Jumatano, 11 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Misimamo Mikali Ni Njama Ya Kirasilimali Kuwapiga Vita Waislamu Na Uislamu Safi

Umma Wakiislamu unazidi kusononeka na kukaribia kukata tamaa kutokana na dhulma na mahangaiko wanayopitia kila uchao. Dhulma hizi zikiwa zinatokana na miito kama “Vita dhidi ya Ugaidi”, “Vita Dhidi ya Misimamo Mikali” nk… ambayo imepelekea Umma wa Kiislamu kuhisi machungu yasiyostahiki hata wanyama na miti kupitia! Miito hii hutumika kuendeleza dhulma dhidi ya Umma wa Kiislamu.

Ili kuweza kufahamu na kupata uhalisia wa mambo ni vyema kujiuliza ni nini maana ya miito hii. Amma nini Ugaidi tayari limejadilliwa sana. Amma Misimamo Mikali ndio linalopigiwa debe kwa sasa. Nini Misimamo Mikali? Misimamo Mikali kwa mujibu wa sayansi ya kisiasa inamaanisha msukumo unaolenga kubadilisha jamii na mabadiliko hayo yawe ni kupitia njia za mageuzi (www.vocabulary.com). Pia humaanisha kuathiri au kubadilisha msingi asili (mapenduzi) wa jambo/kitu. Kwa hivyo neno lenyewe kibinafsi halileti maana ya jambo zuri au baya, bali matumizi yake pamoja na maneno mengine ndio itakayo julisha uzuri au ubaya wa kilicholengwa. Amma kwa miaka ya karibuni neno hili limepewa istilahi mpya iliotoka kutoka vitengo vya usalama vya Marekani na Yuropa kumaanisha wenye kulenga mapinduzi ya kimsingi kwa miondoko ya kijamii ilio zoeleka kupitia misimamo itakayo pelekea fujo na umwagikaji wa damu. Wakafanya majina haya- Ugaidi na Misimamo Mikali kuwa ni sawa yakitumiwa kuchafua wale wanaolenga kuleta mabadiliko katika ulimwengu. Na kwa kuwa hakuna waliobeba mfumo wa kimaisha tofauti na unaotawala sasa wa Kirasilimali uloharibu mazingira wa Mwanadamu kuishi, iwe ni kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiilimu nk… ila Waislamu na mfumo wao wa Uislamu wanaouamini na kuulingania usimame badala wa huu ulioko, wamebandikizwa jina kuwa ni wenye Misimamo Mikali kama walivyo bandikwa jina kuwa ni Magaidi. Haya si mageni kwani katika historia ubandikizaji wa majina ili kuhalalisha dhulma dhidi ya watu limekuwa likijirudia mara kwa mara. Kenya yajifanya kusahau historia yake pale Mabepari wa Kiengereza walipoitawala na kuwapa walowezi ardhi ilio na rutuba nzuri na kuwafurusha wenyeji wakaishi mwituni. Dhulma zilipozidi wenyeji wakasimama kimakundi makundi kutetea haki na ardhi zao, ikiwemo Mau Mau ambao ndio lilikua kundi kubwa na lenye kutishia umakinifu wa Ubepari wa Waengereza hapa Kenya. Ili kupambana na kundi hilo Serikali ya Kiengereza iliamua kutia hofu jamii hio kwa kutekeleza mauaji ya kiholela, na yalifanyika haya baada kulitangaza kundi hilo kuwa ni la Kigaidi! Bali hawakutosheka hapo, wale walioshikwa na jeshi la Kiengereza walipelekwa kwa Daktari mkuu wa akili, J.C. Carothers, ambae kuwa baada ya uchunguzi alidai ana ushahidi wa kisayansi kuwa mwamko wa Mau Mau dhidi ya Waengereza si wa kisiasa bali ni kutokana na upungufu wao wa akili! Ukitaka kumuua Mbwa mwite koko!

Hivyo twaona kuwa Misimamo Mikali ni pazia inayotumika moja kwa moja kumlenga Muislamu yeyote na popote alipo bora tu awe anapodai mabadiliko ima ni ya kibinafsi au kama jamii kupitia Uislamu wake kama mfumo kamili wa Maisha! Hii ikiwa ni jambo lakutarajiwa maanake kiasili tangu kuumbwa ulimwengu na kuwekwa binadamu na uhai ndani yake basi kuna mapambano kati ya Haki na Batili yanayoendelea mpaka Yaumul Qiyama. Lakini kwa karne hii na mwishoni mwa karne ya kabla ya hii kumeshuhudiwa mapambano mazito kati ya Uislamu kama mfumo utokao kwa Muumba dhidi ya Mfumo Batil wa Urasilimali unaotokamana na akili finyu za binadamu hususani kutoka magharibi! Mapambano haya yanaendelea kiasi kwamba Urasilimali ambao unadhaminiwa na kupigiwa debe ulimwenguni kote na Marekani na washirika wake kupitia miito ya Uhuru, Demokrasia, Soko Huru n.k; ambao kufikia sasa wameshindwa kudhibiti wimbi linalodai mageuzi ya kupitia Mfumo wa Haki wa Uislamu baada ya kuuona kuwa Urasilimali umefeli kuwasimamia wanadamu ulimwenguni kote. Kwa sababu ya mapambano haya imeipelekea Marekani na washirika wake kubuni sheria, mbinu au sera zinazolenga kusitisha au kutia kikwazo katika kasi ya wanaotaka mageuzi kupitia Uislamu kama mfumo; hivyo kukabuniwa miongoni mwa sera ni Kupambana na Ugaidi, Kupambana na Misimamo Mikali n.k. Mbinu na sera hizi zimewagawanya Waislamu katika makundi ikiwemo wale wanaokubali kutenganisha Dini na maisha, misingi ya Uhuru inaozalisha ushoga, uzinifu, utumiaji wa vileo nk, Uchaguzi wa kilaghai wa kiDemokrasia n.k kuwa ni ‘Waislamu Poa” na Waislamu wanaopinga yote hayo kwa kujifunga na Uislamu wao ima kibinafsi au kama Jamii na kuulingania Uislamu kama Mfumo na kufanya mikakati ya Kusimamisha Serikali ya Kiislamu ya Khilafa kwa njia ya Utume ili isimamie hali za walimwengu na iendeshe mambo kwa mujibu wa Al-Qur’an, Sunnah, Ijmaa Sahaba na Qiyas basi wao huitwa “Waislamu Wenye Misimamo Mikali”.

Hapa nchini Kenya baadhi ya Sheria, Mbinu au Sera ambazo Serikali imepitisha ni pamoja na:

Sheria ya Kukinga Ugaidi ya 2012 “Prevention of Terrorism Act 30 of 2012”
Sheria ya Usalam (Mabadiliko) ya 2014 “Security Laws (Amendment) Act, 2014”
Mikakati ya Kitaifa ya Kupambana na Misimamo Mikali “National Strategy to Counter Violent Extremism”
Balozi Maalumu ambaye pia ni Msimamizi wa Kituo cha Kupambana na Ugaidi na Misimamo Mikali – Kuhudhuria Kongamano la Kumi na Sita la Kimataifa lililoandaliwa na Taasisi ya Kimatiafa ya Kupambana na Ugaidi “International Institute for Counter-Terrorism (ICT) 16th International Conference” – 13 Septemba, 2016, Sharon Hotel, Herzliya ‘Israel’

Kutokana sheria, mbinu au sera hizo kumetokea dhulma za kila aina dhidi ya Umma wa Kiislamu Ulimwenguni na hapa nchini Kenya. Hali ni ya kusikitisha mno tukiangalia yanaowafika Waislamu nchini Syria, Palestine, Afghanistan, Uzbekistan, Jordan, Iraq, Burma, Yaman n.k wote wanapitia hali ngumu ikiwa ni juu ya pazia iliyomakinishwa na kupigiwa debe ulimwenguni kote kama “Kampeni Dhidi ya Misimamo Mikali na Ugaidi” ilhali nchi zinazokubali kubebeshwa na kushiriki kikamilifu katika Kampeni hiyo hatari wakipewa mabilioni ya pesa ikiwemo Kenya ambayo hivi sasa ishapokea zaidi ya Bilioni Ksh.20 za kupambana na Ugaidi pamoja Misimamo Mikali!

Madhila haya yanawakumba Waislamu lakini lakushangaza ni kuwa vyombo vya habari ambavyo jumla yao vinamilikiwa na mabwenyenye wanaokula njama na Serikali tawala pamoja na Nchi za kimagharibi kuhakikisha kuwa wanajenga mazingira munasaba ya kuhalalisha mauaji ya Waislamu na kuwapongeza na kuwasifu wasimamizi pamoja na taasisi husika za kupambana na ugaidi kwa kazi nzuri! Napia wanatumika kukuza maoni na uamsho kuwa sambamba na mapendekezo ya wadhamini wa vyombo vya habari na ndio maana kabla hata uchunguzi kufanywa utasikia vyombo vya habari vikikurupuka na kusema “Gaidi kalipua mahali fulani au tukio lakigaidi limetokea ”ilmuradi muhusika ni Muislamu!

Ndugu zenu Hizb ut-Tahrir Kenya tunawaambia musikate tamaa kwa wanayotupangia Makuffar.

(وَيَمْكُرُونَ وَيَمْكُرُ اللَّهُ وَاللَّهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ) “Wakapanga mipango yao, na Mwenyezi Mungu akapanga yake. Na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa mipango.” [Surah Al-Anfal:30]

Hakika hadhi na heshima yetu iko katika Uislamu kama Mfumo na hakuna anayestahiki kutuelekeza kuhusu Uislamu wetu isipokuwa Mwenyezi Mungu;

(الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمْ الإِسْلاَمَ دِينًا) “Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Dini.” [Surah Al-Ma’idah:3]

Enyi Waislamu:

Ni amri kwenu kutoka kwa Allah (swt) kujifunga na Uislamu kikamilifu na wala sio kuukumbatia Uislamu unaopigiwa debe na Wamagharibu kwa mtizamo wao wa Kikafiri wa Kati na Kati uliotokamana na itikadi ya kutenganisha Dini na Maisha. Uislamu unatokana na Allah (swt) na Ameuridhia juu yetu kinyume na Wamagharibi wanaouchukia na kuupiga vita kimaneno na kwa vitendo.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً) “Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu” [Surah Al-Baqara:208]

Tofauti zetu za kimakundi au madhehebu zisitupelekee kuingia katika njama tuliyopangiwa na Wamagharibi kuwa eti kuna Muislamu wa Misimamo Mikali na Muislamu Poa. Hii ni Sumu ambayo lau tutainywa basi bila shaka tutajikuta tunazozana na pia hata kupigana kati yetu ambalo ndio lengo Wamagharibi wanalolifanyia kazi usiku na mchana haswa ikizingatiwa nguvu ya Uislamu na Waislamu ni Umoja na Ushikamano wao.

Magaidi Wakuu katika Vita dhidi ya Misimamo Mikali na Ugaidi ni Marekani na ‘Israeli’ ambao ni wazi kuwa vita hivi wame walenga Waislamu na Uislamu hususan tukizingatia kuwa Makongamano makubwa yanaandaliwa na ‘Israeli’ na udhamini mkubwa wa kifedha na sera za kufaulisha maovu na njama hizo ni Muamerika.

Tunatoa nasaha kwa Waislamu na yoyote Yule anae penda haki kuwa tusizinyamazie hali hizi zinapotokea bali tuzikemee pasi na kujali watakao laumu. Na pia haitoshi kuwasubiri Viongozi wetu wa kisiasa au Mashekhe kutuzungumzia kwani twaona vipi walivyobwaga majukumu yao. Baada yakuwa hawana lakusema kutetea Umma na madhila, ambalo lenyewe ni uovu, wao hudandia kulaani washukiwa kabla ushahidi kupatikana. Na haya wanayafanya si kwa lengo lengine illa kutaka kujipendekeza kwa serikali ili wapate maslahi au kukhofia maslahi yao yasipokonywe. Haya yamejitokeza wazi katika matukio ya hivi karibuni ya kushikwa Waislamu ovyo wakiwemo wanawake na watoto na mara nyengine hata kupotezwa. Pia hatuna budi ili madhila haya yaondoke ni lazima tujitahidi kufanya ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Uislamu kupitia kusimamisha serikali ya Kiislamu ya Khilafa kwa njia ya Utume. Mauaji, Mateso katika jela za kitwaghut n.k zisiwe ni tishio kwetu bali tuziangalie kama mitihani itokayo kwa Allah s.w.t na iliyojaa kheri nyingi ikiwemo kupata pepo kwa wanaokuwa na subra ya hali ya juu. Na tusiwe na shaka na Dini yetu juu ya kurudi kwa Ngao yetu ya Khilafah kwa Njia ya Utume:

(وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لاَ يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الْفَاسِقُونَ) “Mwenyezi Mungu amewahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema. Ya kwamba atawafanyiaa makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao, na atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao.” [Surah An-Nur 24:55]

H. 24 Rajab 1438
M. : Ijumaa, 21 Aprili 2017

Hizb-ut-Tahrir

Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Demokrasia: Tumekomeka! »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu