Je, Mafanikio kwa Waislamu yanaweza Kupatikana kupitia Siasa za Kidemokrasia?
- Imepeperushwa katika Siasa
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kutokana na mauaji makubwa ya halaiki yanayotokea Gaza na dori ya Marekani katika kusaidia na kuunga mkono yaendelee, kumekuwa na mijadala mingi miongoni mwa Waislamu kuhusu jinsi ya kujihusisha zaidi kisiasa na jinsi jamii ya Kiislamu inavyoweza kuwa mstari wa mbele katika kuunda siasa za Marekani ili kubadilisha dunia kuwa bora. Ndani ya mijadala hii, mengi yanasemwa kuhusu kujishughulisha na uraia, kujiunga na kuunga mkono wagombea mahususi wa kisiasa, kunyima kura zao kama aina ya adhabu, na hatimaye kupata Waislamu zaidi, au "washirika" kwenye nyadhifa katika ngazi za dola na majimbo. Kuna gumzo hata miongoni mwa kina dada wakidai kwa furaha kwamba wanajaribu kumlea kijana au binti yao kuwa Rais wa kwanza wa Marekani Muislamu. Haya yanawekwa kama mafanikio sio tu kwa Waislamu wa Amerika, lakini Waislamu kote ulimwenguni. Huu unawekwa kama mpango wa mafanikio licha ya ukweli kwamba vyama vyote vya kisiasa, iwe vya rangi ya samawati, nyekundu, au kijani vinaunga mkono umbile la Kizayuni, au dola zengine zenye kufanya mauaji ya halaiki mithili ya China na India.