Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Trump Awaongoza Wafuasi wake kutoka kwa Watawala katika Ardhi za Waislamu kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!
(Imetafsiriwa)

“Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitisha alfajiri ya Jumanne mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu Ukanda wa Gaza baada ya kuidhinisha rasimu ya azimio lililowasilishwa na Marekani na kuunga mkono mpango wa amani wa Trump katika sekta hiyo, na Rais Trump aliisifu kura ya Baraza la Usalama kuhusu azimio la Gaza kama wakati wa kihistoria...” (BBC, 18/11/2025). Kuhusu Azimio Nambari 2803, lilichapishwa na vyombo vya habari na lilikuwa ni idhini ya mpango wa pointi 20 wa Rais Donald Trump wa kukomesha mzozo mjini Gaza, lililotolewa mnamo tarehe 29 Septemba 2025.

Masuala hatari zaidi yaliyotajwa katika azimio hilo la Baraza la Usalama ni manne:

1- Kuanzishwa kwa Bodi ya Amani (BoP) kama utawala wa mpito wenye shakhsiya ya kisheria ya kimataifa unaochukua mfumo na kuratibu ufadhili wa kuijenga upya Gaza kulingana na mpango kamili na kwa mujibu wa kanuni za sheria husika za kimataifa, hadi Mamlaka ya Palestina ikamilishe mpango wake wa mageuzi.

2- Utekelezaji wa utawala wa mpito, ikiwa ni pamoja na usimamizi na usaidizi kwa kamati ya kiufundi ya Palestina isiyo ya kisiasa inayoundwa na watu waliohitimu kutoka kwa wakaazi wa Ukanda huo.

3- Inaziruhusu nchi wanachama zinazofanya kazi na Bodi ya Amani na bodi yenyewe kuanzisha Kikosi cha muda cha Udhibiti wa Kimataifa (ISF) mjini Gaza kilichounganishwa chini ya amri moja inayokubalika na Bodi ya Amani, pamoja na michango kutoka kwa dola zinazoshiriki… pamoja na kikosi kipya cha polisi wa Palestina kilichofunzwa na kuchunguzwa, ili kusaidia kulinda maeneo ya mpakani; na kuleta utulivu katika mazingira ya usalama mjini Gaza kwa kuhakikisha silaha zinaondolewa katika Ukanda huo, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya kijeshi, kigaidi, na mashambulizi na kuzuia ujenzi wake upya.

4- Inaamua kwamba Bodi ya Amani na uwepo wa kimataifa wa kiraia na usalama ulioidhinishwa chini ya azimio hili utabaki na mamlaka hadi tarehe 31 Disemba 2027, kwa mujibu wa hatua yoyote inayofuata ya baraza na kwamba itachukua hatua za kuwezesha harakati za watu wanaoingia na kutoka Gaza kulingana na mpango kamili… na inaiomba Bodi ya Amani kuwasilisha ripoti ya maandishi kwa Baraza la Usalama kila baada ya miezi sita kuhusu maendeleo yaliyofanywa katika suala hili.

Enyi Waislamu: Mtu yeyote anayezingatia azimio hili la Baraza la Usalama hahitaji kufikiria kwa kina ili kutambua kwamba ni tangazo la usimamizi na ukoloni juu ya Gaza, kwani linajumuisha uundaji wa chombo kinachotawala (Bodi ya Amani), na chombo hiki kinaanzisha Kikosi cha Utulivu cha Kimataifa, na chombo na kikosi hicho kinachoanzisha kinaendelea kwa zaidi ya miaka miwili, yaani, hadi 31/12/2027, na hii si kikomo cha mwisho lakini kinakabiliwa na hatua yoyote inayofuata ya baraza! Zaidi ya hayo, chombo hicho pia kinaanzisha “utawala na idara ya mpito” na inasema kwamba kisiwe cha kisiasa kukiondoa katika masuala ya utawala... na si hivyo tu, bali chombo hiki kinadhibiti harakati za watu wanaoingia na kutoka Gaza!! Ikimaanisha kwamba azimio hili ovu ni zaidi ya usimamizi na ukoloni!

Enyi Waislamu: Azimio hili la Baraza la Usalama halikuzaliwa kutokana na wakati huo bali lilibuniwa na Trump kwa idhini ya wafuasi wake kutoka kwa watawala katika ardhi za Waislamu tangu mkutano wa Umoja wa Mataifa mnamo Septemba 2025, ambapo Trump aliongoza mkutano huo uliojumuisha Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan, kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mnamo Jumanne, 23/9/2025, akiuelezea kama mkutano muhimu zaidi, kisha akawasilisha—au akaweka—juu yao mpango wa pointi 20, na pointi ishirini za mpango wake zilizungumzia kupotea kwa Gaza na usimamizi na ukoloni wake, na kuifanya Gaza kuwa bustani inayofurahiwa na Trump na washirika wake wa Kiyahudi! Kisha baada ya hapo, Sisi alifanya sherehe katika ardhi ya Kinana kwa Trump na mpango wake muovu wa kuipoteza Gaza chini ya utawala wa Trump na mwenzake Netanyahu na watawala Ruwaibidha (watepetevu na duni) katika ardhi za Waislamu walifurahia utiifu wao kwa Trump na katika kutekeleza mpango wake! Na watawala hawa walisahau—au walijifanya kusahau—kwamba utiifu wao kwa makafiri ni jinai inayosababisha udhalilifu katika dunia hii na Akhera:

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللَّهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An'am:124].

Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu: Je, damu yenu haimo kwenye mishipa yenu wakati Gaza Hashem inanunuliwa na kuuzwa huku mkitazama na kusikiliza? Je, hamutamani mojawapo ya matokeo mawili mazuri mnaposhuhudia mauaji ya Mayahudi dhidi ya watu wa Gaza—watoto, wazee, na wanawake? Je, hamulipizi kisasi misikiti, shule, na hospitali ambazo zimepigwa mabomu na kuharibiwa kwa wale wanaotafuta hifadhi ndani yake kwa uvamizi wa kikatili ambao umelenga kila kitu mjini Gaza—watu, miti, na mawe? Je, hamutamani heshima ya dunia hii na Akhera, ili mumnusuru Mwenyezi Mungu na Yeye akunusuruni?

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ * وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْساً لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu. * Na walio kufuru, basi kwao ni maangamizo, na atavipoteza vitendo vyao.” [Muhammad:7-8].

Je, nyinyi enyi wanajeshi katika majeshi yaWaislamu hamna uwezo wa kuwafuata wale wanajeshi wa Uislamu waliokuwa kabla yenu na kuikomboa Palestina na Gaza Hashem? Ndiyo, hakika mnao uwezo, kwani mnalizunguka umbile la Kiyahudi kama bangili kwenye kifundo cha mkono, lakini mnahitaji kiongozi mwenye ikhlasi na mkweli! Je, hakuna kiongozi kama huyo miongoni mwenu ambaye angewaongoza kupigana na adui yenu ambaye amepigwa uhdalilifu na mateso, na ambaye hashindi katika kupigana dhidi yenu?:

[وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i 'Imran:111]. Kisha kiongozi kama huyo awaongoze wanajeshi wa Uislamu kuikomboa Gaza Hashem, Qiblah cha Kwanza, na Msikiti wa Tatu katika Misikiti Miwili Mitakatifu, na mwangwi wa ushindi wa takbira ungevuma kama walivyofanya na al-Faruq wakati wa ufunguzi, na Salahuddin wakati wa kukombolewa kwa Bayt al-Maqdis, na Abdulhamid wakati wa kulinda Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na uovu wa Mayahudi… na kisha kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ…» “Mtapigana na Wayahudi na mtawaua…” (Imesimuliwa na Muslim katika Sahih yake).

Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu: Gaza inatafuta nusrah yenu (msaada), kwa hivyo inusuruni:

[وَإِنِ اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Al-Anfal:72]. Kwani mambo yamepita mipaka yote hadi yalipofikia usimamizi na ukoloni! Na utiifu wenu kwa watawala wenu katika kutopigana na adui yenu ili kuirudisha Ardhi Iliyobarikiwa, ardhi ya Isra’ na Mi‘raj, kwenye nyumba ya Uislamu—utiifu huu utawaletea fedheha katika dunia hii na adhabu chungu kesho Akhera… hata watawala mnaowatii watakukaneni... na kisha mtajuta, wakati majuto hayatakuwa na faida:

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]

Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao. * Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqarah:166-167].

[إنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf:37]

H. 28 Jumada I 1447
M. : Jumatano, 19 Novemba 2025

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu