Jumatatu, 20 Rajab 1446 | 2025/01/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Wito kwa Waislamu kwa Jumla, na kwa Watu wa Ash-Sham Hasa

Enyi Waislamu kwa jumla, na watu wa Ash-Sham hasa: Kiongozi wa Hizb ut Tahrir, asiyewadanganya watu wake, anakuonyeni juu ya mikono ya mashetani wa wanadamu wanaotaka damu yenu imwagike bure, ili msifikie wema msafi na dhahiri, kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, bali hukmu iliyotungwa na mwanadamu lakini yenye jina na maana tofauti. Badala ya kuwa Umma ambao makafiri wanauchukulia kwa uzito, mumerudi kuwa wafuasi wa makafiri wakoloni na vibaraka wao, na huu ni uhalifu, Mwenyezi Mungu aepushie mbali, ambao hatima yake ni udhalilifu duniani na adhabu kali kesho Akhera.

Soma zaidi...

Marekani, kupitia Usitishaji vita, Inafikia Malengo Mawili Muhimu kwa Uvamizi wa Kiyahudi: Kuondolewa kwa Vikosi vya Hezbollah vinavyoungwa mkono na Iran Kaskazini mwa Mto Litani, na Kutenganishwa kwa Pande Mbili!

Mnamo tarehe 27 Novemba 2024, usitishaji vita ulitangazwa katika upande wa Lebanon kati ya umbile la Kiyahudi na Hezbollah. Moja ya masharti yake ilikuwa kwamba umbile la Kiyahudi lingeondoa jeshi lake linalovamia kutoka kusini mwa Lebanon ndani ya miezi miwili, huku Hezbollah ingerudisha nyuma majeshi yake kaskazini mwa Mto Litani. Makubaliano hayo pia yalivipa vikosi vya Kiyahudi uhuru wa kutembea kusini endapo chama hicho kitakiuka makubaliano hayo, sambamba na kuendelea na safari za ndege za adui katika anga ya Lebanon kwa ajili ya uchunguzi na ujasusi.

Soma zaidi...

Enyi Wanajeshi wa Kiislamu, Je, Hakuna Salahuddin Mpya Miongoni Mwenu? Kukuongozeni Katika Kuwanusuru Mashahidi na Kuliondoa Umbile la Kiyahudi?

Je, hakuna miongoni mwenu Abdul-Hamid, mlinzi wa Palestina kutokana na Mayahudi… ambaye alimrudisha mwakilishi wao akiwa amekata tamaa na kushindwa, bila kupata chochote, na akamfundisha somo la hekima, akisema: “Siwezi kupeana hata shubiri moja ya ardhi ya Palestina?, kwani sio mali yangu, bali ni mali ya Ummah wa Kiislamu. Watu wangu waliipigania ardhi hii na kuinywesha kwa damu yao… Mayahudi nawabakie na mamilioni yao, kwani ikiwa Dola ya Khilafah itasambaratika siku moja, basi hapo wanaweza kuichukua Palestina bila thamani yoyote, lakini maadamu niko hai, hilo halitafanyika…”?

Soma zaidi...

Enyi Watawala wa Nchi za Waislamu... Hamuoni Aibu? Je, Hamuogopi Kufedheheka hapa Duniani na Adhabu Kesho Akhera? Je, Hamuelewi?

Enyi askari katika ardhi za Waislamu: Je, hakuna miongoni mwenu mwenye hekima? Ambaye anawaongoza askari, hasa kutoka katika nchi ya Misri (Kinanah), Ash-Sham na ardhi ya Al-Fatih, ili majeshi yaliyosalia yamfuate, yakiimba Allahu Akbar, ili Ummah ufuate Takbira hizo nyuma yao kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt)?

Soma zaidi...

Baraza la Usalama liko “Mfukoni mwa Marekani” Likiendeshwa na Maslahi yake na Maslahi ya Mayahudi na Wakoloni wa Makafiri

Mnamo tarehe 11/6/2024, Baraza la Usalama lilitoa azimio la kuunga mkono mradi wa Biden kwa ajili uvamizi wa kikatili wa Kiyahudi dhidi ya Gaza, bali Palestina yote! Maandishi ya azimio hilo, kama yalivyochapishwa na CNN, mnamo tarehe 11 Juni 2024, yalisema yafuatayo: (Baraza la Usalama “linakaribisha pendekezo jipya la kusitisha mapigano lililotangazwa mnamo Mei 31, ambalo lilikubaliwa na ‘Israel,’ na kutoa wito kwa Hamas pia kulikubali, na kuzitaka pande husika zikubali kutekeleza masharti yake kikamilifu bila kuchelewa na bila masharti.”

Soma zaidi...

Enyi Waislamu: Mnaona Jinai za Mayahudi kwenye Kivuko cha Rafah, Gaza na kwa hakika Palestina yote. Na Watawala Hawapeleki Jeshi kwa ajili ya Kunusuru; Badala yake Wanapuuza Mistari yao Mekundu! Wameridhika na Upatanishi wa Marekani na Wafuasi wake!

Enyi Waislamu: Inatosha sasa. Ukatili unaofanywa na Mayahudi kwa watu, miti na mawe hauhesabiki! Sasa wanavamia kivuko cha Rafah, ambacho utawala wa Misri ulikichulia kuwa mstari mwekundu ambao haungekaa kimya kuhusu uvamizi dhidi yake.

Soma zaidi...

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37]

Mnamo Jumamosi, 11/11/2023, takriban watawala sitini wa Kiarabu na wasiokuwa wa Kiarabu wa nchi za Waislamu walikutana jijini Riyadh kujadili uvamizi wa Mayahudi dhidi ya Gaza, yaani zaidi ya mwezi mmoja baada ya uvamizi wa Mayahudi kuanza, na baada ya mashahidi zaidi ya elfu kumi na moja na Karibu elfu thelathini kujeruhiwa.

Soma zaidi...

Enyi Askari katika Majeshi ya Waislamu, “Hivyo, hamna hata mtu mmoja miongoni mwenu aliye ongoka?” [Hud:78]

Ni karibu mwezi mmoja sasa tangu uvamizi mkubwa wa wanyakuzi wa Kiyahudi huko Gaza, pamoja na Ukingo wa Magharibi, na Lebanon. Wamewauwa watu, wazee, wanawake na watoto, na wameharibu miti na mawe katika vitendo vilivyo zidi uhalifu wote na zaidi ya aina yoyote ya uvamizi! Ilhali watawala bado wamekaa kimya, na wanapozungumza, ni kuhesabu idadi ya waliokufa shahidi, kujeruhiwa, na maeneo yaliyoharibiwa.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu