Tofauti Kubwa Kati ya Azimio la Istanbul na Fatwa Zilizotangulia!
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mwishoni mwa kongamano lao waliloliita “Gaza ni Jukumu la Kiislamu na la Kibinadamu” lililofanyika jijini Istanbul kwa siku sita la maulamaa, lililoandaliwa na Erdogan, walitoa tamko la mwisho. Walianza na aya za Qur’an kuhusu maandalizi na Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), ili kwamba yeyote anayeisoma afikirie kwamba kitakachofuata kingekuwa ni programu ya kivitendo ya jinsi ya kujishughulisha mara moja na Jihad ambayo sio tu inaiondolea Gaza bali pia inaikomboa Palestina na al-Masjid al-Aqsa. Hata hivyo, uhalisia ulikuwa kinyume.



