Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ni Rasmi: Mamlaka nchini Tunisia Zinasaidia Amerika na Umbile la Kiyahudi katika Mauaji ya Halaiki dhidi ya Watu Wetu huko Gaza na Palestina yote

Mji wa Vicenza wa Italia ulishuhudia hafla ya kusainiwa kwa itifaki ya mwisho ya taratibu za kupanga mazoezi ya kijeshi ya Simba wa Afrika 2025 nchini Tunisia. Makubaliano hayo yalitiwa saini kati ya Kanali Mwandamizi wa Tunisia Mguidich Mejid na Kanali wa Marekani Drew Conover, Mkurugenzi wa Mafunzo wa Jopo Kazi la Jeshi la Marekani la Kusini mwa Ulaya.

Soma zaidi...

Kushiriki katika Mafunzo ya Kijeshi pamoja na Adui wetu ni Fedheha kwa Majeshi yetu na Usaliti kwa Watu wetu mjini Gaza

Mnamo tarehe 1/11/2024, Wizara ya Ulinzi ilitoa taarifa ikisema: “Tunisia itakuwa mwenyeji, kuanzia Novemba 4 hadi 15, wa zoezi la majini la kimataifa “PHOENIX EXPRESS 24”, kwa ushirikiano na Kamandi ya Marekani ya Afrika, kwa ushiriki wa takriban wanajeshi 1,100 na waangalizi wanaowakilisha nchi dada na rafiki 12, ambazo ni Algeria, Libya, Morocco, Mauritania, Senegal, Uturuki, Italia, Malta, Ubelgiji, Georgia, na Marekani, pamoja na Tunisia, nchi mwenyeji.”

Soma zaidi...

Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia kinazindua kampeni yenye kichwa “Ufisadi wa Elimu Unatokana na Ufisadi wa Serikali, na Marekebisho Yanahitaji Mabadiliko ya Utawala.”

Kwa kuzingatia mgogoro mkubwa unaoathiri sekta zote muhimu nchini kutokana na ushawishi mkubwa wa wakoloni wanaodhibiti taasisi zake kuu, kuzorota kwa sekta ya elimu kumekuwa na athari kubwa sana. Kuzorota huku kunaathiri kila mtu nchini Tunisia— kina baba, kina mama, walimu, na wanafunzi vilevile—kutokana na mshikamano wake tata na pande nyingi zinazopishana.

Soma zaidi...

Wapambe wa Utawala wa Tunisia Waruhusu Huduma za Kijasusi za Mossad na za Kigeni Kuenea Nchini humu na Kuwatesa Wanawake wa Tunisia Kwa Sababu ya Kuiunga Mkono kwao Gaza!

Katika hali inayojitokeza mara kwa mara katika matembezi mengi yanayoandaliwa na Hizb, Mashababu huhangaishwa na usalama, hasa ufuatiliaji wa wale wanaotoa hotuba wanapokuwa njiani wakirudi, ima kwa kuwaita kwenye vituo vya usalama au kuwaitisha vitambulisho vyao kana kwamba wanashukiwa kufanya vitendo vya uhalifu!

Soma zaidi...

Uchaguzi ni Njia ya Kuendeleza Mfumo wa Kisekula ambao lazima Ubadilishwe kwa Kusimamisha Khilafah

Tangu kuzuka mapinduzi ya Umma nchini Tunisia mwishoni mwa mwaka 2010, Hizb ut Tahrir imesisitiza kuwa mradi pekee wa kihadhara wenye uwezo wa kuyafanikisha mapinduzi hayo na kufikia matakwa ya wanamapinduzi unatokana na kuupindua utawala wa kisekula na badala yake kuubadilisha kwa mfumo adilifu wa kisiasa, na hili linaweza tu kufanywa kupitia Uislamu, chini ya dola moja; dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Soma zaidi...

Je, Wananchi na Jeshi la Kifahari la Tunisia Wanakubali Mapokezi ya Waziri wa Ulinzi wa wale Wanaoua Ndugu zao mjini Gaza?!

Mnamo Jumatano, Agosti 28, 2024, Jenerali Michael Langley, Kamanda wa Kamandi ya Amerika ya Afrika (AFRICOM), alisema wakati wa mkutano wake na Waziri wa Ulinzi wa Tunisia Khaled El-Suhaili kwamba Tunisia iko mstari wa mbele katika nchi za Kiafrika zenye ushirikiano wa kihistoria na wa kipekee. Marekani, ikielezea utayari wake wa kuendeleza na kupanua mahusiano haya. Ziara hii inajiri siku tatu baada ya kuapishwa kwa wajumbe wa serikali.

Soma zaidi...

Pongezi kwa Mnasaba wa Idd al-Adha al-Mubarak Kutoka Ardhi ya Zaitouna, Tunisia, hadi Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina

Huku sauti za mahujaji kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu zikipaa kwa mwito wa Mwenyezi Mungu, sauti za watu wa Gaza zimepaa tangu Kimbunga cha Aqsa katika kumwita Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo, vikosi vyote vya ukafiri na dola za kihalifu kutoka Magharibi, ambazo zina chuki dhidi ya Uislamu na watu wake, zinakula njama dhidi yao ili kuliokoa umbile katili la Mayahudi na kuupiga vita mradi mtukufu wa Kiislamu unaotokana na itikadi yetu, na kumaliza matamanio yetu ya utu na wokovu kupitia kutabikisha sheria ya Mola wetu.

Soma zaidi...

Chombo cha Usalama huko Kerkennah Kinawafuatilia Wanaotafuta Kuwaokoa Watu Wetu huko Gaza Wakitoa Wito kwa Majeshi Kuwanusuru, Na Kuwachukulia kuwa ni Washukiwa wa Uhalifu Wanaostahili Kuchunguzwa na Kukamatwa!!

Huku Gaza ikiungua mikononi mwa umbile halifu la Kiyahudi, na wanawake na watoto wakikatwa vipande vipande kikatili, katika kimya kamili kutoka kwa tawala za Kiarabu zinazosaliti na shirikishi, katika wakati ambapo Palestina; Isra na Mi’raj, Ardhi Iliyobarikiwa, cha kwanza kati ya vibla viwili, inalilia majeshi ya Waislamu kwa ajili ya hatua ya haraka kukomesha uhalifu wa mauaji ya halaiki ambao haukomi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu