Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kusisitiza Sheria ya Hifadhi ya Jamii ni Kupambana na Watu katika Maisha yao, Kupora Riziki za Watoto wao na Kushambulia Ukakamavuna Azma yao
(Imetafsiriwa)

Ni kwa kuna nini msisitizo huu wa Mamlaka ya Palestina (PA) wa kuhuisha Sheria ya Hifadhi ya Jamii? Je, ni kwa sababu ya wasiwasi wake kwa watu wa Palestina? Au ili kulinda ukakamavu wao na kuwatia nguvu katika Ardhi Iliyobarikiwa? Je, ni nani mnufaika halisi wa sheria hii? Je, ni wafanyikazi, waajiriwa, na waajiri, au ni wale walio madarakani?

Mamlaka ya Palestina iko katika hali ya wasiwasi na mbio za kulazimisha msururu wa sheria. Unapozichunguza sheria hizi, mtu ataona kwamba zote ziko katika kundi moja, ambalo linapiga vita Uislamu na hukmu zake na kupora fedha za watu. Madhumuni ya jinai hizi ni kudhoofisha uwezo wa watu kusimama kidete na kutekeleza Ribat (ulinzi), na kulinda na kutumikia uvamizi. Huu ndio uhalisia wa Mamlaka ya Palestina na dori yake kuu.

Watu wamesimama dhidi ya Sheria ya Hifadhi ya Jamii kwa sababu ya kushambuliwa kwa riziki zao, matunda ya juhudi zao, na maisha yao kwa kisingizio cha "kuwadhamini!", lakini PA haikukata tamaa, kwa hivyo iliregea tena kwa sababu sheria hii ingezalisha mamia ya mamilioni ya dolari kwa ajili yake, na ilikusanya nguvu zake zote na wanaume katika taasisi na vyama vya wafanyikazi ili kuipigia debe na kuwapotosha watu kwa marekebisho ya bandia ambayo hayabadilishi kiini cha toleo la awali au athari zake mbaya.

Sheria hii iko juu ya uhasi na dhuluma yake yote, na mbali na kuwa eneo lenye rutuba la wizi na ufisadi, ni kucheza kamari na pesa zenu. Kuwepo kwa Mamlaka ya Palestina, hakuna mustakabali, ubwana wake uko chini ya kapeti za uvamizi, na Rais wa PA amerudia zaidi ya mara moja kwamba atakabidhi funguo za PA kwa uvamizi huo, kwa hivyo ni nani atahakikisha dhamana? Nani anakuhakikishieni pesa zenu? Na ni nani anayelinda akiba zenu? Ni dhamana, isiyo na dhamana, wala mdhamini!

PA ni taasisi fisadi yenye ushuhuda wa watu wake na taasisi zinazoiunga mkono. madhihirisho ya ufisadi wake yako kila mahali na kashfa zilizofichwa za watendaji wake ni kubwa zaidi kuliko zile zilizochapishwa. Ina uzoefu wa aibu katika hili. Upendeleo na wizi uliathiri taasisi zote, na Mfuko wa Kitaifa wa Palestina, Mfuko wa Pensheni, Hazina ya Hospitali ya Saratani ya Khaled Al-Hassan, na Wakfu wa Izz ni ncha tu ya mlima wa barafu.

Enyi Watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa: Kuingia kwa undani wa sheria hii na marekebisho yake hakuna faida yoyote, na ni hadaa ya Mamlaka ya Palestina na kuwapotosha watu. Lakini tutatosheka kwa kuregelea 16% ambayo PA itachukua na kuiweka kwenye mfuko wa dhamana. Je, ni matokeo gani ya kiasi hiki kwa wafanyikazi, waajiriwa, waajiri na biashara ndogo ndogo? Je, madhara yake ni yapi kwa gharama za uendeshaji na bei za bidhaa na huduma? Je, madhara yake ni yapi kwa bidhaa za ndani na uwezo wao wa kushindana na bidhaa kutoka nje? Je, sheria hii itaongeza nafasi za kazi na kupunguza ukosefu wa ajira, au itakuwa ni kichocheo cha kufunga biashara ndogo ndogo na kuwasukuma wafanyikazi kufanya kazi nchini ‘Israel’? Je, matokeo yake ni yapi kwa kiwango cha maisha na kipato, au yatazidisha mapengo ya kiuchumi kati ya matajiri na maskini na kuongeza idadi ya maskini?

Sheria hii haitaathiriwa na makampuni ya ukiritimba kama vile Jawwal au Unipal...n.k., kwa sababu makampuni haya huongeza kila gharama ya ziada kwa bei za bidhaa na huduma zao ili faida zao zibaki ndani ya mipaka ambayo haipunguki kutoka kwao, na hii itasababisha kupanda kwa bei. Madhara halisi ni kwa umma kwa jumla, wafanyikazi na wamiliki wa biashara ndogo ndogo. Mishahara ya wafanyikazi na waajiriwa haiwatoshi, na wamiliki wa biashara ndogo ndogo wanatatizika kuweka biashara zao zifanye kazi, na watu wanateseka kwa gharama kubwa ya maisha, bei ya juu, na mishahara kidogo.

