umma wa Kiislamu, wenye kulemewa na majeraha na kustahamili shinikizo la moja kwa moja na lisilo la moja kwa moja la kikoloni. Kwa mnasaba huu, tunawataja makhsusi watu wetu wenye subira mjini Gaza Hashim na kwa jumla katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, tukimuomba Mwenyezi Mungu azifanye siku za Idd hii kuwa chanzo cha utulivu wa nyoyo zao.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu