Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Amali za Kilimwengu za Hizb ut Tahrir katika Kumbukumbu ya Kuvunjwa kwa Khilafah 1446 H – 2025 M
- Imepeperushwa katika Kampeni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika mwezi wa Rajab Mtukufu mwaka huu 1446 H - 2025 M, tunakumbuka kumbukumbu mbaya ya miaka 104 ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu na wahalifu wa Waarabu na Waturuki, ambayo ilianzishwa na Bwana wa Mitume, Muhammad, rehma na amani ziwe juu yake, na Maswahaba zake watukufu na waliobarikiwa, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, na kuondolewa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) mnamo tarehe 28 Rajab Tukufu katika mwaka wa 1342 H sawia na tarehe 3 Machi 1924 M mikononi mwa mhalifu Mustafa Kemal. Kutokana na hili, Hizb ut Tahrir inaandaa amali mbalimbali za umma katika nchi zote ambazo inaendesha shughuli zake za kuwahamasisha Waislamu kufanya kazi kwa bidii ili kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.