Sheria hii itachukua kiasi kikubwa cha pesa za watu na kuziweka mikononi mwa mabepari wachache wenye ushawishi ili wazitumie katika uwekezaji wao. Walengwa wakuu wa sheria hii ni wafisadi na mabepari wakubwa wanaohodhi masoko. Hawa ndio wanufaika wa sheria hii. Ama wafanyikazi na waajiriwa watachukua makombo hayo baada ya kunyonywa damu na kuporwa pesa. Endapo PA itaitumia sheria hii watu wataunguzwa na moto wa sheria hii katika nyanja zote za maisha, hivi itakuwaje hatma ya watu pale maslahi yao yatakapohusishwa na vyeti vya kibali kutoka kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii?

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa, Enyi Mliotukuzwa kwa Uislamu:

Maregeleo ya Mamlaka ya Palestina juu ya mfumo wa kibepari wenye ulafi katika sheria na kanuni zake zote, na utiifu wake katika maamuzi yake yote kwa nchi za Kimagharibi ambazo zina chuki dhidi ya Uislamu, ndizo zinazofanya sheria na maamuzi yote ambayo PA inayachukua, ima maamuzi ya khiyana au sheria za kidhalimu ndizo zinazoleta ugumu wa maisha ya watu wa Palestina. Muelekeo wowote ule inayouchukua; hauleti kheri yoyote.

[وَضَرَبَ اللهُ مَثَلاً رَجُلَيْنِ أَحَدُهُمَا أَبْكَمُ لَا يَقْدِرُ عَلَى شَيْءٍ وَهُوَ كَلٌّ عَلَى مَوْلَاهُ أَيْنَمَا يُوَجِّهْهُ لَا يَأْتِ بِخَيْرٍ هَلْ يَسْتَوِي هُوَ وَمَنْ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَهُوَ عَلَى صِرَاطٍ مُسْتَقِيمٍ]

“Na Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa watu wawili. Mmoja wao ni bubu, hawezi chochote, naye ni mzigo kwa bwana wake. Popote anapo muelekeza haleti kheri. Je! Huyo anaweza kuwa sawa na yule anaye amrisha uadilifu, naye yuko juu ya Njia Iliyo Nyooka?” [An-Nahl: 76]

Mamlaka ya Palestina na sheria zake ni batili na katika misingi yake na fisadi katika matawi yake yote, na kwa hivyo si sahihi kujadili marekebisho na hairuhusiwi kujihusisha na maridhiano, na chini ya jina la "uamuzi wa sheria" haramu inaruhusiwa na sheria zinabadilishwa. PA hii haiupi uzito Uislamu, matukufu, au watu, na imekaliwa na nchi za Magharibi kikamilifu. Kwa hivyo, simameni dhidi ya PA na mukatae uhalifu wake. Sheria ya dhamana si hatari zaidi kuliko sheria ya Ulinzi wa Familia au Sheria ya Ulinzi wa Mtoto au yale marekebisho ya mitaala. Badala yake, sheria hizi ni hatari na hatari zaidi kwa sababu zinalenga Dini yenu na watoto wenu. Mamlaka ya Palestina na wale walio nyuma yake wanatekeleza vita vilivyojumlisha kila kitu dhidi yenu, wakilenga Dini yenu, watoto wenu, familia zenu, fedha zenu, na maslahi yenu, na lengo kuu la haya yote ni kulinda umbile la Kiyahudi na kulipa uwezo ndani ya Ardhi Iliyobarikiwa.

Enyi watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina:

Uislamu mtukufu, ambao Utawala wa Palestina na watu wake wameupa mgongo, umedhamini haki za watu wote kwa nafasi zao kama raia wa dola bila kujali dini, kabila na rangi, umewahakikishia mahitaji yao ya kimsingi ya chakula, vinywaji, mavazi, nyumba, matibabu na elimu. Umebainisha hukmu za Shariah zinazohakikisha kutokomeza umasikini, na hukmu za Shariah zinazohusu masuala ya riziki kwa vijana, wazee, walemavu na wanawake. Umeilazimu dola kufanya kazi ya kuwasaidia wananchi katika kupata mahitaji ya ziada kadri inavyowezekana. Hakuna namna ya kuishi kwa staha isipokuwa chini ya Uislamu na hukmu zake, kwa hivyo tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaalie Khilafah Rashida kwa njia ya Utume yenye kuuweka Uislamu kivitendo, inayoondoa umasikini, inayofanya uadilifu kwa waja, na kuwatunza kwa haki ya uangalizi, na kuzikomboa ardhi na watu kutoka katika uvamizi na vyombo vyake miongoni mwa vibaraka na watawala madhalimu, na kufikia utulivu, usalama na maisha ya staha kwa watu, na kuwaepusha na mfumo mbaya wa kibepari ambao umeleta maafa juu ya wanadamu wote.

H. 1 Dhu al-Qi'dah 1444
M. : Jumapili, 21 Mei 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu