Ujasiri Wenu Kwa Mwenyezi Mungu, Enyi Madhalimu, Unatangaza Kukaribia Mwisho Wenu
- Imepeperushwa katika Palestina
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wakati Mayahudi walipokuwa wakiizingira Hospitali ya Kamal Adwan mjini Gaza, kisha kuivamia, kisha kuichoma moto, na kuwapeleka wagonjwa, majeruhi, na wafanyikazi wa matibabu kwenye hatima isiyojulikana hadi wakati wa kuandika taarifa hii, badala ya mamlaka hiyo kulaani uhalifu wao, badala ya kuuchochea ulimwengu dhidi ya vitendo vyao viovu na vya kikatili, badala ya kuuhamasisha Umma wa Kiislamu kuwanusuru watu wa Gaza, badala ya kuona haya kwa heshima ya majeraha ya Gaza na Ukingo wa Magharibi, walikataa kufanya chochote isipokuwa kuwa Jenin, wakifanya matendo ya Mayahudi na kuwanyanyasa watu wa Palestina mithili Mayahudi wanavyowanyanyasa.