Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Maimamu Hawana Wajibu wowote wa kutoa Ufafanuzi kwa Mawaziri Wanaounga Ugaidi

Waislamu na wasiokuwa Waislamu vile vile, wale walio na adabu na ubinadamu wa kimsingi, wameonyesha wazi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kwamba wanakataa kukubali kimya kimya jinai zisizoelezeka za Wazayuni ambazo serikali ya Denmark imefanya kila kitu ili kuzifinika. Huku wakiunga mkono kwa moyo wote ugaidi wa kimpangilio wa watu halali wa Palestina, wanalenga, wakiwa na kadi ya ugaidi mkononi, hasa sauti za Waislamu zinazotaka ukombozi wa Palestina.

Soma zaidi...

Mwanachama Mwengine wa Hizb ut Tahrir Atiwa hatiani kwa Kutoa Wito wa Ukombozi wa Palestina: Historia Itakumbuka Neno la Kweli na Wahalifu wa Kweli

Siku 303 baada ya mauaji ya halaiki ya Wazayuni yanayoungwa mkono na Denmark dhidi ya raia wa Gaza, hukumu nyengine imetolewa katika Mahakama ya Wilaya ya Copenhagen dhidi ya mwanachama wa Hizb ut Tahrir kwa kutoa wito wa ukombozi wa kijeshi wa Palestina.

Soma zaidi...

Hakuna Uamuzi wa Kisiasa wa Mahakama Utakaositisha Wito wa: “Israel” Lazima Iondolewe na Palestina Yote Ikombolewe

Mnamo siku ya Jumanne tarehe 25/6/2024, nilihukumiwa kifungo cha nje siku 60 katika Mahakama ya Jiji la Copenhagen kwa kutoa wito wa ukombozi wa Palestina. Jaji anayeendesha kesi aliamua wakati wa kutoa hukumu kwamba hotuba yangu ya 2021 katika suala hilo haikuelekezwa kwa Mayahudi kama kundi la kidini, lakini alitoa wito wa kuondolewa kwa umbile haramu la Kizayuni linaloitwa “Israel” kupitia uingiliaji wa kijeshi. Wito huu ulitangazwa na mahakama ya jiji kuwa sio halali!

Soma zaidi...

Kesi ya Kisiasa Inafichua Uungaji Mkono wa Denmark kwa Uvamizi wa Mauaji ya Halaiki

Serikali ya Denmark inaendelea na uungaji mkono wake wa dhati kwa uvamizi wa Kizayuni wa Palestina na mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza, ambayo yameitia hofu kila nafsi adhimu katika sayari hii, na kuwaamsha watu kuona kwamba vima vinavyodaiwa vya dola za Magharibi vimezikwa na maiti hizo za maelfu ya wanawake na watoto chini ya magofu ya Gaza. Haki za binadamu, haki ya kuishi na kujiamulia, haki za wanawake na ustawi wa mtoto - yote haya yanatupwa chini ya tingatinga la Uzayuni na wanasiasa na mamlaka, ambao kwa hivyo wanaonyesha unafiki wao wa hali ya juu na kufichua jinsi gani "vima" hivi kivitendo ni ala tu za kisiasa.

Soma zaidi...

Marufuku ya Uingereza juu ya Hizb ut Tahrir: Udhibiti wa Kutapatapa na Unafiki wa Hali ya Juu

Leo, Januari 19, 2024, Hizb ut Tahrir imepigwa marufuku nchini Uingereza kwa uamuzi wa kisiasa pasi na kivuli cha mchakato wa kisheria. Marufuku hiyo ilianzishwa siku nne tu baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, James Cleverly, kutangaza kwamba angeiongeza Hizb ut Tahrir kwenye orodha ya magaidi ya Uingereza.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu